List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

duh!!!
ina maana mzee Shein hana kazi za kufanya au kudeal na Ze Comedy ndo part ya majukumu yake?
GN ebu tupatie ratiba nzima ya Mh. Zitto sisi twende tukasiskilize nondo za maana.
 
Kuna watu walishasema yeye ni Mzee wa kutembea na mkasi kwa ajili ya kukata utepe wa kuzindua mambo mbali mbali. Akichoka kuzindua ndipo anaenda kuangalia mdebwedo na kufungua matamasha/warsha/semina/makongamano na mengineyo ya jinsi hiyo. Kwa kweli post hiyo inaweza kumdumaza mtu maana hata haieleweki iko ikoje!
 
mwendapole... yeah.. wasingefanya haraka kama hivyo.. wangeyafanya sometimes next week baada ya kuhakikisha kuwa mikoa yote imo ndani.. na yangefanyika kwenye makao makuu ya mikoa yote... Sipendi mambo ya kuharakisha.. yakosa real organization... wangejiandaa kwa karibu wiki hivi...
 
makamu wa Rais DR.Shein mvuto hana,mvuto wake naweza nikaufananisha na mwenge wa uhuru siku hizi,maana ili upate watu lazima wananchi walazimishwe kutokwenda mashambani,na wachaga wafunge maduka,kutishiana faini na nzagu.
tumemuachia kazi ya kutembea na mkasi mfukoni tu ili awe anafanya uzinduzi wa matundu ya vyoo,nk.sijui kama hua anakumbuka kuunoa.
huyo hata iweje sio tishio.kwanza kitakachofanyika ni kuuwekea zengwe mkutano wa zito.
 
huyo ruta baada ya kuambiwa na wewe sasa upo ktk mgao akapoa,je nini kilimfanya hasijuizuru wadhifa wake baada ya maamuzi yake kukataliwa,asitudanganye na watu wanaujua ukweli kama anabisha hafungue hiyo kesi tuone mbivu na mbichi
 
Oh, Yes, kwa hapa hili la IPTL Ruta huenda anapoint!
Ila kwenda kwake mahakamani kutasaidia sana kwani ataweka wazi hao waliomshinikiza ambao ndo tunawataka!. Lakini pia itabidi aeleze kwanini alicompromise? je alipozwa? ama alifunzwa ndo akaja shiriki vyema la TANGOLD?
 
Sam,
Being objective, hiyo article mara ya mwisho jinsi nilivyokuwa nikiisoma, ilionekana kama huyo Brian COOKSEY ni mouthpiece ya Ruta. Sijui kama unanipata? Mwandishi wa habari hiyo alipata vipi data zote hizo....its like he was there wherever Ruta was.
Am just being objective to the situation, maana naona tayari watu wanachagua sides kwasababu tu ya hiyo article. Lets look at the bigger picture.
 
...yah Ruta alikuwa on the "good side" ktk suala la IPTL. hiyo TANGOLD nina wasiwasi nayo kwasababu imejaa makatibu wakuu[ulinzi,fedha,madini] wengi kama wakurugenzi.

isije ikawa Mzee Slaa imechungulia sehemu asizotakiwa kuchungulia. nadhani mnanielewa.
 

...unajua sasa naanza kupata idea kuna ufisadi wa hali juu na Mkapa anahusika katika hii ofisi ya Mauritius,i remember Steve Mkapa alikuwa anasema anaenda kikazi Mauritius wana ofisi yao...mafisadi kweli kweli hawa.
 
Tangu tutangaze orodha ya mafisadi pale viwanja vya MwembeYanga, mjadala mkali sana umetokea katika taifa. Mara baada ya kutangaza orodha hiyo siku ya jumamosi tarehe 15 Septemba, waliotajwa wengi walikaa kimya bila kujibu chochote wakiamini kuwa vyombo vya habari havitataja majina yao. Ni kweli takribani vyombo vyote vya habari havikutaja majina yao.

Wiki iliyopita ikabadili kabisa mjadala huu ambao ulikua umeanza kulala. Gazeti la MwanaHalisi lilitaja Mafisadi wote kwa majina na kwa vipi wamehusika. Hapo ndipo waliotajwa walipoanza kujibu mmoja baada ya mmoja.

Najua kuwa Mkuu wa Kaya aliagiza kupitia Waziri Marmo kuwa kila mtu ajibu tuhuma zake. Waziri Mkuu alikuwa ni mmoja wa watu waliogomea agizo hilo la mkuu wa kaya ya kwamba kila mtu ajibu tuhuma zake mwenyewe. Aakamtuma Mzee Kingunge ajibu. Haikutosha na pia mwungwana akahimiza kupitia kwa Waziri anaepata nguvu za ajabu hivi sasa ndugu Marmo. Karamagi akaanza!

Majibu ya Karamagi na yale ya Mgonja, ambae alifuatia yanafanana sana. Mtindo wao wa kujibu ulikua ule ule.

Hata hivyo, majibu ya Patrick Rutabanzibwa, mmoja wa wasomi wazuri sana katika Taifa hili yamenifanya nitake tujadili, tumjadili kwa kina yeye na ufisadi wake na ikibidi humu humu totoe 'verdict'. Wale walio karibu nae wamwombe aje humu katika mjadala huu. Kwa nini yeye?
Angalau yeye amejibu baadhi ya tuhuma zake katika mkutano wake na waandishi wa habari. Wakati Karamagi na Mgonja wametishia tu kwenda mahakamani, Rutabanzibwa yeye kasema ni masuala gani hahusiki nayo na yepi anahusika nayo. Kasema kwa kina ni vipi hahusiki na IPTL lakini kakubali kuwa katika bodi ya TANGOLD na pia kuwa na hisa za kampuni hii. Wengine wote isipokuwa Chenge wamechenga kusema chochote. (Chenge kakubali kuwa na hisa katika TANGOLD).

Nilikutana na Ruta kwa mara ya kwanza mwaka 2003 nikiwa pale Chuo Kikuu cha Dar. Nilikua kiongozi wa DARUSO na tuliandaa mjadala kuhusu Netgroup Solution, kwanini nchi iingie katik mkataba huu (NETGROUP ulikuwa ni mkataba mbovu pia). Tulifanya mjadala pale Council Chamber, alijenga hoja na kutuacha wote hoi licha ya kujindaa kweli kweli.

Tunaambiwa Ruta ni mmoja wa Bureaucrats wenye uzalendo wa hali ya juu na alie tayari kulinda maslahi ya nchi kwa gharama yeyote. Tunaweza kukubali kuwa Ruta alipinga IPTL, lakini IPTL bado ipo na nchi inafujwa.

Kakubali kuwa na hisa katika TANGOLD, kwa niaba ya serikali. Uchunguzi unaonesha kuwa TANGOLD ni monster. Kampuni hii imehusika moja kwa moja na wizi wa fedha za umma katika Benki Kuu. Mzalendo Ruta anakaa katika bodi ya kampuni hii. Anasemaje juu ya hili.

Rafiki yangu mmoja aliniambia, jamani mmekosea kumtaja Ruta. Ni mwadilifu! Dkt. Slaa, hana tatizo lolote binafsi na watu waliotajwa. Ametimiza wajibu wake na alitoa mwezi mzima kwa serikali kuact, wakadharau. Orodha iliyotolewa ni orodha iliyofanyiwa kazi vya kutosha na wala haikuwa na lengo la kumwonea mtu. Rutabanzibwa, ambae anaonekana kutetewa na watu wnegi sana hapa nchini, ni vema aseme ni vipi ahusishwe na uporaji wa nchini.

Ikumbukwe kuwa katika orodha hii kuna mafisadi wa moja kwa moja na wale waliotumia mamlaka yao ya umma.

A. USHIRIKI WA MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

Katika kundi hili wamo viongozi na/au maafisa wa umma na/au mawakala na/au washirika wao katika sekta binafsi ambao kwa namna mbali mbali wameshiriki katika kupora utajiri na/au fedha za umma na hivyo kulisababishia taifa na umma wa Watanzania ufukara na/au umaskini mkubwa.

B. USHIRIKI KATIKA KUTOA MAAMUZI YA KIFISADI

Katika kundi hili wamo viongozi wa umma ambao kwa kutumia nyadhifa na/au vyeo vyao katika utumishi wa umma wamefanya maamuzi ambayo kwayo taifa limepoteza mapato na/au utajiri na rasilmali zake na kuwaneemesha raia na/au taasisi za kiuchumi na/au za kibiashara za kigeni. Kwa mfano, viongozi wa umma walioshiriki katika kusaini mikataba mibovu katika sekta za madini na/au nishati na/au maeneo mengine yenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya taifa na jamii ya Watanzania.


Patrick Rutabanzibwa atajwa kama ntu aliyetumia madaraka yake vibaya kuingia mikataba mibovu na kushindwa kuizuia. Ruta aweza kuwa safi, lakini analo la kujibu kwa Watanzania.

Tumjadili Patrick Rutabanzibwa, Katibu Mkuu wa zamani (1997-2006) wizara ya nishati na madini na Katibu Mkuu wa sasa wa Wizara ya Maji.
 
Zitto,
hivi na Raisi naye atajibu tuhuma dhidi yake? Raisi atatupa maelezo ya ushiriki wake ktk kuandaa sera na sheria ya madini inayotutia hasara?
 
Zitto,
Hongera sana mkuu.Hakuna kulegeza kamba.Kila mkono wa damu lazima ufichuliwe na kushitakiwa mbele ya umma wote wa wananchi.
Najua kazi hii ni ngumu ila kwa kuwa tumesimamia haki na wao wamesimamia dhuluma tutashinda tu.
Wembe.
 
Baadhi ya maelezo huyu jamaa ni haya hapa"Rutabanzibwa alisema kigezo kuwa alitumia wadhifa wake vibaya kwa kulitia hasara Taifa wakati akiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini si sahihi na wala hakuna ukweli.

Alifafanua yeye hakuhusika katika kutia saini mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura wa IPTL na Serikali na kwamba mkataba huo ulipitishwa na Baraza la Mawaziri na ulifuata sheria ya madini ya Taifa.

"Sikuwa Katibu Mkuu wakati mkataba wa IPTL ukisainiwa Mei 26, mwaka 1995 na niliteuliwa kuwa Katibu wa Wizara ya Nishati na Madini Mei 11, mwaka 1997", alisema Rutabanzibwa."


Ok,kasema alipokua katibu mkuu wizara ya madini,tuhuma dhidi yake kuwa aliingizia taifa hasara kwa maamuzi yake,si za kweli.
Swali je mbona hakutueleza ukweli upo wapi?Yeye kama katibu mkuu wa wizara ya madini,alichangia vipi kuishinikiza serikali kutoingia mikataba holela ya madini?Mie naona bado hajajibu hoja kamili,tupeni nondo zake.
 
Nadhani hii iuanganishwe na ile nyingine.. labda kichwa cha habari kinaweza kuwa modified..
 
kama ruta yy aliipinga iptl mbona hakusema hadharani anakuja kusema ss hv maji yashamwagika?na pili mbona ana hisa katika kampuni ambayo inahusika kwa %110 kuchukuwa fedha za umma...jamani kweli huyu ana uchungu na nchi au ndio zile zile ana uchungu machoni lakini moyoni.......naye agaiwe %10 hata kama fedha za umma zitaliwa na wananchi kukosa huduma muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…