List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

We KT

Ulilala na mimi huko mikoani mpaka wajua nimerejea?

Watoto tu walinipa shida, wakati mwingine nitakuaga.

Asha

Mmmmh mbona Hivyo!Humu ndani Burudani tosha,naona akina Mama wameshika Hatamu!!!Hawataki mchezo kabisa......
 
asha karibu tena,pole kwa ziara ndefu ya mikoani

KATIBU TARAFA...........

no da aASHA ABDALLAH alikuwa bizi na mapishi ya FTARI ya mzee si unajua swaum hii,lkn hivi sasa mzee amesafiri kwa shughuli ya kikazi huko mikoani ndio amepata nafasi kuja tena hapa JF.

da ASHA karibu tena JF makini,ile LOGO yetu KUMKOMALIA NYANI GILADI daima mbele tu,lakini siku hizi NYANI ANAKOMALIWA MCHANA KWEUPE.
 
haya bibie,kwani urais umekuwa maigizo?EL anafaa kuwa mwigizaji..AKIPEWA KUGOmbea urais kwa tiketi ya sisiemu utakuwa mwanzo wa kuanguka na kukigawa chama chetu,
 
Jamani

Mi ndio maana nampenda Lowassa. Hatimaye amejitokeza amemjibu mmbea Dr Slaa. Amemjibu kupitia mwandishi wake Nguba. Amesema yeye Lowasa hatajibu. Anawaacha wengine ndio wajibu. Kutokujibu nalo si jibu jamani? Wengine wanasema kutokujibu ni ishara ya kukubali, ni nasema lowasa amefanya vizuri kuacha kujibu uzandiki. Ukianza kujibishana na mwehu nawe utaonekana mwehu bure. Hongera Lowasa, urais 2015 uko karibu yako.

Asha

Kwa hiyo, kwa akili yako, hii ndiyo sifa ya rais anayehitajika 2015? Kumbe ndiyo maana mnachagua sura! Baadhi ya wapiga kura wana akili za kitoto!
 
Jamani

Mi ndio maana nampenda Lowassa. Hatimaye amejitokeza amemjibu mmbea Dr Slaa. Amemjibu kupitia mwandishi wake Nguba. Amesema yeye Lowasa hatajibu. Anawaacha wengine ndio wajibu. Kutokujibu nalo si jibu jamani? Wengine wanasema kutokujibu ni ishara ya kukubali, ni nasema lowasa amefanya vizuri kuacha kujibu uzandiki. Ukianza kujibishana na mwehu nawe utaonekana mwehu bure. Hongera Lowasa, urais 2015 uko karibu yako.

Asha

Kwa hiyo EL kakubali kuwa ni fisadi.hahahaha,sasa tena urais wa nini?Au rais wa chama cha wasanii?hahahah,angalia akina Kingwendu watawatoa nyongo.
 
dada Asha vipi kuhusu yule mtoto wa form 1 kule Ukerewe mwanza?hapo unasemaje?je na Dr. Slaa pia mtamtumia vijana wa "Usalama wa Taifa"kumuuliza ni nani kamtuma?
 
Hya sio majibu ya waziri mkuu, ni mzaha kwa watanzania ama hajui kwamba watu wapo serious?

Waziri mkuu wa Japan alijiuzulu pindi alipotuhumiwa na rushwa , wa kwetu anasema kuwa yeye hawezi kujibu anawaacha wengine wajibu, ,

Ningekuwa Nguba nisingeweza kuwaeleza watanzania ujinga huu.
 
Swali moja la mtoto wa ukerewe limemshinda na bado analitafutia jibu, ataweza kujibu nondoz za Mhe. Slaa?
 
Swali moja la mtoto wa ukerewe limemshinda na bado analitafutia jibu, ataweza kujibu nondoz za Mhe. Slaa?

Si ndo hapo???

Lakini hii ni simple kwani zero times zero = Zero. Hata sikumoja haiwezi kuwa 1.

Tutasikia na kuona mengi ngwe hii!!! 'Ya akina malaika watu wasiokosea siku zote'
 
Si ndo hapo???

Lakini hii ni simple kwani zero times zero = Zero. Hata sikumoja haiwezi kuwa 1.
Tutasikia na kuona mengi ngwe hii!!! 'Ya akina malaika watu wasiokosea siku zote'

Kaka Rwabugiri kula tano zote kwa superb observation hiyo,hakika nimekukubali,natamani huyo Said Nguba angewekewa ubongo wako...ni kweli 0x0=0 kabisaaaaa....mtoto wa Ukerewe tu kamtoa jasho vipi kwa Dr.Slaa? by the way eti nasikia na yeye pia atakuwa kwenye hiyo ziara ya kuzunguka nchi nzima "kujibu wapinzani"? vipi akiombwa aufafanue mkataba wa Buzwagi?kwi kwi kwi kwi (ni joke tu Dada Asha)...
 
Corruption is for real, says Judge Bomani

-Warns of possible fall-out from court cases

PENDO PAUL NDOVIE
Dar es Salaam

PROMINENT former judge and attorney general Mark Bomani declared yesterday that corruption in the country was real and widespread.

He told a news conference in Dar es Salaam that attempts to portray the country as a corruption-free haven were woefully misguided.

Bomani, who is still a practising advocate of the High Court, furthermore discouraged top government and public officials named by opposition legislator Dr Wilbrod Slaa in the now-famous 'List of Shame' from seeking legal redress.

''I urge those who are threatening to go to court over the allegations of corruption against them, to think twice before taking such a step because it may develop into something totally unexpected,'' he said.

He added: ''Based on my experience in these matters as a judge and currently as an advocate, I would advise these people to do a rethink and consider if there is any real need to take this issue to the courts.''

At least three of those named in the list of prominent leaders alleged to have been involved in several dubious multi-billion shilling deals while in office in recent years, have separately announced over the past week their intention to sue Dr Slaa and a private Kiswahili tabloid for making the list public.

They are the Minister for Energy and Minerals, Nazir Karamagi; the Permanent Secretary in the Ministry of Finance, Gray Mgonja; and the Permanent Secretary in the Ministry of Water, Patrick Rutabanzibwa.

By contrast, yesterday's news conference was convened by Bomani to clarify on remarks attributed to him in an article published by the Kiswahili weekly Rai, where he ostensibly spoke in defence of the public leaders named in the 'List of Shame'.

Bomani said the newspaper not only misquoted him, but also published an article that was completely out of the context of the actual interview.

The former attorney general, who also once chaired a government task force on the Legal Sector Reform Programme, asserted that corruption was indeed present in Tanzanian society in both the public and private sectors.

Claims that corruption does not exist in Tanzania are a falsehood, he stated.

He pointed out that President Kikwete himself declared publicly last year that he had a list of public leaders involved in corruption, and gave them an ultimatum to reform or risk being reprimanded.

Speaking generally about the state of corruption in the country, Bomani said the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) should effectively enforce the newly-passed anti-graft legislation to tackle high-level corruption.

He specifically cited provisions of the Prevention and Combating of Corruption Act of 2007 that compel public officials to truthfully declare all their assets.

Bomani challenged the PCCB to exercise its powers and prosecute public officials who under-declare their assets under this Act.

He noted that the Bureau has so far done little to apply the new legislation for the prosecution of corrupt people looting government funds in the public sector.

''It is high time that the PCCB starts to fully discharge its mandate and wipe out corruption. It should start taking real legal action against all public officials who are in contravention of the new anti-graft law,'' Bomani said.
 
Mtei, then Bomani.

Gazeti la RAI vipi? Quoting out of context!
 
Mwanakijiji pokea tano wakwetu.

Yaani kichwa kinanizunguka na hasira kibao! hii yawezezekana tanzania tu.
 
Hebu tuangalie hii taarifa. Mwandishi wa Rais hamsaidii Rais kwa kuanza story yake na kauli ya Rais kushambulia wanaotoa tuhuma, wakati katika mkutano huo, Rais alionekana moja kwa moja kuzipokea tuhuma dhidi ya viongozi wake na kuahidi kuzifanyia kazi bila kumuonea wala kumuogopa mtu na ndio akaomba uvumilivu katika kufuatilia tuhuma hizo kwa kutumia mkondo halali wa sheria. Inawezekana Maura ameguswa na hilo la kushambuliwa watoa tuhuma akitaka kumtetea bosi wake wa Zamani, Benjamin Mkapa.
 
Hii ni ngumu, ''tumedhamiria kupambana na rushwa na kwa kuanza tumeanza ndani ya SISIEM''.

Ina maana toka alipoingia madarakani alikuwa hajaanza, huyu jamaa ameanza tena ka utaratibu kariko mpatia kura nyingi yaani kuji attach na viongozi wa dini. Tafadhali viongozi wa dini nawaonya MSISIFIE TU KWA VILE MNATAKA MALENGO YENU YA KUKUSANYA HELA YATIMIE, simameni kukemea madhambi yanayofanywa na watawala. Haiwezekani hali ya maisha inaendelea kuwa ngumu hakuna matumaini mnasifiasifia tu, HAPANA, kemeeni rushwa.

Rais na viongozi wote watambue kuwa, tunapotaka barabara, ulinzi wetu na mali zetu na mengine sio hisani ni haki yetu na wanapaswa kutupatia pasipo majisifu kwani tunawalipa mishahara mikubwa tena waliojipangia wenyewe.

Maaskofu waache unafiki, tuungane kuwaambia viongozi pale wanapokosea

Hatuna imani na vyombo vya sheria, hatuwezi kuviachia vikatenda haki hata siku moja. Suala la Buzwagi na BOT lingeachwa Bungeni bila kupelekwa kwa wananchi na wananchi ku react unategemea nini? Vyombo vya dola vinamwajibisha mpigania haki leo unawaambia watu waviachie vyombo vya dola, wapi na wapi, ni sawa na kesi ya nyani kula mahindi kuipeleka kwa ngedere au kesi ya SISIEM kuipeleka kwa mkuu wa kaya ambaye ni kinara wa SISIEM

Narudia tena, hii nchi sio mali ya watu wachache waliopo madarakani, Viongozi wa dini acheni tabia ya kujikomba kwa lengo la kufanikisha maslahi yenu, piganieni haki za waumini wenu na wananchi kwa ujumla. MAISHA BORA TUNAYAHITAJI HATA KAMA SISIEM WASINGEHUBIRI HILI.
 
tatizo ni kuwa wanafikiri madai yote yaliyotolewa yanahusu Rushwa!! sasa wakienda kuchunguza na kukuta hakuna rushwa watatuambia hakuna rushwa.. tatizo ni kuwa hakuna mtu aliyedai kulikuwa na rushwa!!!.. kuna suala la mgongano wa kimaslahi, matumizi mabaya ya ofisi, matumizi mabaya ya cheo n.k Its not all about rushwa.. ndio maana walipoenda kuchunguza RCD walikuja na taarifa kuwa hakuna rushwa. Kwenye suala la Buzwagi hakuna mtu aliyedai fulani kala rushwa!! Ufisadi is more than rushwa/hongo. Corruption is more than just bribery and kickbacks!!
 
Kama ameona hili ni vizuri, wananchi wamechoka kudanganywa kila asubuhi mchana jioni kuona wahalifu na mafisadi wakienda bila kupata adhabu, Na nani zaidi wa kuwajulisha uovu kama sio viongozi wanaoyapinga haya mambo. Hakuna aliyekamatwa na sidhani kama kuna upelelezi wowote unaohitaji kufanyika mambo haya yapo kila siku ya maisha yetu.

Hukumu anayoizungumzia hapa ni ipi, sijaona hata 1 akilipa mabilioni aliyojichotea au hata mmoja akienda gerezani? hukumu ya wananchi pale tu watakapoamua kuchagua viongozi wengine na sioni kama hicho ni kitu kibaya kwa watu wa taifa hili.

Hakuna pabaya zaidi kama kila siku unasikia habari za wahujumu nchi wakiendelea kujinufaisha bila kujali binadamu wanaowaongoza na hatua yeyote haichukuliwi juu yao wakati wengi wetu tunashindwa pa kuanza ili kupata mahitaji ya maisha ya kila siku. Mahitaji ambayo hayashikiki kwa sababu wasimamizi wa nchi hii wameshindwa kuhakikisha wananchi wa taifa hili kwanza na wengine ndio wanafuata.

Sheria zipi hizo? za mwaka 47 na vyombo vya sheria tunavyovijua ama kuna vingine? vyombo ambavyo mwenye pesa akijitutumua kidogo anaonekana mtakatifu wa watakatifu.

Hata viongozi wa dini wanajikausha kiasi hiki, we are in big trouble. nani asiyeona mambo haya ya rushwa?????? there are so many ways one can say something without stepping on other people's toes. Na hawa wachunga kondoo wasianze kupotosha watu. angeweza kumpongeza kwa mambo mengine like having a good smile, kucheka cheka wakati anatoa hotuba zake ambayo he is very good at.


Hapa inaonyesha jinsi waCCM walivyo if they can play these dirty games among themselves, nani atabakizwa. Kabla haujasema chochote ask yourself unajenga ama unaharibu kabisa. Na sisi tutajuaje kama sio mnataka kuwaondoa wale ambao hawapo katika mtandao wenu mkaona njia haswa ni kuwasukia story? halafu mtu anasema watachukuliwa hatua, hatua my foot.


Mbona hatujaona misingi na kanuni zozote zikifanyika, hao mawaziri kuzunguka nchi nzima kuendelea kudanganya wananchi ili wawape nafasi nyingine ya kufanya ufisadi ni ndio kanuni na misingi? Na pesa wanazotumia sizingetumika pale zinapohitaji ka zaidi kama kweli lenu ni kujenga taifa hili.

Hapa watu waanze kuchapa mwendo watz wamechoshwa na uongo na ubabaishaji. na viongozi wa dini mna mchango mkubwa sana katika kuiweka nchi panapostahili hakuna haja ya kuona maovu yanaendelea na nyinyi mkapiga makofi na kupongeza huku wengi wetu tukiumia bila siku ya mapumziko katika shida zetu.

Ndg JK hapa bado haujaanza kupambana na rushwa, maneno mengi bila utekelezaji and as they say talk is cheap, we need to see some action.
 
Back
Top Bottom