List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Utabiri wangu mimi Lunyungu karibia utatimia. Niliyasema haya baada ya kuona trend ya matukio na action za Mkuu wa Nchi. Kukaa kimya hadi kusema USA, then kuuliza maendeleo ya ziara za Mawaziri mikoani na hata Kaka Ditto kuwa msemaji wa serikali . Hapo nikajua hakuna lolote na there will be a huge twist.Now Rais mwenyewe kaanza kuziba mashimo na akili yao yote inawafanya waone kwamba ni Rushwa pekee ya BOT lakini kasema Mzee wa Kijijini kwamba Ufisadi una maana pana na matukio yake ni mapana pia .Hapa dawa ni Slaa na sisi Watanzania kusimama kideta maana hakuna wa kwenda Mahakamani wala Rais hana mpango wa kusikiliza kilio chetu sababu inakuwa ni kulindana na kukifanya Chama chao kizidi kuonekana kisafi. Rais anaanza na kauli za kutisha , anataka watu wakae kimya na PCCB waachiwe wakati anajua kwamba walio tuhumiwa wako juu ya Sheria katika hii Nchi .

Kuna haja ya Wapinzani sasa kwenda Mahakamani na kuwapelekea wote walio tajwa akiwa Rais wakati akiwa waziri aje kusema anayo yajua kuhusiana na mikataba . Waziri Mkuu wa Israel kesha hojiwa na polisi kuhusiana na ubinafsishaji wa Bank moja tu itakuwaje sisi madini yote Rais anatukemea kwa nia ya kutisha watu ?
 
tatizo ni kuwa wanafikiri madai yote yaliyotolewa yanahusu Rushwa!! sasa wakienda kuchunguza na kukuta hakuna rushwa watatuambia hakuna rushwa.. tatizo ni kuwa hakuna mtu aliyedai kulikuwa na rushwa!!!.. kuna suala la mgongano wa kimaslahi, matumizi mabaya ya ofisi, matumizi mabaya ya cheo n.k Its not all about rushwa.. ndio maana walipoenda kuchunguza RCD walikuja na taarifa kuwa hakuna rushwa. Kwenye suala la Buzwagi hakuna mtu aliyedai fulani kala rushwa!! Ufisadi is more than rushwa/hongo. Corruption is more than just bribery and kickbacks!!

Mwanakijiji.
Hapo umenikuna kichwa,wao wanadhani ni rushwa tu,hawajui kuna vitu vingi vinafanyika na kulisababishia taifa hasara kubwa bila ya hata rushwa kutumika.Hapo ndipo huwa nasema nina wasiwasi mkubwa na uelewa wa viongozi wetu,yaani wanaonekana mbumbumbu sana,sioni mtu wa kuweza kujenga na kusimamia hoja,wote bora liende tu.
 
Huyu JK asifikirie bado tupo kwenye enzi za kutishia watoto kwa nyau (paka). Kwa vitisho vyake ndo anaharibu mambo kabisa. Ni bora angeonyesha action kimya kimya pengine angalau hasira za watu zingepua. Kama ningekuwa kikwete, hatua muhimu ambazo ningechukua ni 1. Kumweka pembeni karamagi 2. Kumfikisha mahakamani, 3. Kusitisha mkataba wa Buzwagi - kabwe mara moja na 4. Kuvunja baraza la mawazili na kuliunda upya.
 
Whatsoever the case, the message from president is simple,,, kila kilichosema ni TUHUMA tu, until prove in the court of law, kitaendelea kuwa TUHUMA;

And you have to remember he did not said ni uongo au ni ukweli! until uchunguzi,,, sijui mlitaka rais awe Jaji Ramadhani, i do not know reall!

Zaidi ya hapo ni Kuvunja Katiba kwa kutompa huyo MTUHUMIWA haki yake ya msingi ya kujitetea mbele ya SHERIA, msioelewa hilo kwa kweli mnataka tujenge taifa lisilofuata sheria!

No wonder mtu anajenga Jangwani, bila kibali, na kuelezwa kwamba ni eneo hatari kwa maisha yake, na kupewa kiwanja ajenge sehemu nyingine, at end of the day akivunjiwa nyumba anasema serikali imemuonea...

Ndio taifa tunalojenga,,, tulalamike likiwa chini ya CCM, lakini hali itakuwa mbaya kama wananchi watakuchukua sheria mkononi hata taifa hili likiwa chini ya Kipenzi Zitto au Mbowe!!!

Ni vyema kama watu hao wanajiaandaa kushika nchi wawafundishe/kuwahimiza wananchi kufuata sheria maana ndiyo itafanya wafanye wanayokusudia kulifanyia taifa.

Naungana na Mzee Mwanakijiji kwamba Mh. kama vile amejikita kwenye RUSHWA, lakini hata kama sio kwenye RUSHWA hata wizi huo mwingine, utumiaji wa madaraka vibaya, also need to be proved,,, tangu lini Dr. Slaa akawa na vyeo vyote hivyo vya kuprove vitu!

Mwenzako Akinyolewa Wewe Tia Maji!

I'm expecting the same reaction hata kama Rais angekuwa Prof. Lipumba, Leonard Shayo, Mh. Mbowe, Mh. Zitto, Mh. Mudhihiri..

But I should of course expect different reaction kama Rais angekuwa... Kaka... Agustion Lyatonga Mrema
 
Kama ningekuwa kikwete, hatua muhimu ambazo ningechukua ni 1. Kumweka pembeni karamagi 2. Kumfikisha mahakamani, 3. Kusitisha mkataba wa Buzwagi - kabwe mara moja na 4. Kuvunja baraza la mawazili na kuliunda upya.

RPG,

Ndio maana hautawahi kuwa Rais, kwani tahamaki za namna hiyo zinaishia wewe kufanya makosa na kukosa imani hata kutoka kwa watendaji wako na hilo ni tatizo kubwa linalosabibisha hata wewe binafsi kupigwa chini!

Mawazo kama ya kwako ndio yaliyosababisha Katiba iseme Rais awe na Umri gani!
 
Killtime;
Watoa hoja hawakuhukumu, Huyu Padri au Askofu - ni Mfarisayo na anamsifia mfalme mla rushwa. Watanzania msihadahike, mnawalaumu mawaziri kiasi kwamba sielewi kama mnajuaje serikali inaendshwaji. Organisation chart, ni ile ile, what a minister endorses the president knows; and what the minister will part with the president will know, it is a relations between a parasite and an organ (symbytic); Mkapa aliiba millions bila mawaziri kujua? au you're telling me if Lowasa is a billionaire as others are saying in this forum JK is poor? or RA and the like are corrupting the system, you're telling me the president doesn't benefit in one way or another? The issue here, i will not attack Karamagi or any minister, the president himself is hiding behind the ministers and Mafarisayo like baba askofu to threaten the people! The president should be a culplit number 1! Especially if he doesn't act!
 
Kilitime, ni nani mwenye jukumu la kuchunguza tuhuma na kuzithibitisha? Mimi ninapohisi fulani kaniibia kuku wangu, na kesho yake nikamuona kuku huyo kwenye kibanda chake akisubiri kuwa kitoweo, ninapoenda Polisi kutoa taarifa nawaambia Polisi "fulani kaniibia kuku wangu, na kuku mwenyewe ni yule". Ni jukumu la POlisi sasa kuangalia madai yangu na ushahidi ninaoutoa na kwa vile wao wanazo nyenzo basi wanaweza kuenda kumhoji yule bwana alimnunua wapi kuku yule n.k Sasa kwa kitendo cha watu wengine kudai ati nimekuwa mtoa tuhuma, jaji (kwa kuonesha kuku ninayedai wangu) na kwenda polisi ili jamaa akamatwe (mkamataji) ni kunichezea akili! Vinginevyo, kuanzia sasa wananchi wasitoe tena tuhuma, wasioneshe kila wanachoamini ni ushahidi na wasiwe tayari kuwaelekeza polisi walipo watuhumiwa!!

Walichofanya wapinzani ni kile kile na si zaidi ya hicho.

- Wametoa tuhuma: Dhidi ya watu kumi na moja kwa kuelezea kinagaubaga msingi wa tuhuma hizo.

- Wamewaeleza Polisi ni kina nani hao: Wametangaza hadharani fulani na fulani "wamechukua kuku wa kijiji" na ushahidi ni huu

- Wamewaelekeza waliko watuhumiwa hao: Wametaja ofisi zao na vyeo vyao

Sasa leo wanatakiwa wafanye kazi ya polisi pia kwa "kuleta ushahidi zaidi"! Huo ni upuuzi! Ni jukumu la Polisi na vyombo vya usalama kuwaendea na kusema "tumesikia mmedai kuwa mmeibiwa ng'ombe wenu na mna vielelezo, hetu tuvione ili tuweze kuchunguza".

Cha kuchekesha serikali ya CCM haitaki kufanya hivyo na badala yake inakuja na "zipuuzeni hizo ni hoja za wapinzani". Sasa ningekuwa mimi ndiye mwenye neno la Mwisho kwenye hiyo serikali ningeamuru kina Manundu wakae na kina Dr. Slaa mbele ya mawakili, wapewe nakala za taarifa zote, na mara moja wafanye uchunguzi wa kipepelezi kwa kuanzia na taarifa hizo, na ningeamuru wale wote waliotajwa kuwapa ushirikiano wote na mimi mwenyewe ningekuwa tayari kukaa na kuulizwa maswali na wapepelezi hao mbele ya mawakili wa kina Dr. Slaa. Ningehakikisha kuwa kama kuna mahali ambapo binafsi nimeboronga ninakiri sikuwa makini na kuamua kujitoa kwenye makampuni ambayo yanaonesha mgongano wa kimaslahi.

Zaidi ya yote ningeamuru Baraza langu zima la Mawaziri kutangaza hadharani makampuni yote waliyo na hisa nazo na kuona kama kuna kampuni ambayo inaendana na wizara zao na kuwataka wauze hisa hizo mara moja au kuziweka kwenye trust fund au waamue kujiuzulu ili kusiwe na mgongano wa kimaslahi.

Jambo moja nisingefanya, kuwataka wananchi wapuuzie!!
 
KILITIME,
Kwa mtazamo wangu ni kwamba inaonekana mzee hukuzaliwa bongo na umekuja hapa ukiwa mtu mzima,sasa turudi kwenye mada hasa hiyo sheria,ccm na serikali yake siku zote wanaangalia sheria ambazo wanamasilahi nazo na si vinginevyo.

Eneo la jangwani ni hatari kwa maisha je serikali ilikuwa wapi wakati watu wanaanza kujenga mpaka kufikia kijiji.unapokaribia uchaguzi wamachinga wote wanarudi mjini lakini baada ya uchaguzi unaambiwa wanachafua jiji sijui utawala wa sheria ni upi.hizi tuhuma zipo wazi kwa nini serikali inakuwa na kugugumizi ktk kuunda tume huru ilikuchunguza hizi tuhuma.

Kama kunautaratibu wa kufanya basi serikali ni kazi yao kuuweka wazi ili wananchi wajue na sio kuendeleza vitisho kitu ambacho hakitasaidia zaidi ya kuongeza hasira zao.swala la mahakamani lisu alitolea mfano kesi ya byunkulu ambayo mpaka leo haijapiga hatua yoyote hata kusikilizwa bado toka 1995,je tutafika kweli.

Chukua mfano mwingine wa mbunge wa buchosa mtanisahihisha kama nimekosea jina ambaye uchunguzi wa polisi umethibitisha kugushi vyeti lakini sheria hapa ipo kimya,ndio maana hata jk amepokea cheque yenye makosa lakini anachekelea tu.kuna mambo mengi ambayo yanakiuka sheria lakini kwa sababu ni sera za ccm hapo hakuna sheria.Mwenzetu kama ni kada wa ccm tuambie ilitusipoteze muda.ccm kwanza sheria nyuma.
 
Kwa kweli sina hata cha kusema, WE ULITEGEMEA ASKOFU ASIMSIFU RAIS WAKATE ANATEGEMEA KITITA CHA MCHANGO, nia yake ilikuwa hizi million zilizopatikana. Askofu naye ajijue kuwa na yeye sio Mungu, kama anatetea uzembe itamgharimu
 
kilitime,
Dr.Slaa amemtuhumu JK kwamba alipokuwa Waziri wa Madini alisaini mikataba ambayo inapora rasilimali yetu ya dhahabu. Dr.Slaa ameitaja mikataba hiyo kwa majina na lini ilisainiwa.

Wakati wa kampeni JK alikuwa anatuhumiwa kwamba yeye ndiye alisaini mkataba wa IPTL. JK alieleza kwamba mkataba wa IPTLuliposainiwa yeye alikuwa tayari amehamishwa kwenda wizara ya Fedha. Minungono ya JK na IPTL nayo ilikwisha mara moja.

JK anapaswa kueleza/kufafanua kilichomo ktk mikataba aliyosaini. Vilevile anapaswa kutueleza kwanini anafikiri mikataba hiyo ni ya manufaa kwa taifa. Zaidi aeleze mazingira yaliyopelekea mikataba hiyo kusainiwa.

Hata kama mikataba hiyo inatuingiza hasara[yaani ni ufisadi] siyo lazima waliosaini mikataba hiyo walikuwa mafisadi.
Inawezekana kabisa JK hakutegemea kwamba tungeingia hasara kama hii tunayoingia.

Inawezekana kabisa kwamba mikataba hiyo ilisainiwa kwa nia njema kabisa pamoja na kwamba ni mibaya. Kwani ni mara ngapi sisi wananchi wa kawaida tukaanzisha biashara na kupata hasara!!

Kinachonifadhaisha mimi ni CCM na serikali yake kutokubadili muelekeo ktk sera yetu ya uwekezaji ktk madini na nishati. Tayari wanajua walikosea lakini hawataki kuchukua hatua madhubuti kurekebisha hali hiyo.

NB:
Hizi siasa za kuchafuana kwenye vyombo vya habari zilianzishwa na wanamtandao. Kwa muda wa miaka 10 walikuwa wakimsakama FTS kwamba ni fisadi na mlarushwa.

Kampeni hizo ndizo zilizomnyima "tonge" FTS na kumpa JK. Wapinzani wamejifunza toka kwa CCM mtandao na kujenga imani kwamba kampeni chafu ndiyo njia ya uhakika ya kuingia Ikulu.

Hivi wana CCM mtandao walipokuwa wakimsakama FTS, waziri mkuu wa serikali ya CCM, hawakuwa wakiogopa uwezekano wa nchi kutokutawalika?

Wazungu wana msemo wao "when the toothpaste is out of the tube it is very hard to get it back in."
 
Hivi bila whistle blowers utajuate kama mahali pana rushwa. Sasa nashangaa JK anawapiga mkwara halafu anasema atafuatilia. Hivi vyombo vinavyohusika vitapataje taarifa? Mambo ya Bongo kila kitu kinafanya kinyumenyume tu!!!!
 
Kilitime, ni nani mwenye jukumu la kuchunguza tuhuma na kuzithibitisha? Mimi ninapohisi fulani kaniibia kuku wangu, na kesho yake nikamuona kuku huyo kwenye kibanda chake akisubiri kuwa kitoweo, ninapoenda Polisi kutoa taarifa nawaambia Polisi "fulani kaniibia kuku wangu, na kuku mwenyewe ni yule". Ni jukumu la POlisi sasa kuangalia madai yangu na ushahidi ninaoutoa na kwa vile wao wanazo nyenzo basi wanaweza kuenda kumhoji yule bwana alimnunua wapi kuku yule n.k Sasa kwa kitendo cha watu wengine kudai ati nimekuwa mtoa tuhuma, jaji (kwa kuonesha kuku ninayedai wangu) na kwenda polisi ili jamaa akamatwe (mkamataji) ni kunichezea akili! Vinginevyo, kuanzia sasa wananchi wasitoe tena tuhuma, wasioneshe kila wanachoamini ni ushahidi na wasiwe tayari kuwaelekeza polisi walipo watuhumiwa!!

Walichofanya wapinzani ni kile kile na si zaidi ya hicho.

- Wametoa tuhuma: Dhidi ya watu kumi na moja kwa kuelezea kinagaubaga msingi wa tuhuma hizo.

- Wamewaeleza Polisi ni kina nani hao: Wametangaza hadharani fulani na fulani "wamechukua kuku wa kijiji" na ushahidi ni huu

- Wamewaelekeza waliko watuhumiwa hao: Wametaja ofisi zao na vyeo vyao

Sasa leo wanatakiwa wafanye kazi ya polisi pia kwa "kuleta ushahidi zaidi"! Huo ni upuuzi! Ni jukumu la Polisi na vyombo vya usalama kuwaendea na kusema "tumesikia mmedai kuwa mmeibiwa ng'ombe wenu na mna vielelezo, hetu tuvione ili tuweze kuchunguza".

Cha kuchekesha serikali ya CCM haitaki kufanya hivyo na badala yake inakuja na "zipuuzeni hizo ni hoja za wapinzani". Sasa ningekuwa mimi ndiye mwenye neno la Mwisho kwenye hiyo serikali ningeamuru kina Manundu wakae na kina Dr. Slaa mbele ya mawakili, wapewe nakala za taarifa zote, na mara moja wafanye uchunguzi wa kipepelezi kwa kuanzia na taarifa hizo, na ningeamuru wale wote waliotajwa kuwapa ushirikiano wote na mimi mwenyewe ningekuwa tayari kukaa na kuulizwa maswali na wapepelezi hao mbele ya mawakili wa kina Dr. Slaa. Ningehakikisha kuwa kama kuna mahali ambapo binafsi nimeboronga ninakiri sikuwa makini na kuamua kujitoa kwenye makampuni ambayo yanaonesha mgongano wa kimaslahi.

Zaidi ya yote ningeamuru Baraza langu zima la Mawaziri kutangaza hadharani makampuni yote waliyo na hisa nazo na kuona kama kuna kampuni ambayo inaendana na wizara zao na kuwataka wauze hisa hizo mara moja au kuziweka kwenye trust fund au waamue kujiuzulu ili kusiwe na mgongano wa kimaslahi.

Jambo moja nisingefanya, kuwataka wananchi wapuuzie!!

Mzee MwanaKijiji,

Nadhani Umesahau kidogo, wakati ule naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani alivyokuwa akihudumu kesi za ndoa? Uliona sawa eeeeh! Ndiyo hayo unayotaka eeeh.... Akisema mtu ndiyo ushahidi,,, hukumu hapo hapo na hakuna ku-appeal, yet mtaka utawala wa sheria...

Dr. Slaa huyo huyo ndiye aliyeboronga hata tarehe ambazo aliyekuwa katibu Mkuu... Rutakanzibwa sorry I misspelled the name....

Nitaendelea Kuwa Upande wa waleo wanaomini kwa tuhuma ni tuhuma tu,,, kwa kuwa mifano ya tuhuma zao uwongo tunazo...

Mojawapo ilitoka kwa Mzee Mwanakijiji, kwamba Karamagi alimchunia Zitto baada ya Kuhoji MKJJ akaonekana alikuwa mwongo!!!

Sasa ni Mzee Mwanakijiji Huyu anayekataa mambo yachunguzwe bali tuamini anayasema...

NARUDIA, Siwezi hukumu kama Dr. Slaa ni Mwongo au Rais ni Mwongo, No... Uchunguzi na Muda Unavyoenda tutamjua mkweli...

BoT, sasa hivi kunafanyika proffesional auditing, chini ya kampuni la kimataifa,,, report itatoka na baada ya hapo hatua zitachukuliwa au kutochukuliwa... but we will be able to comments...

Sasa Auditing inafanyika watu hawataki, ati wanataka Mrema au Mwanakijiji ndiye akafanye Auditing,,, hii ni aibu kubwa watu hawaheshimu taaluma,,,

Ndiyo hawa hawa wanaoamini ukiwa na mabomu mengin ndio kuwa kiongozi mzuri, kutoa mabomu ni jambo lingine na kuongoza ni jambo lingine!
 
Kilitime,
Alicho nacho Dr. Slaa si tuhuma tu. Anao ushahidi. Kuna vithibitisho vya akaunti za benki na namba zake. Hata ile mikataba ambayo mnadhani ni siri imeshavuja. Sikiliza kesho mahojiano yake na VOA. Saa mbili usiku ( saa za Tanzania) Bado kuna mengi yatafumuka.
 
Kwa kweli sina hata cha kusema, WE ULITEGEMEA ASKOFU ASIMSIFU RAIS WAKATE ANATEGEMEA KITITA CHA MCHANGO, nia yake ilikuwa hizi million zilizopatikana. Askofu naye ajijue kuwa na yeye sio Mungu, kama anatetea uzembe itamgharimu

Ujue Kuna waumini wa dini ya Askofu huyo hapa, sasa kama wasema kiongozi wao ni mwongo anaabudu binadamu... shauri yako,,, lakini nakuomba uwe makini!
 
KILITIME

Hivi kuna shida gani kwa kamati ya bunge inayoshughulikia maswala ya Finance kuchunguza tuhuma kama hizi na pale inapobidi wanaomba msaada kwa wataalam? CCM na Serikali sasa hivi wanajiona na kufikiri hii nchi ni ya kwao pekee. Tanzania will remain but people will pass and you will be lucky to reach 80 yrs.
 
Last edited by a moderator:
Kilitime,
Alicho nacho Dr. Slaa si tuhuma tu. Anao ushahidi. Kuna vithibitisho vya akaunti za benki na namba zake. Hata ile mikataba ambayo mnadhani ni siri imeshavuja. Sikiliza kesho mahojiano yake na VOA. Saa mbili usiku ( saa za Tanzania) Bado kuna mengi yatafumuka.

Still ni tuhuma, mamlaka yenye uwezo wa kuhakikisha vielelezo vyako au ushahidi wako ni sahihi sio Jasusi, Kilitime, MKJJ, Kichwa Maji... ni Mahakama!!!
 
Basi tusubiri mahakama. Slaa anasubiri kwa shauku kubwa sana.
 
Still ni tuhuma, mamlaka yenye uwezo wa kuhakikisha vielelezo vyako au ushahidi wako ni sahihi sio Jasusi, Kilitime, MKJJ, Kichwa Maji... ni Mahakama!!!

akatuni001ur3.jpg

Si unaona nimerudi sasa mtanikoma bado nasubiri wanirudishie ile bastola yangu kibindoni.

Mahakama ya Tanzania chini ya serikali ya JK ambayo imemwachia muuaji Dito kwenda kuipigia debe kule Tabora.
 
Mahakama ya Tanzania chini ya JK ambayo imemwachia muuaji Dito kwenda kuipigia debe kule Tabora.

Du! Katiba inasema mahakama iko chini ya JK? Uwiiiiii Tunajenga kizazi gani hapa!!!!

Na ujue unawatukana majaji na Mh... Jaji Mkuu Ramadhani, please do not, watu wanajiheshimu bwana!!!

Hivi umesahau ni hukumu ngapi zimeenda against serikali??? tuwe wakweli kama watu ambao at least mara chache,,,tunapitia kwenye milango ya makanisa na misikiti au mibuyu!!!
 
Kilitime
Huyo aliyekuwa naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani hakuwa anahukumu, alikuwa anasuluhisha.Hebu tuambie wangapi walikwenda jela au kupata kifungo cha nje au kulipa faini serikalini??
Mfano wa Mwanakijiji haufai hapa hata kidogo.Yeye kaja hapa kaeleza kuwa alikosea kwa kuwa alileta taarifa mwanzoni kabisa kumbe baadaye hali ikawa tofauti.
 
Back
Top Bottom