List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Halafu kinachoudhi ni kuwa wamezirahisisha hoja zote kuwa zinahusu Rushwa. Sasa Mkapa kufanya biashara Ikulu nani kasema alipewa rushwa kufanya hivyo? Na Mkapa na Yona kujiuzia biashara kwenye kampuni yao wakiwa madarakani, ni nani alisema walitoa rushwa.. sasa ukiwatuma TAKUKURU kwenda kuchunguza rushwa wataipata?
 
bil sasa wewe ndugu haueleweki, mwenzao anaelezea kwa uzuri wewe unampiga vita kweli kuna kamaendeleo hapo?
 
Nadhani SISIEMU na Serikali yake wametafsiri neno UFISADI kama Rushwa tafsiri ambayo si sahihi hata kidogo.

Kibaya watoa tafsiri ya UFISADI kuwa Rushwa kwa makusudi ili kupeleka ujumbe kwa wananchi kwamba Dr Slaa, Zitto na Lissu walitoa tuhuma za Rushwa kumbe Tuhuma zao zinahusu Ukikaji wao wa kanuni,Taratibu na Sheria wakiwa viongozi wa juu wa serikali ya Tanzania kwa misingi ya kujitajirisha.
Madhummuni na Nia yao kuu ya kupotosha maana kuwafanya Wananchi waelewe na kuamini kwamba tuhuma za Dr Slaa na Lissu kwao viongozi Zilikuwa ni juu ya Rushwa tu ili kupunguza makali ya hoja na kuingiza kutu hoja yetu mkombozi.

Rushwa ni sehemu ndogo na muhimu sana ndani ya Ufisadi.

Ufisadi maana yake ni kutumia Heshima,Mamlakana na Utukufu ulionao ambayo ni dhamana uliyopewa na wananchi kupindisha Kanuni Taratibu na Sheria kwa faida na manufaa yako binafsi na familia yako au jamaa zako, marafiki na watu wengine wa karibu.

Mifano mizuri ya Ufisadi ni;
kubakiza wizarani Fedha iliyotengwa kujenga madarasa ya Shule za Sekondari na kuzitumia kwa Warsha na ma Kongamano wizarani nje ya Utaratibu wa bajeti.

Kujilipa mafao hewa au zaidi ya kiwango kitakiwacho.
Kuajiri mtu au watu kwa kutumia cheo chako.
Kumpeleka Mkeo au Mumeo kufanya Shopping London na new York kwa gharama ya fedha za wavuja jasho.

Kuingia Mikataba na mashirika ya nje kwa namna inayo likosesha kodi Taifa baada ya kupokea;
Rushwa ya kusomeshewa watoto Marekani na Uingereza
Kununuliwa nyumba South Afrika na London
Kupewa mamilioni ya Dola na kufunguliwa aacount Dubai
Kuhongwa ngono ya vimwana wa kizungu wenye chuchu za kuchongoka na macho ya gololi.
Ulimbukeni wa kupewa uanachama na kuingizwa kwenye Club kubwa za Matycoon wa Dunia walioko New York na Paris.
Na namna nyingine nyingi za kukiuka Sheria kwa misingi ya kujinufaisha.

Hiii ndo maana ya UFISADI.
 
Matatizo makubwa ya CCM, bado ninaamini kuwa yapo kwenye ushauri, na hasa Muungwana kama rais, kwa kweli nina tatizo sana na washauri wake wa siasa, kwa sababu anapaswa kuwa bigger than yaliyoandikwa kwenye hii article,

Wa-Tanzania wengi, hasa vijana wanamkubali Muungwana kama agent of change, na hasa jinsi alivyoweza kuikaba establishment, mpaka akawa rais, in the process hata na yeye aliwahi kuwashutumu kina Gama na Msuya, kuwa walikula njama za kumuangusha kwa makususdi asipate urais, mwaka 1995, je kuna aliyemlaumu kuwa anahatarisha amani kwa hayo maneno yake?

Hapana, WHY? Ni kwa sababu hata viongozi wa CCm walisha-sense kuwa time zimebadilika, wakanyamaza kimyaaa, halafu pia kwenye uchaguzi wa NEC, mwaka 2000, Muungwana, alipopigwa chini tena, mbona aliwatukana wajumbe wote wa CC, kule Zanzibar kama watoto, na hasa Mkapa, kwa kumfanyia ujanja kwenye kura zake, je kuna aliyemlaumu kuwa anahatarisha amani na hizo tuhuma zake? Na kwamba sasa yeye amekuwa hakimu, na prosecutor pamoja?

Kwakweli, ningemuomba Muungwana, awaangalie tena washauri wake wa siasa, ambao wanaonekana kutoelewa kabisa siasa za kisasa na kukumbatia siasa zilizopitwa na wakati, kwa sababu:-

1. kufukuzwa kwa Zitto, bungeni,
2. Orodha ya mafisadi,
3. Kuzomewa kwa viongozi wa CCM,
4. Kuvuja kwa mkataba wa Buzwagi,

I mean hizi ni political points, zinazohitaji a serious political response through a change of the way of doing political things katika jamiii yetu, Muungwana alipaswa not only kuzikumbatia hizi points kwa faida yake na CCM kwa ujumla, bali alitakiwa azi-hijack na kuzifanyia kazi kwa manufaaa ya CCM, na wananchi wa taifa letu kwa ujumla, badala ya yeye kushuka chini kwenye level za akina Warioba na Bomani, na kuwafanya waonekane kuwa message zao zina something to do na yeye Muungwana, maana zinafanana sana haswa kwenye point ya amani ya taifa kuchafuliwa, hoja ambayo ni hafifu sana ukifuatilia njia aliyoitumia kufikia urais wake,

Muungwana alipaswa, kukubali mbele ya taifa kuwa wananchi nimewasikia, pamoja na kwamba zilizotolewa ni tuhuma tu, lakini ninawashukuru kwamba mmezipokea bila ya kuvunja sheria zetu za nchi, nimeviagiza vyombo vyetu vya sheria kuzichunguza kwa makini tuhuma hizo nzito dhidi ya baadhi ya viongozi wakuu wa taifa, kwa sababu tunahitaji kuwa na taifa linaloheshimu the rule of law na demokrasia, sita-comment kitu chochote kuhusiana na tuhuma hizo kuepukana na ku-ifluence the outcome,

Lakini at the same token, wananchi nimewasikia tena loud and clear, kuwa kunahitajika mabadiliko ya kisiasa kwa kuanza na viongozi, na the buck stops here kwangu rais wenu. Sasa huu ni wakati mzuri kwa Muungwana to come through na ile ahadi yake kuwa hana ubia na Mtandao au mtu yoyote kwenye urais wake, kwa kuwatosa viongozi wote walioonyesha kuwa na uwezo mdogo katika kipindi chake cha utawala so far, halafu pia wale wote walioshindwa kwenye uchaguzi wa NEC, hii ndiyo ilikuwa nafasi nzuri ya yeye kukubali kura za wanachama wa chama chake CCM, kuwa mawaziri wote walioshindwa akina Ngasongwa, Mungai, na wengine wote wa ngazi za juu kuwa hawafai na busara za political correctness, zina-demand kuwatosa sasa nje ya cabinet, kwa sababu Muungwana apende asipende, kisiasa ukweli ni wananchi wanaanza kumuonyesha kuwa wana wasi wasi kama kumchagua hawakufanya makosa, meaning kwamba confidence ya wananchi kwake kiuongozi, hapa imepigwa kidogo inahitaji kujengwa tena, na pole pole na kwa uangalifu sana, lakini sio kwenda kuzungumza kwa padri kama alivyofanya, maana sasa hivi wananchi sio wajinga tena kujua kuwa kujichomoza kwa makanisa kila kona ya nchi sasa hivi kunaashioria tu kuwa nayo hiyo dini sasa ni biashara safi na yenye manufaaa,

Kuvuja kwa mkataba wa Buzwagi, ni fundisho la kuwepo baadhi ya viongozi wenzake wa juu wasioridhika na utawala wake, sasa tatizo sio ni nani hao, bali tatizo ni wanataka nini? Huenda wanayoyataka ni kwa faida ya taifa zima, sasa dawa ni kuwasikiliza na sio kuwatishia na usalama wa taifa au Takuru, au kuwabagua, Mkapa, pia yalimkuta haya, viongozi wenziwe wakamfanyia uhuni CCM ikashindwa ubunge wa Temeke na Bariadi, alipoingia tu na makiki yake, ingawa alikuwa mjanja na kukaa chini kuwasikiliza, ni bahati mbaya kuwa viongozi hao hawakuwa na nia njema kwa wananchi at large, bali matumbo yao tu, lakini Muungwana asi-assume kuwa in this case pia nia yao ni mabya bila ya kuwaiskiliza,

We can go on and on, lakini kwa maoni yangu Muungwana, anahitaji washauri wapya wenye kuelewa wakati tulionao, na ambao wanahitaji kutambua kuwa uchaguzi wa rais uliisha siku nyingi, sasa ni kazi, kupokewa kwake na wananchi wengi pale Aiport juzi ni dalili tosha kuwa bado wananchi wengi wana imani naye, lakini wana tatizo na wasaidizi wake, halafu Mtandao kwa ujumla wajifunze kusamehe wapinzani wao kiitikadi kwa faida ya taifa at large, kwa sababu msuguano wao so far hautuletei mema kwenye taifa, na pia viongozi wa CCM na serikali ndani ya bunge, wajifunze kusikiliza wabunge wao, badala ya kufikiri kuwa wao tu ndio wanaojua what is best kwa taifa na CCM, kwa sababu wabunge wengi wa CCM tulio ongea nao wanasema kuwa waliwaonya sana kuepuka na kumfukuza Zitto, bungeni lakini wakaziba masikio, matokeo yake sasa hivi wabunge hao wanacheka sana yanayojiri,

Ni wakati wa Muungwana sasa kuzinduka na kutathmini utawala wake, na the legacy anayoitaka kuwaachia wananchi na taifa kwa ujumla,

Mungu Aibariki Tanzania Yetu!
 
Honest, I think JK is insane or he is about to loose his mind? What you think? Tanzania Judiciary system is dead, total dead! sasa unadhani nani atapoteza muda wake kusubiri mpaka mahakama iamue ndio tulizungumze.

Mr president anataka kutupangia what to think,when to think, and how to make judgement. What i know Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, sasa nini tatizo pindi wananchi wanapo amua kuzungumzia rushwa ndani ya serikali?

Apart from that, what chuki does muheshimiwa talk about? Chuki has exist for couple of years between those who have and those haven't. It is my believe that people in democratics countries tend to judge their goverments on dail bases. So, why Mr president sound angry when his cabinet are accused that they are corrupted? I believe anachotakiwa muheshimiwa ni kuprove kwamba mkataba haukusainiwa Hotelini, na serikali haipati 3% kutoka kwenye migodi, na Karamangi hakusaign mkataba. Just look at the facts and prove us wrong Mr President. Kuwaita watu wamekuwa ma special investigators does not make any sense, lather it just show how dictator you are.

Tanzanian people have wait this long without saying anything. We have been victim of bad decisions from minority of the people. They decide what to do, and we're paying the price for their mess. There is no free lunch anymore Mr JK, NO MORE. We will say what we think need to said, and speak concern any wizi.
 
Dua,

Waliwaambia hao wanakijiji uliwapiga picha kwamba unakuja kuanika nyumba zao humu?
 
Baaada ya kuisoma hii article, ni kwamba ukweli au betweeen the lines wa ishu nzima uko kwenye hivi vifungu viwili, Mkuu Killtime, heshima sana kwa maneno yako ambayo ni clear kuwa ni ya mwananchi mstaarabu, na asiyekuwa na unazi,

Muungwana is right, kuwa so far ni tuhuma tu, ila tunataka kumkumbusha kuwa effort zake hazitoshi kwenye rushwa, asiwe na wasi wasi sana, lakini pia aheshimu changes za ki-maisha, ambazo ndizo haswa zilizompa urais against all the odds, ni hizo hizo changes zinazoendelea kisiasa katika wananchi wetu sasa hivi, na zilitakiwa zi-sart somewhere, na in some fashion, sasa kilichobaki ni pamoja na yeye sasa kuanza kubadilika ili awe on the top of the game za hizi changes za kisiasa, hakuna anyetaka kumpindua au kumfanyia matatizo, au kupunguza heshima yake, ila tu ni a wake up call,
Huko Nigeria, wao huwa wanapindua nchi, sisi ni makelele ya kuwazomea mawaziri na kuunywea chai mktaba wa Buzwagi, we are doing better than Nigeria na Psakistan kwenye hilo, kwa hiyo aongeze kazi na seriousness kazini, kwenye ishu ya Zitto na bunge, tumelikoroga wenyewe CCM sio siri tena, sasa tulinywe likiwa la moto, hakuna wa kumlaumu maana tunahitaji tu kuangalia kwenye kiooo kumpata aliyetuponza!

Isipokuwa next time asidanganywe tena na hawa mapadiri wanaotaka kumtumia tu kuchanga pesa za kanisa!

Heshima Mbele!

Kwa Message hiyo Natamani watu wake JK wangempelekea Ujumbe huo, Nakuheshimu kaka, especially kwa kuweka uzalendo mbele,,, uzalendo hauwezi kuwepo kwa ushabiki hata siku moja, uwe kwa watawala au kwa wapinzani!
 
This is the indication that PCCB is a wing for CCM and not for the nation interests. As a President he was to answer this without manetioning something against his intention versus corruption. If you are corrupt means you are dirty hence you desrve to get cleaned so that you fit for the feast you have set for us. We can not sit together with a dirty person and eat together, and if we tell you that you are dirty then you elaborate such like that then you deserve nothing and remember it's me who put you there where you are, time flies there will be time you will have to quit, and your dirtiness shall never perish ones you are out do it now. "Tempus fugit" JK clean your house!!!!!!
 
kusema kwelim viongozi wetu wa dini ni wanafiki wakubwa sana.kuna kiongozi mmoja wa dhehebu la kilutheri huwa akisimama madhabahuni anaipiga madojngo serikali kutokana na kutotimiza ahadi zake lakini siku moja akaja raisi kwenye fund raising fulani . eebwanaaaeeeee wacha aanze kumsifia jinsi serikali yake inavyofanya kazi kwa umakini mkubwa na kuleta maisha bora kwa kila mtanzania, sisi tunaomjua tukaanza kuguna na wengine kuondoka. Hao ndio viongozi wetu wa dini wa leo hii
 
Alberto Gonzales hires defense attorney By LARA JAKES JORDAN,

Associated Press Writer
2 hours, 15 minutes ago

WASHINGTON - Former Attorney General Alberto Gonzales has hired a high-powered Washington lawyer to represent him in investigations of mismanagement of the Justice Department. George Terwilliger, a white-collar crime defense attorney and the second-ranking Justice official in the early 1990s, was on the White House's short list last month to replace Gonzales.

Investigators are look into allegations that Gonzales lied to lawmakers and illegally allowed politics to influence hiring and firing at the department. Terwilliger said Gonzales, a close friend of the president's and a former Texas Supreme Court justice, maintains he did nothing wrong or illegal, and that hiring an attorney should not signal any guilt

Muuungwana, aaambiwe kuwa hata Majuu viongozi wa juu hutuhumiwa pia kama huyu Gonzalez, anatuhumiwa kwa kuendesha vibaya Justice Department, yeye amejiuzulu kwanza ili kuwapa nafasi wachunguzi wa Federal government, wanaomchunguza kisheria, baaada ya kutakiwa kufanya hivyo na bunge la huko USA,

kwenye demokrasia huko majuu, haya ya tuhuma ni mambo ya kawaida sana, sio kwamba kuna mtu anataka kuhatarisha amani na jamiii na kujifanya yeye ni hakimu na mchunguzi na prosecutor, hapana ni process tu ya kawaida katika demokrasia ambayo siku zote inaamini kuwa bina-adam ni selfish by nature, kwa hiyo under Capitalism system, huyu Bin-adam aruhusiwe kufanya anayoyataka as much as he wants bia kubughudhiwa na serikali, lakini serikali ni lazima iwe extra careful naye, at all the times na ni lazima i-regulate kwa makini kila anachofanya ama sivyo ataanza kuleta mambo ya monopoly na arrogance za kujifanya hajui sheria,

That is all, Wa-Tanzania tubadilike kwa faida ya taifa, badala ya kukumbatia mabadiliko yenye kunufaisha matumbo yetu, lakini inapotokea time kutaka mabadiliko kwa faida ya wananchi wote, basi ni ukali tu na kutafutana uchawi na kwamba kina Zitto na Dr. Slaaa, wanataka kuchafua amaani! Tuache hizi nyepesi nyepesi!
 
pamoja na kwamba jk anasema anazo list za majambazi, mafisadi, na wauza unga kwa muda mrefu, haiaminiki kuwa ana ifanyia kazi. mawaziri na wasaidizi wake wanazunguka mikoa yote, hata ile ambayo wapinzani hawakufika kama singida, wakihubiri juu ya uongo wa tuhuma za upinzani bila kuthibitisha uongo huo. ni vipi jk afanyie kazi taarifa ambazo ameagiza zipondwe.

nadhani muda umefika kwa ndoa ya kanisa na serikali isiyo kuwa na ndini ivunjwe. kanisa litumie njia takatifu kutafuta fedha za kueneza habari njema badala ya fedha chafu za wafanya biashara wanaoletwa na jk kwenye harambee.
 
JK lazima awe tayari kuchukua hatua na sio kuwatisha watu pamoja na ukweli kuwa katiba inamruhusu yeye kuwa hakimu kwa kuamuru kumfunga mtu bila maelezo yeyote , akipenda atumie na nguvu hizo ili kumnyamazisha slaa na wengine .

Hivi ni nani aliyedhibitisha kuwa wale wabunge wa Arusha walitoa ama walikuwa wakitaka kutoa rushwa?mbona tuhuma zao ziliwapeleka mahakamani moja kwa moja within a two days?

Nani alitakiwa kutoa ushahidi kwanza pale wanapokamatwa mahakimu wakituhumiwa kupokea rushwa yshilingi elfu kumi?

Askari wa usalama barabarani wao kila kukicha tunaambiwa kuwa wamepekwa kwa pilato eti wakila rushwa,

Kuna ugumu gani kwa hawa vigogo waliotajwa na aliyetaja kaweka wazi kuwa yupo tayari kuweka ushahidi wazi, na mwingine spika alisema kampelekea mwanasheria mkuu wa serikali hivi huyo mwanasheria mkuuu ameshindwa kusema kuwa tuhuma ni uongo ama ni ukweli ama kuwafikisha mahakamani hawa watuhumiwa?

Hapa ndio utajua kuwa Tanzania sheria ni kwa ajili ya wale wasiokuwa na madaraka makubwa ya kisiasa.

JK chukua maamuzi magumu uliyowahi kutuahidi la sivyo hata wewe utaanza kuzomewa laivu....na hili litakuwa aibu kubwa la mwaka.

Askofu Laizer , wacha kumpaka mafuta mfalme ile hali unapaswa kukemea hiyo hali.

Zimeletwa mvua za wanaoabudu ngombe,BUTHA wa kule tbado mnakaa kimya nchi iletewe mvua na wasiopmwabudu Mungu ALIYE HAI, OLE WENU MNAOWAPOTEZA HAWA MAANA YAFAAA MFUNGIWE JIWE KUUU LA KUSAGA NA MTUPWE KILINDINI MWA BAHARI.
 
Killtime;
Watoa hoja hawakuhukumu, Huyu Padri au Askofu - ni Mfarisayo na anamsifia mfalme mla rushwa. Watanzania msihadahike, mnawalaumu mawaziri kiasi kwamba sielewi kama mnajuaje serikali inaendshwaji. Organisation chart, ni ile ile, what a minister endorses the president knows; and what the minister will part with the president will know, it is a relations between a parasite and an organ (symbytic); Mkapa aliiba millions bila mawaziri kujua? au you're telling me if Lowasa is a billionaire as others are saying in this forum JK is poor? or RA and the like are corrupting the system, you're telling me the president doesn't benefit in one way or another? The issue here, i will not attack Karamagi or any minister, the president himself is hiding behind the ministers and Mafarisayo like baba askofu to threaten the people! The president should be a culplit number 1! Especially if he doesn't act!


Huyu jamaa yeye mwenyewe ndiyo fisadi nambari moja, na anavyoendelea kushangashanga na kuuza sura na porojo zake za vijiweni ndiyo inadhihirisha kabisa. Tatizo ni kwamba hajui maana ya kuwa kiongozi na hususan rais wa nchi. Labda akisoma hii nukuu hapo chini ataelewa kidogo.

" In his farewell address to the American people given in January 1953, President Harry S. Truman referred to one of his simple concepts, "The President--whoever he is--has to decide. He can't pass the buck to anybody. No one else can do the deciding for him. That's his job".
 
Mzee Es heshima yako mzee . Kwa mara nyingine umeongea mambo mazuto na mimi najitokeza kusema kwa hili umetetea Taifa langu kwa dhati bila unafiki .Ila natofautiana nawe kwenye JK kuwa anapendwa na ndiyo maana watu walijaa kumpokea uwanjani akitoka Ziarani.Wale walikuwa ni wana CCM wengi tu na si watanzania wa kawaida na wote wale walitumwa na kutumiwa kum please Mkuu maana kama ujuavyo anapenda makuu kama ulivyo ona anapokewa an lundo la mawaziri nk .

JK is never a serious man na hawezi kusema lolote kwa kuwa kitendo cha kwenda Mahakamani itabidi kufumua mikataba yote hata ile IPTL na amesha onywa na Majaji wazoefu na yeye anaanza kucheza ngoma zembe ya kukemea .It is time aonyeshe kwamba he is a leader na kwamba he meant what he promised lakini najua hawezi hata mara moja ku deliver itabakia hadithi Slaa kamshika pabaya .
 
Ila natofautiana nawe kwenye JK kuwa anapendwa na ndiyo maana watu walijaa kumpokea uwanjani akitoka Ziarani.Wale walikuwa ni wana CCM wengi tu na si watanzania wa kawaida na wote wale walitumwa na kutumiwa kum please Mkuu maana kama ujuavyo anapenda makuu kama ulivyo ona anapokewa an lundo la mawaziri nk .

Mkuu heshima ikurudie,

CCM ni chama cha siasa, na sio chama cha upadiri au charity, kazi yao ni moja tu nayo ni siasa, wananchi karibu wote katika forum hii tunakubaliana kuwa siasa ni mchezo mchafu unaochezwa na viongozi wachache wachafu, lakini hawavunji sheria za nchi yetu katika kuucheza,

Mkuu wangu ni makosa makubwa katika siasa kujivalisha kilemba cha ukoka, kwa sababu kama maneno unayoyasema ni kweli au sawa, basi Chadema ndio waliopaswa kushinda urais uchaguzi uliopita, lakini it was to the suprise hata ya mwenyekiti wa Chadema, Muungwana alipomshinda tena kwa kura nyingi sana mpaka alisema kuwa hawaelewi wananchi wa bongo, baada ya uchaguzi,

At this time and point ni vizuri kukubali kuwa Muungwana, ana wapenzi wake politically wa kudumu, ambao they do not care about his record wala Buzwagi, na hiyo ndiyo base kubwa na muhimu sana kwake, maana ni wengi sana, usi-underestimate hiyo mkuuu, maana sifa za Muungwana zilianzia Dar na kusambaa kila kona ya bongo, just because yeye ni Muungwana, sio kwa sababu amefanya nini madarakani, kwa hiyo it will take Dar kwanza kuivunja hiyo scenario ya Muungwana kupendwa bila sababu kisiasa, so far kwao wao upinzani hawajawapa sababu hiyo, maana mambo ya Buzwagi, mafisadi, na BOT ni too much and very complicated kwao kuyaelewa, ndo maana mpaka leo mjini Dar hajazomewa kiongozi yoyote wa CCM, as opposed na huko mikoani, ndio maana hata nyongeza ya mshahara imelengwa huko nje ya Dar, as long as Muungwana is involved na timu yetu ya taifa ya soccer, na upenzi wa private kwa Yanga, politically he is fine na Dar,


Anyway to make a story short, Muungwana ana strong base ya kisiasa Dar, au mikoa yote ya Pwani na hawa wananchi wa Pwani, ambao wengi wao pia ni wakuja kutoka Bara, huwa wana-ifluence kubwa sana kimawazo over wananchi wa bara, ndio maana wananchi wengi wa Bara hukimbilia mijini, CCM wanaweza kununua wananchi mikoani kumpokea Muungwana, lakini hawahitaji kufanya hivyo Dar, kama vile ambavyo Freeman, hahitaji kununua wananchi kumpokea akienda Hai, hizo ni fact of life bila hata siasa! Ingawa recently upinzani wamefanya kazi nzito katika kuhamasisha, lakini bado Muungwana ni mzaliwa wa Pwani!
 
Kikwete kaingia na mafisadi ambao ndio wanaendesha nchi. Huwezi kuwa rafiki wa mfisadi usiwe fisadi, fedha za kampeni ya Kikwete zilitoka kwa mafisadi walizipata kifisadi na nchi itaendeshwa kifisadi na mnyonge atalia.

Ninaiona siku ipo karibu sana kila mtanzania atachukua mgawo wake kutoka kwa mafisadi, hiyo siku ni kitimtim.

Tayari watanzania wameshajua wanaliwa, kilichobaki ni kuwajengea kujiamini tu sasa halafu kuwaonyesha mafisadi chama yetu kubwa. Lazima kuwaelimisha wananchi nini wajibu wao kwa serikali na nini wajibu wa serikali kwa wananchi.

Je tutafanyaje JF isomwe na watanzania wengi waliopo vijijini?
 
Kikwete kaingia na mafisadi ambao ndio wanaendesha nchi. Huwezi kuwa rafiki wa mfisadi usiwe fisadi, fedha za kampeni ya Kikwete zilitoka kwa mafisadi walizipata kifisadi na nchi itaendeshwa kifisadi na mnyonge atalia.

Ninaiona siku ipo karibu sana kila mtanzania atachukua mgawo wake kutoka kwa mafisadi, hiyo siku ni kitimtim.

Tayari watanzania wameshajua wanaliwa, kilichobaki ni kuwajengea kujiamini tu sasa halafu kuwaonyesha mafisadi chama yetu kubwa. Lazima kuwaelimisha wananchi nini wajibu wao kwa serikali na nini wajibu wa serikali kwa wananchi.

Je tutafanyaje JF isomwe na watanzania wengi waliopo vijijini?
Habari zenu za masiku wa ndugu wote!
Mh. JK ni mshiriki wa yote yanayoendelea sasa na kwa kulielewa hilo ndiyo maana anazidi kufanya usanii kwa kuwakingia kifua mafisadi wenzake!
 
Field Marshal Es,
Unajua uncle maneno yako mazito sana na ndio REALITY haswaaaa!

Wapinzani wote humu mnatakiwa kujifunza kwanza tabia za Wadanganyika kabla ya kutoa hukumu zenu kwani Wadanganyika tumepoteza ama niseme bado hatujajenga kitu kimoja muhimu sana... ELIMU. Kwetu sisi elimu ni ya darasa na tunatumia sana cookbooks kiasi kwamba kilichoandikwa ndio ukweli pekee. Mathlan, viongozi wa dini wamekwisha muita JK ni NABII!...Yaani imekwisha andikwa!...Yeah! reality inasema huwezi kuwa rais kama hukuandikiwa!

Kwa waumini mtaelewa uzito wa neno hili na si rahisi kuondoa nyoyo za watu walioukubali unabii huu. Itachukua nguvu kubwa zaidi ya lawama na kunyooosha vidole kuweza kutengua imani hii ya Mdanganyika.

Kumbukeni pia kwamba - Mwizi ambaye hunufaisha Familia yake hupewa sifa kubwa kuliko mtu yeyote anayejali sana maslahi ya taifa na kufa maskini!..Hii ndiyo imani ya Wadanganyika wengi.. na ukibisha au kupinga imani hii utaonekana mchawi wewe!

Kila mtu anataka kipande hiki cha mkate na sii rahisi kuwaondoa maskini ktk fallen ya kujipatia riziki na sifa ya kwamba hata mimi nilikuwepo kukuunga mkono!

Muungwana kisha jengewa ngome nzito toka wakati wa Nyerere akionekana kama kiongozi Mtarajiwa isipokuwa alikuwa akisubiri siku yake.. na siku hiyo imeisha timia na wafuasi wake ni wengi sana pamoja na kwamba taratibu wanapungua!

Kwa hiyo hata vyama vya Upinzani ni lazima muwe makini sana katika kupanga hartakati zenu dhidi ya Utawala wa CCM maadam nabii huyu bado yupo madarakani. Na pengine hata kumweka Msalabani haiwezi kusaidia kitu ktk kuondoa imani za wengi walokwisha kunywa mvinyo wa imani ya Chukua Chako Mapema.
 
Mwinyi: Tuhuma zisipuuzwe




na Tamali Vullu na Irene Mark



MADAI dhidi ya kushamiri kwa ufisadi, rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, jana yalipata sura nyingine baada ya Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, kuibuka na kusema kuwa madai hayo hayapaswi kudharauliwa na viongozi.
Akizungumza katika kongamano la kuadhimisha miaka minane tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere jana, Mwinyi alisema kuwa watu wanaotoa madai hayo wana akili na wameamua kufanya hivyo kutokana na hali ya mambo wanayoishuhudia.

Wakati Mwinyi akitaka kutopuuzwa kwa tuhuma hizo, mwanaharakati mwingine, Jenerali Ulimwengu, naye ameonya kuwa watu wanaodaiwa kuwa mafisadi, wanahatarisha kuanzishwa kwa vita nchini.

Akizungumza katika kongamano hilo lililoandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam na kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwinyi alisema akili za watu hivi sasa zimepanuka na ndiyo maana wanaweza kuikosoa serikali hadharani.

"Haya yote ni matunda ya miti aliyoipanda Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye alikazania suala la elimu, ili watu waondokane na ujinga," alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, hivi sasa watu wako huru kuikosoa serikali na akasema kufanya hivyo ni ‘ruksa'.

"Sasa watu wanaikosoa serikali left, right and centre (kushoto, kulia na katikati), lakini hakuna anayetishiwa wala kukamatwa… haya ni matunda ambayo tunavuna kutokana na juhudi za Mwalimu Nyerere, ambaye alitoa uhuru wa watu kuzungumza na kukosa.

"Kuna mambo mengine yanazungumzwa katika magazeti, yanakereketa, lakini (mimi) sikasiriki… na baadhi yanayokosoa yana maana na yakifanyiwa kazi yanaweza kuleta maendeleo katika nchi yetu," alisema Mwinyi.

Alisema siasa ya kujitegemea haina makosa na wala haitakuwa na makosa, na akashauri iendelee, kwani kinachotokea sasa ni kutofautiana katika njia za kutafuta maendeleo ya nchi.

Pia, alimsifia hayati Baba wa Taifa kwa kueleza kuwa hakuwa mbinafsi na kwamba mpaka anastaafu hakuwa na nyumba wala shamba.

Alisema Mwalimu Nyerere aliacha kazi ya ualimu iliyokuwa na mshahara na kuingia kuongoza chama kilichokuwa na posho pekee, kwa lengo la kutetea wanyonge na kwamba alikataa kujinufaisha binafsi.

"Nani kati yetu anaweza kufanya hivyo? Hii inaonyesha Nyerere alikuwa mtu wa aina gani. Hakuwa na tabia ya ubinafsi," alisema.

Alitumia nafasi hiyo kuieleza CCM Mkoa wa Dar es Salaam kuwa, wamechelewa kuanzisha kongamano la aina hiyo, kwani walipaswa kuanza mapema baada ya kifo cha Mwalimu Nyerere.

Naye Waziri katika Ofisi ya Rais, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Jamii, Kingunge Ngombale-Mwiru, alitoa mada kuhusu tafakari ya falsafa ya Mwalimu Nyerere, alisema njia nzuri ya kumuenzi ni kusikiliza hotuba zake.

"Kwa kutumia hotuba za Mwalimu Nyerere tunaweza kujifunza zaidi na kuyafanyia kazi, hii ndiyo njia kubwa ya kumuenzi Mwalimu Nyerere," alisema.

Alisema hivi sasa watu wengine wanasahau adui dhuluma, lakini akasema hiyo inawezekana akawa ni adui mkubwa kuliko wengine wanaotajwa.

"Tumezoea kusema Mwalimu alitufundisha kupambana na adui ujinga, maradhi na umaskini na kusahau dhuluma. Hii inawezekana ndiyo ikawa inasababisha haya mengine kutokea.

"Watu wa CCM hili tulitafakari sana, kwani tuna viongozi wanaopenda kufanya dhuluma," alisema Kingunge.

Alisema kuwa rushwa ni aina ya dhuluma, kwani inamnyima mtu haki yake, lakini cha kushangaza wakati mwingine watu wanaishangilia. Alisema hivi sasa viongozi wengi wanaweka mbele masilahi binafsi na kusahau ya taifa.

Akizungumza katika kongamano kama hilo, lakini lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ulimwengu alisema watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi wanahatarisha amani ya nchi iwapo hawatakuwa tayari kutekeleza maagizo ya hayati Mwalimu Nyerere ya kujikosoa na kujirekebisha.

"Wachochezi wa vita ya baadaye ni mafisadi wa leo," alisema Ulimwengu, hali iliyosababisha makofi na nyimbo kutoka kwa wanazuoni na baadhi ya watu waliohudhuria wakiwemo viongozi wa serikali, wanasiasa, mabalozi, maprofesa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU), Dk. Salim Ahmed Salim.

Ulimwengu alibainisha kuwa sera na mipango mizuri inayotekelezwa ndiyo matokeo ya amani na utulivu ulioimarishwa na hayati Baba wa Taifa.

Kuhusu mwelekeo wa nchi, Ulimwengu alisema hivi sasa ukoloni unarudi kwa kasi kuliko ilivyokuwa kabla ya uhuru.

"Tanzania na Afrika nzima inazidi kuwa koloni la weupe kuliko ilivyokuwa wakati wa ukoloni, siku hizi viongozi hakuna, hawa ni watawala," alisema na kushangiliwa tena.

"Uongozi umegeuka kuwa ni bidhaa inayonunuliwa, mtu anakaa Marekani anapiga hesabu ya kununua jimbo hadi jimbo kwa dola zisizozidi bilioni tatu.

"Wananchi tupo sokoni tunauzwa, mtu anakupigia hesabu ya kuchukua Ikulu ili kutawala nchi kwa dola bilioni kadhaa… fedha inanunua nchi," alisema.

Ulimwengu aliwataka watawala kumuenzi Baba wa Taifa kwa kutekeleza aliyokuwa akipigania ili kudumisha haki, amani na ujamaa kwa kukataa kutawaliwa.

Aidha, aliwataka kufahamu kuwa wananchi si wajinga na kuwashauri wanazuoni hao kuanzisha chama cha ujamaa kwa lengo la kupambana na nguvu mpya ya ukoloni na ubeberu.

"Nyerere kabla ya kifo chake alikuwa mzee lakini alikuwa na mawazo ya ujana, nawashauri vijana wasomi, undeni chama cha ujamaa halafu mwende kwa Msajili wa Vyama vya Siasa muone kama mtasajiliwa," alisema.

Aliongeza kuwa woga wa watawala baada ya Mwalimu Nyerere unasababisha vurugu za mara kwa mara, huku akitolea mfano migomo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Kuhusu misaada tunayopata, Ulimwengu alibainisha kuwa enzi za uhai wa Baba wa Taifa wakati wa Azimio la Arusha mwaka 1967, aliwataka wananchi kufahamu kuwa misaada ya wahisani itaifikisha nchi mahali pa kushindwa kuwa na sera binafsi na kuzitekeleza.

"Nilitamani kukutana na (Waziri wa Fedha) Meghji, siku chache kabla ya kusomwa kwa bajeti ili nimuulize amekuja lini kutoka Washington… siku hizi bajeti inapangwa Ulaya kwa e-mail tu, hapa waziri ana-download kisha anaenda bungeni kuisoma," alisema Ulimwengu.

Source:
Tanzania Daima.

Hadi kieleweke.
 
"Nilitamani kukutana na (Waziri wa Fedha) Meghji, siku chache kabla ya kusomwa kwa bajeti ili nimuulize amekuja lini kutoka Washington… siku hizi bajeti inapangwa Ulaya kwa e-mail tu, hapa waziri ana-download kisha anaenda bungeni kuisoma,"

ndio utaratibu wao wa kazi,ukuona hata majuzi muungwana ilibidi asogeze muda wa kusoma ratiba mpaka malize kuipitia hotuba sababu alikuwa hajaisoma,unaona nchi inaongozwa na watu wengine wasanii zaidi ya Rais,
hasa hasa mwandishi wa El manaake ,mifano ambyo huwa anampa ndanda huwa ni pumba tupu..angali sula la njiwa na ndege inayopaa(toka lini ukaona mwandishi wa habari aliyesoma Mass Com akajua mambo ya Economics..??>
 
Back
Top Bottom