List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

..kuna wakati watu wa ulaya walikemewa wasiingilie mambo yetu!

..sasa,kama ndo tunaombaomba kwao,wataacha kutuiingilia?

..yaleyale ya nnataka sitaki!

Tatizo kubwa la kutegemea misaada/mikopo ni kukosa uhuru wa kujiamulia mambo yetu...ndio ukoloni wenyewe huo. Simple and clear.

Tanzania yetu inasikitisha kwa uongozi tulionao.
 
Jamani naomba tumweke Post Mrema ili alipwe Pension ya Viongozi, Maana nakumbuka alivyo fukuzwa au kuondolewa Madarakani, alinyimwa mafao yake/pension, wakati aliondolewa kwa kupingana na Viongozi kuhusu Ufisadi. Mwenzie Maali Seif kapewa sasa. Na pia kuna watu wengine pia ambao wako ktika mkumbo kama huo.
 
Mwanakijiji itakuwa saa ngapi, Please confirm as that is so important to follow
 
hivi huyu mwinyi yeye si FISADI?

mtu wa pwani
yeye ndiye aliyewalea hawa mafisadi...yeye ndiye Mwallimu wake mkuu,hii ni siasa tu ya mzee Ruksa,anataka kusema suala la Loliondo alikuwa hajui?hajui kwamba mkewe ndie aliwafumbua watu kuwa mafisadi?
anafikiri mama kmkapa lijifunzia wapi ujasiriatanza wapi kama sio kutoka kwake..
 
Waliotangaza kumshitaki Dkt. Slaa wanywea

VIGOGO wa Serikali waliotajwa kwenye orodha ya tuhuma za ufisadi na kutishia kufungua kesi dhidi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, kwa walichokiita kuwakashifu, wako kimya mpaka sasa.

Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata baada ya kufuatilia kwa takriban wiki mbili na kuthibitishwa na waliotishiwa kufunguliwa kesi na vigogo hao, akiwamo mwanasheria wa CHADEMA ambaye ni wakili wa kujitegemea, Bw. Tindu Lissu na uongozi wa gazeti la Mwana Halisi zimeeleza kuwa hadi sasa hakuna kesi iliyofunguliwa.

"Hakuna kesi iliyofunguliwa dhidi yetu, kama wangefungua kesi si wangetuita kutueleza hata kwa maandishi?," alihoji Bw. Lissu alipozungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana.

Kauli kama hiyo ya Bw. Lissu pia ilitolewa na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwana Halisi, Bw. Saed Kubenea, ambaye alisema hawajapokea hati yoyote ya kuitwa mahakamani.

"Mtu anayelalamika ndiye anayepaswa kwenda mahakamani sisi hatujapata hati yoyote ya kuitwa," alisema Bw. Kubenea.

Gazeti hilo lilitishiwa kufunguliwa kesi na vigogo hao kwa madai ya kuchapisha na kusambaza habari zilizowatuhumu kwa ufisadi.

Takribani miezi minne iliyopita katika mkutano wa hadhara uliitishwa na umoja wa vyama vinne vya upinzani katika viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam, Dkt. Slaa alitaja orodha ya vigogo 11 akiwahusisha na ufisadi.

Baadhi ya vigogo ambao walitajwa kwenye orodha hiyo na kutishia kwenda mahakamani iwapo hawataombwa radhi na kulipwa fidia ni Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bw. Gray Mgonja.

Mwingine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Bw. Patrick Rutabanzibwa, ambaye pia alitaka aombwe radhi, vinginevyo aende mahakamani.

Mtuhumiwa mwingine, mwanasheria mkongwe, Bw. Nimrod Mkono, alishasema hana haja ya kwenda mahakamani kwani Dkt. Slaa, hana fedha za kumlipa fidia.

Pamoja na kuandikiwa barua ya mawakili wa Bw. Karamagi wakimtaka Bw. Lissu kumwomba radhi na kumlipa fidia ya sh. bilioni 10, alikaririwa na vyombo vya habari hivi karibuni akisema kama Waziri Karamagi anataka kwenda mahakamani aende "lakini itabidi aithibitishie uadilifu alionao anaotaka ulindwe na mahakama."

Hivi karibuni, baada ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Daud Balali, vyombo vya habari vilimkariri Dkt. Slaa akihoji Serikali kutowachukulia hatua vigogo aliowataja katika 'orodha ya mafisadi'.

"Orodha ya mafisadi imeishia wapi, wananchi wanataka kujua hawa watachukuliwa hatua lini, wengi walitishia kwamba watanipeleka mahakamani, lakini hakuna hata mmoja aliyethubutu kufanya hivyo," alisema Dkt. Slaa.

Gazeti hili lilipofuatilia kwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ili kujua kama vigogo hao wamefungua kesi juhudi hizo zilishindikana kwa kilichodaiwa ni wahusika kuwa likizo.

Tangazo lililobandikwa katika ubao wa matangazo wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam lilieleza kuwa Mahakama Kuu na ya Rufaa nchini zimefungwa kuanzia Desemba 15 mwaka jana hadi Februari 4 mwaka huu kutokana na watumishi wa mahakama hizo kwenda likizo ya kawaida.

Kesi na shughuli nyingine za mahakama hizo zitaendelea kama zilivyopangwa kuanzia Februari 4. Hata hivyo chanzo chetu kutoka ndani ya mahakama hiyo, kilieleza kuwa hadi wanakwenda likizo, hakuna kesi iliyokuwa imefunguliwa ya vigogo hao.

Waziri Karamagi alipopigiwa simu yake ya mkononi jana ili aeleze sababu za kuchelewa kufungua kesi kama alivyotangaza, alisema yuko kwenye ziara ya Rais Kikwete mkoani Kagera, hivyo hakuwa katika nafasi ya kulizungumzia.

"Hapa niko katika ziara ya Rais, subirini nikirudi Dar es Salaam ndipo mniulize hilo," alisema Bw. Karamagi.

Source: Majira
 
I don't remember if I ever did bring this report to you guys; Kama sikufanya hivyo, naomba niwasilishe report hii niliyoiedit some months ago. I think it'll make sense of "what happens here". Ni report iliyotokana na paper ya Dr. Slaa a little while ago. I think it'll be a very good read for it contains some statement of facts and his own experience since "the List of Shame" came out.
 
Attachments

Certainly,

You did earlier, here it is:

corruptionintanzania[1].pdf

and this topic includes other ATTACHMENTS like:

Orodhayaaibu.pdf

List of shame in Tanzania-mafisadi.doc
 
Kabla ujaanza kuwa na doubt na Dr Slaa au pengine hii ilikuwa ni kibiashara zaidi
 
Naomba niwakumbushe tu orodha ya mafisadi kama ilivyoorodheshwa na Dr. Slaa katika mkutano uliofanyika Mwembe Yanga, Temeke tarehe 15 Septemba, 2007.

1. Dr. Daudi T.S. Balali - sasa marehemu ?
2. Andrew J. Chenge - mgombea Ubunge kupitia CCM, Bariadi.
3. Basil P. Mramba - mgombea ubunge kupitia CCM, Rombo.
4. Gray S. Mgonja - Kaibu Mkuu mstaafu, Hazina.
5. Patrick P. R. Rutabanzibwa - Katibu Mkuu mstaafu ?
6. Nazir Karamagi - Waziri mstaafu.
7. Nimrod Mkono - mgombea ubunge kupitia CCM, Musoma vijijini
8. Rostamu Azizi - mgombea ubunge kupitia CCM, Igunga.
9. Edward Lowassa - mgombea ubunge kupitia CCM, Monduli.
10. Benjamin W. Mkapa - Raisi mstaafu, CCM.
11. Jakaya Mrisho Kikwete - mgombea Uraisi kupitia CCM

Kikwete kwa sasa ndiye mlinzi wao mkubwa na CCM ndiko waliko salama na wanakohifadhiwa - Kazi kwetu wananchi tarehe 31 October, 2010.
 
Watanzania tu wajiga kweli, pamoja na ufisadi wao bado tunawashangilia
 
Pengine wengine hawafahamu maana ya ufisadi na pia hatuhusianishi kati ya ufisadi na maadili ya uongozi wa umma.
 
f.png

Duu!Hii kali ya mwaka!WTH!??
 
Wametakaswa na Kikwete wamekuwa safi sana - tabu tukiwachagua tena watachafuka upya, na uchafu wao utaturukia kwa uhakika.
 
Hao watu waliopo kwenye hiyo orodha bila shaka wana woga wa kutisha siku hizi. Maana Slaa atakapochukua nchi ataifanyia kazi. Watachunguzwa, hata Balali itabidi achunguzwe kama kweli hayupo nasi tena.
 
hivi chenge, anamtii amri ya mahakama au amri ya jk, cause amekaidi amri ya mahakama
 
Back
Top Bottom