List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Hongera sana Dr Slaa kwa kuwataja, nadhani hii imesaidia sana ujenzi wa barabara vijijini, kupeleka maji, umeme na huduma muhimu. Hii ya kutaja mafisadi ndio iwe sera ya CHADEMA inasaidia sana.

Bila shaka huelewi hata maana ya ulichoandika. Kupeleka maji na Umeme ni wajibu wa kimkataba wala sio hisani. Subiri muda unakaribia mtoe hesabu za ulaghai mlizofanya na ahadi lukuki zisizotekelezeka. Mnabaki kunyofoa vipengele vya sera za CDM na kuzitekeleza mkidhani wananchi bado wamelala.
 
Poleni sana sasa mnapigana ndani na nje. Yaan mngependa kusimamia hoja ya ufisadi lakini bahati mbaya listi anayo Zitto sasa inabidi mu discredit hiyo list. Kidumu chama cha mapinduzi.
Viongozi wote wa Chadema wanajua kuwa list anayo Zitto wao wanataka wapewe kina Lema.

Yaani Zitto kapambana peke yake kutafuta hiyo list kirahisi tu ampe Dr.Slaa au Mbowe.

Chadema wana wanajitapa kuwa chama makini wameshindwa kweli kuitafuta hiyo list.
 
Last edited by a moderator:

Kwahiyo kimsingi mnakubaliana na hiyo List sio?
Kuna haja gani ya kuendelea kuongoza?
Kigumu chama cha Mapuuzi...
 
Kwa mujibu wa Dr.Slaa mpaka sasa hivi Chadema hawana sera wala ilani ya uchaguzi refer majibu aliyotoa alivyokimbia mdahalo, sasa wamenyofoa wapi hizo sera?
 
Hii ndio list of shame....lowassa yupo na jamaa mmoja anaitwa kikweli
 
Kwahiyo kimsingi mnakubaliana na hiyo List sio?
Kuna haja gani ya kuendelea kuongoza?
Kigumu chama cha Mapuuzi...
Pro-Chadema leo wapo upande wa CCM wakipambana na Zitto.

Teh teh teh
 
Zitto amesema atataja majina ya watu wenye akaunti Uswis, sasa ajenda ya pale Ufipa leo ni kutafuta kila linalowezekana kuonesha kuwa hata babu yao aliwahi kuwika hapo zamani.
hahahhaha wanakumbushia kwamba nao walijikongoja
 
Yaan tokea wasikie Zitto atasimama pale Mwembeyanga wanaweweseka kweli, mara watatoa mkanda wa bomu la Arusha mara hili ili mradi tu kutaka kumficha Zitto.

Pia wamepagawa sababu Dj pia yumo kwenye orodha
 
Kigumuuuuu!
Sasa unakiri kuwa Zitto a.k.a Yuda, ni mali yenu na alivyo navyo
mnavijua kwakuwa mmemgawia.
Huoni hiyo inawafanya kuwa mnapambana na Zitto badala ya CCM? Miezi mitatu kabla ya uchaguzi nyie mpo tu na Zitto ambaye hana hata kiti cha ubunge badala ya kupambana na CCM yenye viti 200 na ushee
 
hii ndio list of shame....lowassa yupo na jamaa mmoja anaitwa kikweli

Huyo nambari wani kama ilivyo chama kikubwa amerudi tz?kura atajiandikisha huko us au?
 
Karamagi Rostam ni team Lowasa silkiliza baraza LA mawaziri mafisadi
Ask
 
List Ya Mafisadi Ndio hii Ilitolewa na Dk Slaa...Da na sie Watanzania noma uwa kama bendera fuata upepo ya msingi tunayweka sebureni ya sebureni tunapeleka chumbani.My beloved Country Inatakiwa kubadilika sana tena sana na Mungu kaisikia mabadiliko yote November 2015
 
Unajua hii list ya majina ya watu wenye akaunti Uswisi Dr.Slaa alikuwa anataka apewe yeye Zitto akakataa, bifu likaanzia hapo.
Zitto hana list yoyote wala account labda ana list waliofeli kujiunga naye wakati wanahamasa na mahaba kama wewe Ritz.
 

Mkuu wanakuelewa vizuri tu - we sema hawataki kuelezwa ukweli, wanafikili wakipata list basi hilo tu linaweza kubadirisha upepo wa kisiasa nchini!!!
 
lowasa kila takataka yumo,du jamani hii ni hatari na wanaomfata wote wani wezi tu,asa wale wenyiviti awana akili kabisa ,
 
1,lowasa
2,chenge
3 Rostam
4,Karamagi
timu inayotumia lowasa kuingia madarakani ,ccm ole wenu mpitishe hii takataka mtajua mbichi na mbivu.
 
Aisee hii ni fedheha kwa nchi, ni Aibu Kubwa, haipendezi kabisa, na kila siku tunaomba Mungu aibariki nchi yetu. Inatia Huruma. Mungu atusamehe sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…