List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania


Umetoka povu tu hapa
 
Unajua hii list ya majina ya watu wenye akaunti Uswisi Dr.Slaa alikuwa anataka apewe yeye Zitto akakataa, bifu likaanzia hapo.
mkuu usipotoshe jamii andiko liko wazi hapo juu huo ndio ukweli.list of shame itabaki hivyo ,suala la fedha za uswisi hapa halimo .
 
Mzalendo wa nchi hii alijitoa mhanga kututajia mafisadi wakimo marais wastaafu na walio madarakani, watanzania tulimpa support gani kuhakikisha watu hawa wanawajibishwa kwa matendo yao? Ni miaka nane sasa tangu makafiri hawa watajwe kwa kuiibia nchi hii, lakini bado wanaendelea kutanua na kula kuku kwa mrija. Chini ya jua hakuna kinachoshindikana. Watanzania tuungane kupambana na watu hawa. Daima umoja ni nguvu.
 
Tatizo slaa haaminiki...hata aseme nini ni km analopoka tu ndio maana watu hata hawamuulizi udhibitisho wake ni upi?!usitoe majina tu toa vidhibitisho tupembembue mchele na pumba wenyewe!!tunajua zito hana maneno tupu siku akitaja tu kila mtu atataka vidhibitisho kwakuwa sio mlopokaji tu!!kama hana hawezi taja cz hajui kulopoka tu!!hicho tu ndio kinamfanya mwanasiasa machachari na kijana!!
 
Zitto amesema atataja majina ya watu wenye akaunti Uswis, sasa ajenda ya pale Ufipa leo ni kutafuta kila linalowezekana kuonesha kuwa hata babu yao aliwahi kuwika hapo zamani.

Zitto alisema kutaja mafisadi ni old fassion imekuwaje na yeye anataja sasa, tukisema katengenezewa list kwa madhumuni flani mtasema anasingiziwa? Huyu jamaa haaminiki kwa chochote anachokisema. Ni zaidi ya kigeugeu.
 

List itabaki kuwa sahihi, hebu anza kufanya analysisi ya hayo majina kwa uchache naanza hivi.. Daudi Balali alikubwa na kashfa ya EPA na baadae akafa kifo cha utata (Kifo cha Kuficha ufisadi), Gray Mgonja, alikuwa ana kesi ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi ambayo anaendelea nayo sambamba na Basil Mramba, Lowassa alikutwa na kashfa ya Richmond ambayo iligarimu uwaziri mkuu wake, Naziri Karamagi, Kashfa ya Richmond na TICS ambayo iligharimu uwaziri wake, Andrew Chenge baada alikubwa na kashfa ya RADAR (Vijisenti), Nimbrod Mkono anatuhumiwa kwa kufanya kazi na Tanesco kupitia kampuni yake ya Mkono advocates ambayo imekwapua mabilioni ya Shilingi kutoka tanesco.. Rostam Aziz, Kagoda saga, Richmond na Dawans all together.. ESCROW hadi ikulu ilitajwa.. sasa Uongo wa Dr. Slaa uko wapi. Watanzania tunamwamini Dr. Slaa kwasabau aliyosema yote yamekuja kuthibitika wazi wazi hiyo list of shame ndio inayoitesa nchi hadi sasa. Long Live Dr. Slaa.
 

Sema mimi namuamini slaa!sio watanzania!ushahidi kaka maneno mengi ya nini!!pia utambue viongoz wako hasa slaa kama anaushahid anaruhusiwa kuupeleka mahakaman na hivyo akawa ametusaidia!mahakama tu ndio inahaki ya kusema km wanatuhuma za kujibu au la...!!akibaki anasema haitusaidii!!
 
Amesema mjitokeze adharani sio mfanye majungu na kuchafuriana jina kwenye media
 
kweli nyani haoni kundule, kabla haujatoa kibanzi kwenye jicho la mwenzio toa kwanza boriti kwenye jicho lako, ukimnyooshea mwenzio kidole kimoja kumbuka kuna vidole vinne vinakunyooshea wewe.
 

mahakama ipi unayoelekeza apeleke kesi hizo? uliwahi mshudia tumbili akihukumu kesi ya nyani kula mahindi ya binadamu?
 
Aliyedharirishwa aende mahakamani ushahidi utaletwa
 
Slaa ni mwehu alikuwa hana ushahidi wa alichokisema
 
Wengine humu siyo wazima sema wamepata uwanja waache waongee.
Maana kazi ipo tz kufikia maendeleo maana vijana bado tunapenda siasa za kishabiki kuliko kujadili ya mazuli na mapungufu na tunapokosea ili tupate kiongozi sahihi.
Tunakuwa wanyonge nje ya tz kwa kuwa hatunatunacho jivunia!
Na niufahari kwa mtz kuwa nje ya nchi au kufanya kazi nje hata kama niya kishenzi!
Nashauri tupeane elimu ktk usahihi na siyo vinginevyo ,tuwe kizazi kingine cha kuibadilisha nchi yetu
 
Unafikiri wewe buku 7 ungecoment nini zaidi ya hiki?.

usikimbilie kumkashifu mtu kwa kuwa tofauti na ukipendacho au ukiwazacho.. tunakushangaa kwa kumuita Dk Slaa shujaa kwa kuwataja akina MANJI kuwa mafisadi pale mwembe yanga kama ushujaa ndio huo mbona tanzania sasa wapo mashujaa wengi tu tena kuzidi yeye,, kuna mtu hapo juu kakwambia basi hata LYATONGA NAYE atakuwa shujaa,, kama ni hivyo basi hata Mwakyembe naye ni shujaa, akina ZZK nao tuwaite mashujaa sasa,,, tambwe hiza naye atakuwa shujaa sasa.. ISSA PONDA naye ni shujaa sasa....MENGI naye tumtaje kama shujaa sasa maana naye amewataja sana hao kabla hata ya DK SLAA...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…