List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Nimecheka sana mkuu siasa hizi.

Ninachojadili kama mada niliyoleta ni kwamba Lowasa hakuwamo katika list ile ya Mwembeyanga.

Pia Lowasa alipojiuzuru uwaziri Mkuu Viongozi wa chadema walishawahi kusema katika moja ya mikutano yao wapo tayari kumsafisha Lowasa kwa tuhuma za Richmond angegeukia kwao, unakumbuka hilo? Kama walimweka katika list ile wangemsafishaje yakhe?
 
Duh!fedha inaweza kununua uhai!

Mada hii inahusu list iliyotangazwa Mwembeyanga na Dr Slaa na kwamba Lowasa hakuwamo, hilo la pesa kununua uhai tuanzishie mada nyigine na dondoo zake tuijadili kwa mapana na marefu.
 
Duuuh hii ni noma kweli kweli hadi JF wamechakachua hii List o Shame Mzee Mwanakijiji hebu njoo bhana hapa utueleshe ni kweli Lowasa hakuwemo kwenye ile Orodha ya aibu ya mafisadi?
 
Last edited by a moderator:
NIMECHEKA KWELI KWELI..... WANA EDIT KULITOA JINA LA MHESHIMIWA KUTOKA KWENYE LIST.....:teeth:
 
Kwenye thread hii list ipo wazi labda wameedit first post na kuacha posts nyingine.EL yumo

kwenye maelezo kwa nini kila mmoja ni fisadi umeliona jina lake na maelezo????? mfano tuone kwa MGONJA, kuna jina na maelezo.....

4. GRAY S. MGONJA

Bwana Gray Mgonja ni Katibu Mkuu wa siku nyingi wa Wizara ya Fedha. Vile vile ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania na anashikilia nafasi ya ukurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited ambayo maelezo yake tumeyatoa kuhusiana na ufisadi unaomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Kwa kuzingatia nafasi yake kama Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Mkurugenzi katika Benki Kuu na vile vile Mkurugenzi katika Tangold Ltd. iliyolipwa mabilioni ya fedha za umma katika mazingira yenye utata mkubwa, ni wazi kwamba kumekuwepo mgongano mkubwa wa kimaslahi unaomhusu Bwana Mgonja.
 
Sirihusu computer yangu video vizivyohakikiwa virus free, sitaki kuchafua processing system ya computer yangu.

Haya hebu basi huyu Afisa habari tumaini makene kwenye hili andiko lake

jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/351...ya-tanzania-tuko-hatarini-3.html#post13381674
 
Mkuu njaa mbaya sana orodha ya mafisadi waliotajwa Mwembe Yanga na Dr.Slaa walikuwa 11 mtafute mmoja umuweke kwenye orodha yako mimi ninalo gazeti la MWANA HALISI.

Teh teh teh
 
Sawa lowassa sio fisadi hata CCM wanajua hilo. Swali ni hili, je utendaji wake unafanana na tingatinga?
 
Mkuu njaa mbaya sana orodha ya mafisadi waliotajwa Mwembe Yanga na Dr.Slaa walikuwa 11 mtafute mmoja umuweke kwenye orodha yako mimi ninalo gazeti la MWANA HALISI.

Teh teh teh
Mkuu,
Mwambie aende hapa,
 
Angalia hapo juu nimeleta orodha ambayo Mzee Mwanakijiji aliweka mada mara baada ya mkutano mkubwa pale Mwembeyanga. Sidhani kama saver ya JF ina nafasi ya kuchakachuliwa.
Nenda hapa kwenye post ya 774,
 
Nenda hapa kwenye post ya 774,

Tatizo la vyombo vya habari Tanzania ni kuandika visivyofanana kwa kile kile kilichonukuliwa na wote. Orodha niliyoleta mimi ni ile ambayo nimeitohoa toka mada iliyoletwa na Mzee Mwanakijiji na nimeichukua kama ilivyotundikwa hapa JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…