List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Nadhani Kilitime, unarudi palepale, unachojaribu kukisema ndicho tujaribu kukijadili. Slaa ameleta kwetu, na kuleta kwetu kuna maana ya kuomba mob shirikishi. kwa maana nyingine anategemea wananchi watamuunga mkono vipi katika vita hii. sasa kama watu watasema wapelekwe mahakamani kwa sababu ushahidi upo, then humu kuna Wanasheria na wasomi mbali mbali wanaweza kutusaidia kwa hilo. Slaa anahitaji maoni ya wengi ili akishinda iwe ni ushindi wa wananchi na si wa Slaa na Kabwe peke yake.
But bado napinga suala hili kuliita la udaku.
 
Waliowasikia wanasema Waliotajwa ni Balali, andrew chenge, basil mramba, meghji,mgonja, rutabanzibwa, mkono,lowassa, karamagi,rostam,mkapa na mkewe na jk.

na wengine wadogo wadogo walikuwa wakitajwa mara kwa mara. Hakuna gazeti ambalo limeandika hayo majina. To me huko ni kuchafuana tu. Uzushi mtupu!!!!

Kwa mzembe wa kutafakari kama wewe,hata majina yangetajwa kwenye magazeti bado unge-conclude kuwa yaliyoasemwa ni uzushi mtupu.Yaani unachotaka kutueleza ni kwamba ukiambiwa na rafiki yako kuwa ndugu yako amefariki (siombei hilo) then isiandikwe kwenye gazeti,then taarifa hiyo ni ya uzushi?Mtu yeyote mwenye akili ambayo haijaathirika anaweza kuelewa logic ya magazeti yote kuogopa kutaja majina.They definitely know nini kitakachofanywa na walitajwa na Slaa,na (japo sidhani kama wamewatendea haki wasomaji wao) I can understand why they avoided naming names.
 
Nadhani Kilitime, unarudi palepale, unachojaribu kukisema ndicho tujaribu kukijadili. Slaa ameleta kwetu, na kuleta kwetu kuna maana ya kuomba mob shirikishi. kwa maana nyingine anategemea wananchi watamuunga mkono vipi katika vita hii. sasa kama watu watasema wapelekwe mahakamani kwa sababu ushahidi upo, then humu kuna Wanasheria na wasomi mbali mbali wanaweza kutusaidia kwa hilo. Slaa anahitaji maoni ya wengi ili akishinda iwe ni ushindi wa wananchi na si wa Slaa na Kabwe peke yake.
But bado napinga suala hili kuliita la udaku.

Binafsi Narudia kusema hatua ya Dr. Slaa ni ile ile ya miaka 47, tunaomba kama anaushahidi ambao wananchi hawawezi jua zaidi ya yeye mwenye makabrasha yote apeleke mahakamani zaidi ya hapo... yeye ndiye anatufanya tumheshimu kwamba afanya jambo jipya kumbe hakuna ni katika kutudanganya sisi watanzania tusiosoma ambao sisi tunadanganywa kirahisi....
 
Binafsi naamini mh. aliowataja hao waheshimiwa wenzake ana access na wanasheria wa nchi yetu... na anajua wahalifu wanapelekwa wapi! sio Temeke Mwembe Yanga!

Tunaomba kama tuhuma hizi ziko wazi tunaomba awasaidie vyombo/mhimili wa tatu (judiciary) ufanye kazi yake!!! kufanya kwa namna hii aliyofanya ni kukwepa majukumu... siku hizi hili ni kama kamziki au noisy ndogo kwa wala rushwa na baada ya muda wanaendelea, sheria ifuate mkondo wake, then itaoneka kuna useriouseness.. na tutaona Dr. Slaa ni Zaidi ya Mrema,,, nisingependa Dr. Slaa nimlinganishe na Mrema tafadhali

Narudia tena, mbona Mtikila ameihenyesha serikali na kushinda kesi nyingi,,, kwa nini hawa waheshimiwa wasifanye hivyo kwa uzalendo tu! ili kuisaidia nchi yetu!!! wahalifu wanapelekwa mahakamani...

Wahalifu/watuhumiwa wengine hawapelekwi Temeke mwembe yanga kwa nini hawa wa rushwa tena kubwa wapelekwe huko!!! wakati access ya wanasheria ipo, watu makini wapo, chama makini kipo?

Kilitime,
Kuwapeleka mahakamani tu haitoshi, ni kuwashitaki pia kwa wananchi ili wawajue wanaowahujumu na kuwasababishia kero za miaka nenda rudi,

Hao waheshimiwa wanaokula rushwa walipata hizo nafasi zilizowapa uwezo wa kula rushwa kubwa kubwa baada ya kuomba kura za wananchi katika viwanja kama hivyo vya mwembe yanga, nyarugusu, jangwani, manzese, mwanza mabatini, n.k, hao mawaziri wanaotuhumiwa hawakupata uwaziri kupitia mahakamani ,kwanza walikuwa wabunge na kisha ndo wakawa mawaziri, kwa hiyo wananchi waliowachagua hawana budi kuelezwa waheshimiwa hao wanachokifanya (kula rushwa).

wanchi wakishawajua huishii hapo ni kuvipa changamoto vyombo vya sheria kama TAKUKURU ,polisi,usalama wa taifa kuwachunguza watu hao na kuwafikisha katika mkono wa sheria

KUMBUKA RUSHWA NI KOSA LA JINAI, SIYO WAPINZANI WENYE KUSHITAKI, NI JAMHURI NDIYO YENYE KUSHITAKI,
JE NIKUULIZE BWANA KILITIME JE SERIKALI(JAMHURI) INA UBAVU WA KUWACHUNGUZA NA KUWASHITAKI HAO WATUHUMIWA WAKIWEMO MAWAZIRI WAKE?
 
Binafsi Narudia kusema hatua ya Dr. Slaa ni ile ile ya miaka 47, tunaomba kama anaushahidi ambao wananchi hawawezi jua zaidi ya yeye mwenye makabrasha yote apeleke mahakamani zaidi ya hapo... yeye ndiye anatufanya tumheshimu kwamba afanya jambo jipya kumbe hakuna ni katika kutudanganya sisi watanzania tusiosoma ambao sisi tunadanganywa kirahisi....

Unatumia saana wingi kwenye hii post.... unawakilisha kina nani? mbona ni wewe peke yako ndio unasubiri kuona Kikwete na Karamagi wakionyeshwa na TVT, au ITV kwenye TV wakipokea rushwa?
 
Unatumia saana wingi kwenye hii post.... unawakilisha kina nani? mbona ni wewe peke yako ndio unasubiri kuona Kikwete na Karamagi wakionyeshwa na TVT, au ITV kwenye TV wakipokea rushwa?

Mwafrika wa kike

Your post has been ignored by kilitime!

Thanks
 
Hivi ni mikataba gani yenye utata iliingiwa na serikali ya Tanzania wakati Kikwete akiwa Waziri wa Nishati, Maji, na Madini? Na ni mikataba gani yenye utata ambayo iliingiwa na makampuni ya nje wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje (na kama anahusika kwa namna yoyote kwenye mikataba hiyo).. Na zaidi ya yote kwa muda mfupi aliokuwa Waziri wa Fedha ni mikataba gani iliingiwa akiwa na wadhifa huyo.

Mara nyingi inaonekana Rais Kikwete akizungumzia Mikataba (hasa kwenye hotuba yake ya Kufungua Bunge) alizungumza kana kwamba ni mara ya kwanza kusikia kuna mikataba mibovu na hajawahi kuona mikataba hiyo au kushiriki kwa namna yoyote ile katika uingiaji wake.
 
Je ni sahihi kusema kwamba sera ya chadema na upinzani kwa ujumla ni kutoboa siri za rushwa as a way to get ikulu in 2015?
Jibu ni kwamba SIO SAHIHI.I told you earlier,jaribu kutafakari beyond political interests.Hivi kwa mfano,kwa kuwaumbua majambazi hawa,wapinzani wanafanikiwa kutengeneza mazingira ya kuingia Ikulu,and at the same time tunafanikiwa kukomesha wizi huu wa mchana mchana.Wouldnt that be good for you,Mtanzania uliyeleweshwa na uonevu?
Kina kitine, warioba, mrema, mengi, mtikila mbona walishafanya haya na wamewasaidia nini maskini wa tanzania in the process?
Pengine ungekuwa umewahi kusoma historia za mapambano dhid ya udhalimu ungeweza kufahamu kuwa process ya namna hiyo ni ngumu na ndefu.Waliyosema akina Kitine,Mengi,Warioba,etc hayawezi kuwa na faida kwa watu wenye imani haba kama wewe ambao pamoja na kunyonywa,kudhulumiwa,kuteswa na kunyanyaswa bado mnaamini kuwa kuna njia mbadala ya kuwaumbua wanaotuumiza badala ya kuwataja hadharani kama walivyofanya akina Slaa
kwa watu wenye upeo mdogo wa kuelewa mambo watajibu kwamba kuna system fulani imewazuia. Slaa atathubutu vipi kusema nilizibwa mdomo? Unazibwa mdomo kama unapayuka, lakini kama una operate in the context of sera na unajenga hoja ju ya hoja na kuja tolea mifano ya rushwa kama by the way tu, hutazibwa mdomo sababu hawatakuwa na jinsi.
Na kwa wenye upeo dogo kama wewe sio rahisi kujua au kukubali kwamba kuna "nguvu za giza" (vyombo vya dola) vinavyohakikisha kuwa kila anayetamka kwamba kiongozi flani mwizi,au mbadhirifu,basi anadhibitwa haraka iwezekanavyo.Sijui ulikuwa na umri gani wakati yanamfika yalomfika Sokoine,au Stan Katabalo,au Kolimba....pengine tatizo lako sio upeo mdogo bali udogo wa uwezo wa upeo wako
Siasa za slaa na kabwe ni siasa za kitoto za kuchongea ccm kwa wananchi
. Hebu tupe darasa kidogo.Siasa za kikubwa ni kuchongea wapi?Mkapa achongewe kwa mkewe?Lowassa achongewe kwa Kikwete?Karamagi achongewe kwa Rostam Aziz?Come on,man.You need to come up with at least a grown-up assessment
They need to grow up kisiasa na kuja na mbinu ambayo hayo masuala ya rushwa yataingizwa kwenye something more comprehensive. Sio kuwaadaa tu wananchi huko mikoani na udaku.
Nyani haoni kundule.You are the one who critically needs to grow up,and see what's actually happening in the real world and not in your fantasies.Hakuna anayekuhadaa bali unajihadaa mwenyewe kwa kudhani kuwa wanachoongea wazalendo hawa ni hadaa ilhali u mmoja wa mamilioni ya walalachali wanaokandamizwa kila kukicha pasipo dalili ya wakandamizaji hao kupatwa na huruma.Sikulaumu sana kwani natambua kuwa katika jamii kuna wale ambao kwao pain is pleasure.
 
Hivi ni mikataba gani yenye utata iliingiwa na serikali ya Tanzania wakati Kikwete akiwa Waziri wa Nishati, Maji, na Madini? Na ni mikataba gani yenye utata ambayo iliingiwa na makampuni ya nje wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje (na kama anahusika kwa namna yoyote kwenye mikataba hiyo).. Na zaidi ya yote kwa muda mfupi aliokuwa Waziri wa Fedha ni mikataba gani iliingiwa akiwa na wadhifa huyo.

Mwanakijiji,nilidhani baadhi ya majibu ya maswali hayo tuliyasikia kwenye mahojiano yako na Dr Slaa!!!Au nimekosea?
 
Mwanakijiji,nilidhani baadhi ya majibu ya maswali hayo tuliyasikia kwenye mahojiano yako na Dr Slaa!!!Au nimekosea?

You are right, hapa ndipo watu makini wange-concentrate napo, kuchambua tuhuma moja baada ya nyingine!
 
Corrupt leaders will always remain in the darkness of corruption until Those who oppose this darkness expose them to light,

Corrupt leaders will always jeorpadize our prosperity,
Untill those who are brave enough tell them to Stop!

Corrupt leaders will always suffocate the voice of justice,
Until those who want justice stand up firm and resist

Corrupt leaders will continue to dwell in hipocricy
Until those who want truth unfold say no to them

bad of all corrupt leaders will sell our freedom and dignity
and thus make us slaves economically,politically even socially

CORRUPT LEADERS ARE ENEMIES OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
 
Ndgu MKJJ,Nimekuwa nashangaa sana na Kauli za Mkwere JK (Sio Muungwana tena),Kwamba hausiki na Mikataba ya Madini,Nilikwishawahi kuandika huko awali kwamba,tukiichunguza Mikataba yote hapo Wizarani(Madini/Nishati),tutamshika Shati Mkwere,kwani nina uhakika aliwahi kuhusika na Mikataba yenye Utata alipokuwa Waziri.Kwa kumbukumbu zangu alihusika kabisa na utiaji sahihi wa Mkataba wa Madini August/1994.

Kampuni iliyohusika na Mkataba huo inaitwa Samax Limited ambayo ilipewa eneo la machimbo huko Nzega (Rejea mazungumzo ya Dr.Wilbroad Slaa) Pia alitia saini Mkataba mwingine wenye Utata mwaka 1996.Kampuni iliyohusika na Mkataba huo ni Kahama Minning na kupewa maeneo ya Geita na Bulyankulu.

Suala la Bulyankulu lilikuwa zito na ndilo lilitufanya baadhi ya watu kuondoka Tanzania na kuacha ajira zetu kwa Umma,kwa sababu tu ilionekana wawekezaji ni muhimu kuliko Uhai wa watu!!.Ili kupata maelezo ya kina kuhusu issue nzima ya Bulyankulu Zungumza na Rais wa Chama cha wanasheria wa Mazingira.

Sina uhakika na Wizara nyingine alizopita Mkwere na mikataba ya huko.Lakini pia alihusika ktk ule Mkataba wa RADA alipokuwa Foreign.Kwa maana hiyo michezo hiyo anaijua vyema!!
 
Mwanakijiji,
Hivi hujawahi kujiuliza ni kwa nini katika kila safari yake Marekani Mwungana lazima akutane na Sinclair? Na ni kwa nini kila mara Sinclair anapokwenda Tanzania lazima akutane na Mwungwana? Nasikia mkutano wa mwisho walikuwa watatu peke yao, pamoja na Joseph Kahama. Wanazungumzia nini?
 
Wanazungumza jinsi ya kumkatia JK shares na kuendelea kushibisha matumbo yao kwa mgongo wa walipa kodi wa bongo.
 
Waliowasikia wanasema Waliotajwa ni Balali, andrew chenge, basil mramba, meghji,mgonja, rutabanzibwa, mkono,lowassa, karamagi,rostam,mkapa na mkewe na jk.

na wengine wadogo wadogo walikuwa wakitajwa mara kwa mara. Hakuna gazeti ambalo limeandika hayo majina. To me huko ni kuchafuana tu. Uzushi mtupu!!!!

1. Rais Jakaya Kikwete

2. Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

3. Waziri Mkuu Edward Lowassa

4. Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi

5. Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge

6. Waziri wa Viwanda na Biashara Basil Mramba

7. Gavana wa Benki Kuu (BoT) Daudi Balali;

8. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Gray Mgonja

9. Katibu Mkuu Wizara ya Maji Patrick Rutabanzibwa

10. Mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono

11. Mbunge wa Igunga Rostam Aziz

Una ushahidi kwamba huo ni uzushi tu? Waswahili walisema kitu usichojua ni kama usiku wa kiza.
 
Nafikiri mchambuzi asome mawazo ya wengine pia badala la kujaza kurasa suala la sera katika nchi ya tanzania ni ndoto. Hata hao CCM wanaosema sera hata sera zao hawazijui.
 
Huyo anayetaka sera,asisahau kuwa Mrema na Slaa ni wapinzani(wanasiasa) lakini zaidi ni Watanzania. Sasa kama wameamua kutaja majina hayo kama Watanzania sijui bado atataka wawe na sera? Nauliza tu!!
 
Nafikiri mchambuzi asome mawazo ya wengine pia badala la kujaza kurasa suala la sera katika nchi ya tanzania ni ndoto. Hata hao CCM wanaosema sera hata sera zao hawazijui.

Suala la sera tanzania sio ndoto but reality. sera za serikali zipo. Sio sahihi kusema hazipo. Cha kusema ni kwamba hazitekelezwi na pia hazirekebishwi kukidhi mahitaji ya maskini. Othewise nchi gani inaweza endeshwa bila sera. Reason on why hazitekelezwi ni kwamba tupo too much dependent on misaada ya nje to fund our budget.

Na hawa wanaotupa misaada ndio wanatupangia nini tufanye na tutumie fedha wapi. Na ni hao hao wahisani ndio wanakula na wezi hapa nyumbani.

Hata akiingia mpinzani kushika nchi, sina uhakika sana kama much can be done to change that. Sioni leaders wenye vision ya tanzania inayojitegemea zaidi kuliko kutegemea nje na hivyo kuwa kama kasha tu. Uwezo wa kuchange hiyo equation upo but no one cares much zaidi ya kula because hela za misaada ni rahisi sana kula kuliko hela za kutengeneza wenyewe ndani ya nchi.
 
Back
Top Bottom