List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Pengine wengine hawafahamu maana ya ufisadi na pia hatuhusianishi kati ya ufisadi na maadili ya uongozi wa umma.

Tatizo ni kwamba Watanzania wengi hawajui uhusiano uliopo kati ya Serikali au watumishi wake kutumia pesa vibaya na maisha yao ya kila siku. Ni wachache mno wanaojua mchango wao katika uendeshaji wa serikali, ukimwambia msukuma wa Bariadi kuwa Chenge ni fisadi haoni kuwa hilo ni tatizo lake. Hajui ni namna gani pesa alizoiba Chenge zinamhusu , yeye anajua hiyo ni mali ya serikali, na serikali kwake ni serikali, na haina uhusiano wowote na maisha yake tofauti na misaada ya kujengewa visima, shule, zahanati, n.k
Wao wanajua kama Halmashauri ya wilaya ikijenga barabara au zahanati kuwa ni huruma ya serikali au mbunge wao, hawajui kuwa hiyo ni haki yao.
Hawajui ni namna gani wao wanachangia uendeshaji wa serikali kupitia manunuzi na matumizi yao ya kila siku. Siku wakijua ni mchango gani wanatoa katika uendeshaji wa serikali, siku hiyo tutaanza kuona maandamano pale huduma za jamii zinapopanda, ni siku hiyo ndipo Tanzania yangu itapata uhuru wa kweli.

Bila wananchi kuoanisha maisha yao ya kila siku na mapato na matumizi ya serikali CCM wataendelea kuwalaghai na mafisadi yataendelea kushika ofisi za umma.

Natamani siku hiyo ianze 31 October 2010
 
Ndo maana wanajitahidi asifike IKULU maanake patachimbika..
Saa ya ukombozi itaanza baada ya 31-10...
 
Raisi wetu Kipenzi aliyeingia IKULU kwa baraka za wananchi za asilimia 80 leo hii anatumwagia changa la macho,hana adabu na heshima hata kidogo ametushusha hadhi na kutokesesha wasihi wa kiutu kwa kutuvua nguo barabarani huku akigeuza IKULU mahari pa marafiki,,adhabu yake ya kututelekeza kuwachangamkia mafisadi yaliyokubuhu ataiona mnamo mwaka huu si mbali ni tarehe 31/10/2010
NGUVU YA UMMA itatembea
 
Wadau kwaheshima na taadhima ningependa kuwaomba wapiganaji wenzangu "list of shame iliyotolewa na DR.slaa pale mwembeyanga.

Kwakweli nimesearch kwa njia zote mpaka huku JF nimepekua till post za 2007 na sijaweza kupata.

Tusaidiane ilituweze sote kutunza kumbukumbu kwa ufasaha.

Natanguliza shukran zangu za dhati.

Wenu mpiganaji,
Mashingo.
 
1. Jakaya Mrisho Kikwete
2. Rostam Aziz
3. Edward Lowassa
4. Jitu Patel
5. Daud Balali
6. Nimrod Mkono
7. Tanil Somaiya
8. Lundar Chadwa
9.
10.
11.
Malizieni...................
 
Mchungaji hanajipya zaidi ya hizo list za kubuni, amekwisha kisiasa, sera zake zimeshastukiwa. akae pemebeni, kamaanaweza alete demcrasia ndani ya chama chake cha chadema
 
Wadau kwaheshima na taadhima ningependa kuwaomba wapiganaji wenzangu "list of shame iliyotolewa na DR.slaa pale mwembeyanga.

Kwakweli nimesearch kwa njia zote mpaka huku JF nimepekua till post za 2007 na sijaweza kupata.

Tusaidiane ilituweze sote kutunza kumbukumbu kwa ufasaha.

Natanguliza shukran zangu za dhati.

Wenu mpiganaji,
Mashingo.

Hii hapa unaweza angalia hapa na kupata kila kitu :

Orodha ya Mafisadi (List of Shame)
 
waje na majina na ushaidi pia ili tuweze kuamini na waweze kuchukuliwa hatua za kisheria , vinginevyo itakuwa ni upupu tu na uchonganishi.
 
mimi sioni kama A. L. Mrema ni mtu serious katika masuala yamsingi, amekuwa pro-ccm sana. nakumbuka hutuba aliyotoa pale kwenye ukumbi wa kizota dodoma wakati amekaribishwa na ccm, binafsi niliona thinking yake imerudi nyuma, hivyo sitegemei kuona anatoa challenge ya maana kwa serikali
 
lOWASA HAYUMO TENA, AMAEONDOLEWA NA KANISA KATOLIKI . HUMUONI SASA ANATOA MAPESA YA DOWNS HUKO?
 
Badala ya kutafuta jinsi ya kujikomboa kiuchumi we endelea kutafuta majungu ambayo hayakusaidii chochote we na familia yako .
 
Usibweteke kimawazo beko, hiyo list of shame wewe haikusaidii chochote katika maisha yako. Umizi kichwa ni jinsi gani utamudu maisha yako, achana na wanasiasa.
 
Back
Top Bottom