balibabambonahi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 15,771
- 14,294
Dk slaa ndo shujaa na rais Wa mioyo ya watanzania,mtez Dume mwiz tu hata hatukumchagua
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
acha ujinga,mtu anatoa majina ya watu wanaohujumu uchumi serikali inakaa kimya!Ilipaswa chombo husika kama PCCB wamfuate kupata vielelezo na ushahidi juu ya watu wale!Sema kwasababu ni vigogo wa serikali ndio maana hatuoni ufuatiliaji!
Ulishawahi ona wapi nchi inafanya manunuzi ya mabilioni halafu baadaye mabilioni kadhaa yanarudishwa eti ni chenji iliyobaki!
Nchi hii ina mengi!
Hapa unahitaji dr slaa apeleke ushahidi mahakamani?
Unakaa unashabikia ujinga na kuleta maneno ya kanga kwenye mambo nyeti,China wahujumu uchumi wananyongwa,hapa tz ndio wanaonekana madon na wajanja!
Slaa kama ana ushahidi mbona hakwenda mahakamani kushtaki? Porojo tu
Kwa nini mkuu?
Zitto ni shujaa kitambo,ameshawahi fukuzwa bungeni wakati amemvaa Kalamagi,pale ndipo ushujaa wa Zitto ulipoanza kujidhirisha,hata chama Chake kuendelea kukubalika zaidi katikati ya hila za Chadema za kuitisha mkutano kila ACT wanapoitisha nao ni ushujaa wa kiwango kilichopindukua
Katika wote hapo umemuona LOWASSA tuu?lowasa ni fisadi angali akiwa tumboni.Huyu mamvi ana haya kabisa ni mwizi mkubwa sana.Ndio maana magonjwa yana mtafuna.El ni jambazi sugu
hadi leo hawajaenda mahakamani.Waliotajwa waende mahakani Dr. Slaa alishatimiza wajibu wake, mafisadi tumeshawajua na hatuwezi kuwapa dhamana ya nchi tena.
Naomba niwakumbushe tu orodha ya mafisadi kama ilivyoorodheshwa na Dr. Slaa katika mkutano uliofanyika Mwembe Yanga, Temeke tarehe 15 Septemba, 2007.
1. Dr. Daudi T.S. Balali - sasa marehemu ?
2. Andrew J. Chenge - mgombea Ubunge kupitia CCM, Bariadi.
3. Basil P. Mramba - mgombea ubunge kupitia CCM, Rombo.
4. Gray S. Mgonja - Kaibu Mkuu mstaafu, Hazina.
5. Patrick P. R. Rutabanzibwa - Katibu Mkuu mstaafu ?
6. Nazir Karamagi - Waziri mstaafu.
7. Nimrod Mkono - mgombea ubunge kupitia CCM, Musoma vijijini
8. Rostamu Azizi - mgombea ubunge kupitia CCM, Igunga.
9. Edward Lowassa - mgombea ubunge kupitia CCM, Monduli.
10. Benjamin W. Mkapa - Raisi mstaafu, CCM.
11. Jakaya Mrisho Kikwete - mgombea Uraisi kupitia CCM
Kikwete kwa sasa ndiye mlinzi wao mkubwa na CCM ndiko waliko salama na wanakohifadhiwa - Kazi kwetu wananchi tarehe 31 October, 2010.
Tunamdai pesa za kanisa alizoondoka nazo enzi za utumishi wake wa upadri.Mbona hatumuoni kwenye list?
Leo Lowasa chadema watamsafishaje endapo atamua kujiunga chadema. sasa naanza kuamini maneno ya kibajaji kwamba kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu au adui wa kudumu
mkuu mm napenda sana lowasa ajiunge na chadema nazani ndio itakuwa vizuri zaidi maana ndio utakuwa mda muafaka wa kuyaweka yote hadharani.
maana sisi tunaamini kuwa yeye ni fisadi lakini yy anadai yy sio fisadi na hajawahi toa maelezo yoyote juu ya shutuma hizo kwa kina.nazani akijiunga na upinzani swala kubwa itakuwa nikujisafisha kuwa yeye sio fisadi na swali kubwa atakalo ulizwa na wananchi litakuwa ni hilo la ufisadi.kama hata wanachama wenzie walikuwa wanatembea na kunpiga vijembe kuwa yeye ni fisadi nazani akijiunga upinzani na kupewa nafasi ya kugombea nafasi ya uongozi najua lazima ccm watakuwa wanampiga madongo tuu kuwa yeye ni fisadi na hapo ndio na yeye atataka kutoboa ukweli halisi.