List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Dk slaa ndo shujaa na rais Wa mioyo ya watanzania,mtez Dume mwiz tu hata hatukumchagua
 
Zito anaujanja wa kitoto sana eti kajichekesha adi muda unaisha anajidai kusema muda wakufuturu eehhhh bora akawe mkulima kwao hana tena jipya!
 
acha ujinga,mtu anatoa majina ya watu wanaohujumu uchumi serikali inakaa kimya!Ilipaswa chombo husika kama PCCB wamfuate kupata vielelezo na ushahidi juu ya watu wale!Sema kwasababu ni vigogo wa serikali ndio maana hatuoni ufuatiliaji!
Ulishawahi ona wapi nchi inafanya manunuzi ya mabilioni halafu baadaye mabilioni kadhaa yanarudishwa eti ni chenji iliyobaki!
Nchi hii ina mengi!
Hapa unahitaji dr slaa apeleke ushahidi mahakamani?
Unakaa unashabikia ujinga na kuleta maneno ya kanga kwenye mambo nyeti,China wahujumu uchumi wananyongwa,hapa tz ndio wanaonekana madon na wajanja!

Dr slaa ni mlopokaji tu kuna watu wengine kwenye hiyo list mbona hawajafikishwa mahakamani
 
Slaa kama ana ushahidi mbona hakwenda mahakamani kushtaki? Porojo tu

We shetwani pungu 2 Dr Slaa ametimiza wajibu wake! Hao waliotajwa ndiyo walipaswa waende mahakamani ili wamuite Slaa akathibitishe, kwanza anayetajwa kuwa marehemu Gavana wa Benki Kuu ya Mafisadi-BoT alituambia kuwa hizo ni kelele za mlango, hazimzuii mwenye nyumba kulala wakati fedha zimeibiwa kule!
 
Kwa nini mkuu?

kaka faraja inaanzia nyumbani angeanza kutuambia ufisadi ndani ya chama chake ndio ataje ayo majina kwa inavyoonekana iyo list yake imetokana na source za kwenye kahawa kwa sababu hajatupatia ushahidi na chanzo cha iyo taarifa ili hatua za kimahakama zifanyike
 
Zitto ni shujaa kitambo,ameshawahi fukuzwa bungeni wakati amemvaa Kalamagi,pale ndipo ushujaa wa Zitto ulipoanza kujidhirisha,hata chama Chake kuendelea kukubalika zaidi katikati ya hila za Chadema za kuitisha mkutano kila ACT wanapoitisha nao ni ushujaa wa kiwango kilichopindukua

Ushujaa wake ukaporomoka aliposhindwa kutaja orodha ya mafisadi walioficha fedha Uswiss kwa kusubiri wahusika wamfuate wamtongoze kama ilivyokuwa kwenye issue ya Buzwagi!? Yule aliyeitwa "mwizi" na "tumbili" alituambia kuwa Zitto amekula kiapo na kudai kuwa hana hiyo orodha ya mafisadi walioficha fedha uswiss, sasa anapokuja na porojo zake hizo kuchafua historia ya Mwembe Yanga-Temeke anatafuta kick ya chama chake cha wasaliti!?
 
Siasa zinajadiliwa kama team kiba na team diamond...is it real Jamii forum in Nyumba ya great thinkers?????....napata shida kubwa kupata vipimo vya kuwalinganisha Dr slaa name zitto kabwe
 
Kuna umuhimu wa kuja na orodha mpya ya watuhumiwa wa ufisadi..

Hii ijumuishe wote waliotuhumiwa na kuendelea kungangania nyadhifa za chama au serikali.

Pia ijumuishe wale walioshutumiwa bila kipelekwa mahakamani.

Ijumuishe pia marafiki na jamaa za mafisadi wanaotumia fedha walizopora kutanua.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Ile ya kwanza bado haijamalizika kufanyiwa kazi wakimali ndo watulete mpya hatutaki kuchanaganyiwa mambo hapa,
 
Leo Lowasa chadema watamsafishaje endapo atamua kujiunga chadema. sasa naanza kuamini maneno ya kibajaji kwamba kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu au adui wa kudumu
 
Naomba niwakumbushe tu orodha ya mafisadi kama ilivyoorodheshwa na Dr. Slaa katika mkutano uliofanyika Mwembe Yanga, Temeke tarehe 15 Septemba, 2007.

1. Dr. Daudi T.S. Balali - sasa marehemu ?
2. Andrew J. Chenge - mgombea Ubunge kupitia CCM, Bariadi.
3. Basil P. Mramba - mgombea ubunge kupitia CCM, Rombo.
4. Gray S. Mgonja - Kaibu Mkuu mstaafu, Hazina.
5. Patrick P. R. Rutabanzibwa - Katibu Mkuu mstaafu ?
6. Nazir Karamagi - Waziri mstaafu.
7. Nimrod Mkono - mgombea ubunge kupitia CCM, Musoma vijijini
8. Rostamu Azizi - mgombea ubunge kupitia CCM, Igunga.
9. Edward Lowassa - mgombea ubunge kupitia CCM, Monduli.
10. Benjamin W. Mkapa - Raisi mstaafu, CCM.
11. Jakaya Mrisho Kikwete - mgombea Uraisi kupitia CCM

Kikwete kwa sasa ndiye mlinzi wao mkubwa na CCM ndiko waliko salama na wanakohifadhiwa - Kazi kwetu wananchi tarehe 31 October, 2010.

Tunamdai pesa za kanisa alizoondoka nazo enzi za utumishi wake wa upadri.Mbona hatumuoni kwenye list?
 
Leo Lowasa chadema watamsafishaje endapo atamua kujiunga chadema. sasa naanza kuamini maneno ya kibajaji kwamba kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu au adui wa kudumu

mkuu mm napenda sana lowasa ajiunge na chadema nazani ndio itakuwa vizuri zaidi maana ndio utakuwa mda muafaka wa kuyaweka yote hadharani.

maana sisi tunaamini kuwa yeye ni fisadi lakini yy anadai yy sio fisadi na hajawahi toa maelezo yoyote juu ya shutuma hizo kwa kina.nazani akijiunga na upinzani swala kubwa itakuwa nikujisafisha kuwa yeye sio fisadi na swali kubwa atakalo ulizwa na wananchi litakuwa ni hilo la ufisadi.kama hata wanachama wenzie walikuwa wanatembea na kunpiga vijembe kuwa yeye ni fisadi nazani akijiunga upinzani na kupewa nafasi ya kugombea nafasi ya uongozi najua lazima ccm watakuwa wanampiga madongo tuu kuwa yeye ni fisadi na hapo ndio na yeye atataka kutoboa ukweli halisi.
 
Hawezi sema ukweli ataishia kusema zilikuwa chuki za kisiasa basi,,,,fisadi ni fisadi tu.
 
mkuu mm napenda sana lowasa ajiunge na chadema nazani ndio itakuwa vizuri zaidi maana ndio utakuwa mda muafaka wa kuyaweka yote hadharani.

maana sisi tunaamini kuwa yeye ni fisadi lakini yy anadai yy sio fisadi na hajawahi toa maelezo yoyote juu ya shutuma hizo kwa kina.nazani akijiunga na upinzani swala kubwa itakuwa nikujisafisha kuwa yeye sio fisadi na swali kubwa atakalo ulizwa na wananchi litakuwa ni hilo la ufisadi.kama hata wanachama wenzie walikuwa wanatembea na kunpiga vijembe kuwa yeye ni fisadi nazani akijiunga upinzani na kupewa nafasi ya kugombea nafasi ya uongozi najua lazima ccm watakuwa wanampiga madongo tuu kuwa yeye ni fisadi na hapo ndio na yeye atataka kutoboa ukweli halisi.

na hz tabia chafu za kugawa hela si za kifisadi?
 
Back
Top Bottom