Habari za muda huu wakuu.
Ningeomba kupata kujuzwa juu ya madai aliyoyatoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Dr. Willibrod Peter Slaa na kupelekea kuweka hadharani madai hayo kwa kutengeneza Orodha iliyojulikana kama
LIST OF SHAME.
Katika Orodha hiyo aliwataja viongozi wengi ambao wamo ndani ya Chama cha Mapinduzi kutokana na madai ya UFISADI na viongozi hao wengi wao bado wamo ndani ya Chama cha Mapinduzi mpaka hivi sasa.
Dr.W.Slaa. Ulisema hiyo list unayo na hao watu unawafaham kabisa kwa majina, haiyumkiniki kuacha kuwataja watu hao inapelekea kutuaminisha kuwa nini lilikuwa lengo lako ?.
Tulikuamini sana, sasa iko wapi IMANI yako juu raia wapenda HAKI NA MAENDELEO ?. Uko wapi UAMINIFU WAKO hii leo ?. Tutaendelea kukuamini tu kama utaweza kutuwekea bayana/hadharani majina ya watu hao ambao kwa NDIMI YAKO uliwaita kuwa ni MAFISADI, je nawe unawakumbatia ama ni vipi ?. Tuamini nini kwa kile tulichokiamini toka kwako tangu mwanzo ?. Mtu asemapo jambo kisha akashindwa kulidhihirisha kwa jina jepesi ataitwa ni MUONGO, sitaki kutumia jina hili kwako kwa,sababu litakuwa ni tusi kubwa kuliko hata kama ningekutukana bayana nikiamini wazi kuwa bado una muda na nafasi ya kututajia LIST hiyo.
Kwa kuwa ni mwanachama HAI wa
JamiiForums ningependa niambatanishe nakala mojawapo kwako kama mada isemavyo...
NASHKURU SANA.
Cc
Dr.W.Slaa