List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Mchambuzi ni lazima utambue kwamba ili kupambana na rushwa ni lazima upambane na wala rushwa/watoa rushwa,haiwezekani kupambana na rushwa kutoka hewani pasipo kuwa na target.

kuwataja wala rushwa ni mbinu ya kwanza ,kwa sababu wala rushwa wapo na baadhi yao wanajulikana.Sera ni nini? ni mipango ambayo mara nyingi ipo katika Maandishi tu!,Na kama hizi sera hazitekelezwi matokeo yake ni nini? always yatabaki ni maandishi tu! na hakuna result yoyote ya msingi itakayopatikana,

Sasa bwana Mchambuzi inaelekea wewe ungependa sana wapinzani wawe na Sera nyingi nzuri nzuri kwamba tutafanya hiki na kile,n.k,lakini hutaki kukubali kwamba wapinzani bado wana kazi ya ziada zaidi ya kuwa na sera hizo,Kazi yao nyingine ni kuwakosoa watawala kwa yale ambayo yanakwenda kinyume na maslahi ya taifa kiujumla. inapotokea wapinzano wakawajua Wala Rushwa kwa nini wasiyaanike majina yao wazi jamii ikawafahamu, au unataka wakashitaki mahakamani kwanza,au TAKUKURU ndo utaridhika kwamba kweli wapinzani wanafanya kilicho sahihi?.

wala rushwa kama wanajulikana hawana budi kuwa "exposed" na ikibidi kuzomewa na pia kuchukuliwa hatua kali za kisheria ,hao watu wanawatia mamilioni ya watu katika mateso makuu kwa sababu ya ubinafsi uliokithiri ,hii mbinu ya Mrema na Slaa safi sana
 
Inaelekea watu wengi hapa hamumuelewi Mchambuzi. Ukisoma vizuri maandishi yake yana make sense. Kuyapuuza kama mnavyofanya ni kujichimbia kaburi wenyewe.

Ningelikuwa mimi mwanasiasa tena wa upinzani, ningelikuwa namsoma Mchambuzi kwa nguvu zote na kisha kuamua cha kufanya.

Siasa sio rahisi sana kuzicheza ndio maana watu wengi wanashindwa. Siasa sio logics bali ni kuelewa jinsi power, money and politics vinavyocheza pamoja.

Kama ni kweli wamemtaja Muungwana kwamba ni mla rushwa, naamini ni kosa kubwa. Inabidi kucheza divide and rule, hata kama muungwana ana kula rushwa basi kwasasa angewekwa pembeni kwanza ili kumgawa yeye na Lowasa. Hatari hapa ni kwamba kama wananchi wengi hawataamini kwamba Muungwana ni mla rushwa basi hata madai
juu ya hao wengine nayo yatapuuzwa.

Kitu kingine ni hicho cha kukosekana kwa mazungumzo juu ya sera. Kuongelea rushwa ni vizuri lakini kilicho muhimu zaidi ni sera za chama na jinsi ya kumkomboa Mtanzania kutoka kwenye umaskini.
 
Wanabodi,

Mimi sikupata muda wa kusikiliza live, lakini kwenye orodha yenyewe na kwa habari mbalimbali za udaku mbalimbali toka hapa JF na nje ya JF...

HAKUNA JIPYA

Nilishawahi kusema, kumdhania mtu is not any issue at all, kazi kudhibitisha!!! Naamini Dr. Slaa ni mtu makini, sasa yeye kama msomi etc... angefungua kesi mahakamani au kitu kama hicho ili tuone ukweli wa mambo... Mch. Mtikila amefanya hivyo mara nyingi na deliverables zake zilionekana...

Haya ya Dr. Slaa... ni mambo ya baraza tu!!! mbona majina mengi mlikuwa mkiyataja hapa... what so new!!! au kwa vile sasa yametoka kwa Dr. Slaa...

Amkeni,,, mwambieni aende mahakamani, hata akishindwa atakuwa ameonyesha useriousness sio sasa ambao ni udaku tu... No wonder magazeti kama matatu niliosoma hayajaandika hata jina moja, kwa kuwa waliona ni udaku tu kulingana na ethics zao,,, na sio woga kama wengine wanavyodhani....


You have to prove without doubt,,, you can always punch numbers as much as you can... Mzee ES alinizushie nisingesema amedanganya kila mtu angeamini Mzee ES ni mkweli... by the way nilishakusamehe... na-refer tu kidogo kuweka hoja yangu sawa.
 
Hivi Mchambuzi huoni aibu kujidhalilisha namna hiyo,kuwatetea watuhumiwa kabla ya wao wenyewe kusema neno.Hata wao inawezekana wana kigugumizi hawakujua kama watakua kwenye list.Mimi nasubiria reaction za hao mafisadi maanake in real ukifuata logic wote wanaonekana kuhusika kutokana na nyadhifa zao kama Mramba aliyetetea Ndege mbovu na kutoa matusi kwa wananchi,Rada iliyokuwa na kashfa,kikwete na wizara ya nishati na Madini,Balali na benki kuu.......
 
Kama ni kweli wamemtaja Muungwana kwamba ni mla rushwa, naamini ni kosa kubwa. Inabidi kucheza divide and rule, hata kama muungwana ana kula rushwa basi kwasasa angewekwa pembeni kwanza ili kumgawa yeye na Lowasa. Hatari hapa ni kwamba kama wananchi wengi hawataamini kwamba Muungwana ni mla rushwa basi hata madai juu ya hao wengine nayo yatapuuzwa.

Nakuunga mkono kwa hili. Hapa wazee wamechemsha tena mno....

Tanzanianjema
 
Na mimi nakubali kabisa kuwa sera ni kitu muhimu kwa chama cha siasa..... lakini ukweli mwingine ni kuwa sera haziwezi kuzaa matunda au kuwafaa kwa hao wakulima na maskini wengine katika mazingira ambayo rushwa imetapakaa kila sehemu. tena rushwa yenyewe ni ile kubwa ya kuanzia kwenye roho ya uchumi wa nchi kama BOT ambao ndio wako responsible kufanya sera za fedha na uchumi zi materialize sasa wakobobea kwenye rushwa sera nzuri za wapinzani katika uchumi zitafaa nini?

Katika mazingira ambayo rushwa inayohusisha ubinafsishaji wa migodi na utoaji wa migodi kwa bei sawa na kutupa sera za madini za upinzani zitafaa nini? maana madini yataisha pengine hata kabla wapinzani hawaja shika dola! ndo maana katika mazingira ya rushwa na ufisadi lazima upinzani na watanzania wengine wenye mapenzi mema wapambane kwanza na rushwa kwa nguvu zao zote?

Katika mazingira ambayo uzalishaji wa nishanti kama umeme umezungukwa na rushwa, sera nzuri za nishati toka upinzani zita faa nini kama wataingia madarakani tukiwa tuna mikataba mibovu kama IPTL? upinzani uta fanya nini na sera zake za nishati? ndo maana lazima rushwa iwe ajenda muhimu ya upinzani na watanzania wote.

Hali ya rushwa na ufisadi katika nnchi yetu imefika mahala pabaya kiasi kwamba hakuna sera yeyote nzuri inayoweza kufanya kazi kuwa letea watanzania neema! tunazo sera nyingi tu katika sector mbali mbali ndugu mchambuzi unafikiri ni kwa nini hazibadilishi maisha ya watu????? ni rushwa ndo adui yetu? ni rushwa inayo tukosesha fedha za kujenga na kuweka madawa hospitalini.

Ni rushwa ianayo tunyima fedha za kujenga mabarabara, ni rushwa inayo tunyima haki wanyonge katika huduma mbali mbali. ni rushwa inayo shusha utu wetu watanzania.

Na katu sio sera ndo maana na unga mkono juhudi zozote zile zinazolenga kutokomeza DUDU hili baya kwa maendeleo ya Tanzania yenye neema. tukikazana kutengeneza na kunadi sera tutajikuta tanzania haipo tena! maana mafisadi walarushwa na wazembe watakuwa wamesha igawa au kuiuza kabisa.Ni lazima tuwapigi vita sasa na kwa nguvu zetu zote huku tukitengeneza sera za kuwakomboa watu maskini wa Tanzania.

Mungu ibariki tanzania na watu wake wote nanao litetea taifa letu kwa moyo safi na dhati!!
 
Mwanakijiji,
Hiyo news uliyoirusha LIVE Bongo Radio utaifanyia ukarabati kabla ya kuirusha tena KLH News au utairusha kama ilivyokuwa mwanzo?

Kama una nia ya kui-edit kabla ya kuibandika KLH News, mimi nina ombi kwamba tuwekee original version for some hrs then weka hiyo utakayoi-edit, maana nimeona magazeti mengi yameshindwa kutaja majina, na wengine tuna interest za kupata kitu na box. Lakini kama unahisi kunaweza kuwa madhara kwa upande wako basi nitakubali kusikiliza news uliyoi-edit maana usije ukaingia kwenye kikaango.
 
Kama ni kweli wamemtaja Muungwana kwamba ni mla rushwa, naamini ni kosa kubwa. Inabidi kucheza divide and rule, hata kama muungwana ana kula rushwa basi kwasasa angewekwa pembeni kwanza ili kumgawa yeye na Lowasa. Hatari hapa ni kwamba kama wananchi wengi hawataamini kwamba Muungwana ni mla rushwa basi hata madai juu ya hao wengine nayo yatapuuzwa.

Ninakubaliana na wewe kwamba kuwagawa JK na EL inaweza kuwa strategy nzuri, lakini njia kama hiyo iliwahi kutumika awamu ya tatu ambapo kila kukicha Sumaye alikuwa akiandamwa na tuhuma za rushwa huku BWM akiwekwa pembeni. Cha kushangaza ni kwamba Sumaye hakuwahi kujibu tuhuma hizo na badala yake BWM ndiye alikuwa akimsaidia kujibu kwa kusema kwamba huo ulikuwa ni wivu wa kisiasa.

Kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba kama JK ni msafi (si mla rushwa), basi mawaziri na watendaji wake wakuu wangekuwa waoga sana wa kula rushwa. Angalia majibu yake kuhusu maswala ya Richmond, Rada, Buzwagi, ANBEM na mengineyo, majibu yake yanakuonyesha wazi kwamba he is not interested in combating corruption.

Suala la Rada alikiri wazi kwamba "tumwache Mzee wetu apumzike", Richmond akasema aliita file na hakuona kama ile deal ilikuwa na connection na mtoto wa mkubwa. Kwenye Buzwagi hakutaka kusema yeye akaishia kumtumia mwandishi wa habari kwamba NK ni waziri so hakuna haja ya yeye kujua kama mkataba umesainiwa au la.

Yaani mwenyekiti wa baraza la mawaziri hajui nini kinafanywa na waziri wake? Ina maana waziri wanaweza kuuza mbuga za wanyama kwa wawekezaji bila rais kujua, na wala hawezi kuulizwa, je huyo ndiyo unatakiwa kumtenganisha na watendaji wake wakuu ambao ni wala rushwa?

Impliedly ameisha onyesha wazi kwamba anawatetea kwa nguvu zote, kwa hiyo na yeye inawezekana yumo japo havumi au anakwenda kwa kunyata na siyo kama wenzake wanaokwenda kwa kishindo wakijua kwamba wana full support ya mkuu wa kaya na likitokea baya basi JK atajua namna ya kuwasafisha maana PCCB iko kwa ajili ya kuwasafisha kwa sabuni za marashi mazuri na kuwanukisha na utuli wa nguvu!

Kumuweka JK kwenye orodha au kutomuweka kwa maoni yangu naona kwamba haina tofauti yoyote. Hao hao akina EL na RA wanajua jamaa anakula vipi na wapi, na si ajabu akina EL na RA huwa wanamkatia pansenti yake kwenye ma-deal yao.

Kama anapata mgao unategemea hata ukimtenga ndiyo atawafanya nini hao waliotajwa? Sana sana ataagiza PCCB wafanye kazi ya kusafisha na kuja na report kama ya Richmond kwamba kulikuwa na mapungufu kidogo lakini hakukuwa na rushwa yoyote!
 
Hizi ni siasa za udaku. kutaja viongozi wala rushwa ndio itakupa ushindi 2015?

This is an absurd accusation, how are are you sure that Mrema
want to contest for presidency in 2015?

And suppose he didn't mention them could that give him victory in 2015?

How can you blame someone who has the courage to raise his finger to point to those who without mercy plunder the economy of our country and let millions of our brothers and sisters live in an unbearable poverty?

What is the best stratergy according to you? to act and play like CCM? and thus according to you they will be matured?

I agree with devide and quanqer stratergy as supposed by Mtanzania but if truly JK was also involved in those scandal there is no way out the society could be made aware of that fact,and this could make the people to continue to believe that he is clean while not(incase he was trully involved),the effect of this is that ,it would give him a chance to revive CCM strength in the future and thus continue to defeat wapinzani for along long time.

You can not change the mind of People concerning JK if you dont show them who a Really JK is, never expect that by trying not to involve JK in the scandal(if he trully did) will shift the love of people from JK to Wapinzani.never!

First you have to discredit him before peoples eyes, then people will say that "we chose you with 80% of our our precious vote but behold you too you are among them )(if trully he is).
then here the love of people will really shift from him to those who raise their voices for them

The move of wapinzani which i see here, is to awaken the people and show them that though you think in CCM there are only few people who are corrupt, but the truth is that even those who you think are clean, they are not clean at all they are corrupt too.this will put CCM on the offensive.
 
Hivi SERA ni nini? Je, CCM ambayo watu wengi wamekuwa wakisema kwamba ina sera nzuri na zinazouzika kwa wananchi, sera hizo zimewasaidia vipi wananchi wa Tanzania ambao wamebaki kuota ndoto za "Maisha bora kwa kila mtanzania?"

Mara nyingi ninadhani kwamba tunaweza kuwa carried away na hizi termilogy za kisiasa ambazo haziko clear, sana sana zinawasaidia hao wana CCM ili kuendelea kuitafuna hii nchi huku wananchi wakiendelea kushabikia kwamba CCM ina sera nzuri. Inawezekana sera hizo hizo za CCM zinapinga ulaji na upokeaji rushwa, lakini ni hao hao wana CCM wametuonyesha walivyo wataalam wa kuiba kura na kutoa rushwa.

Uchaguzi wa mwaka huu umefichua mengi maana inasikitisha unapokuta Katibu wa CCM wa wilaya ametuhumiwa kula rushwa au kakutwa na kura fake kwenye chumba cha kuhesabia kura. Mahali tulipofika sisi watanzania hatuhitaji maneno matamu na laghai za hapa na pale, tunahitaji ACTION zaidi kuliko hizo sera ambazo zimebaki kuwa kwenye maandishi na inapofika wakati wa uchaguzi ndio utasikia kwamba waulizeni wapinzani wana sera gani?

Lakini uchaguzi ukipita hakuna anaeongelea sera tena bali wanachangamkia tenda ya kuchukua chao mapema within 5 yrs ili wasije wakatoka wakavu just in case wananchi wakiwashitukia.
 
Unajua tangu aingie madarakani JK amekuwa akiepushwa na kila aina ya uovu kuonesha kwamba yeye sio sehemu yaya tatizo. Yote hii tunarudi kulekule kwenye kautamaduni ketu ka-ovyo: unafiki na nidhamu ya woga, kumwambia mfalme amependeza wakati yupo uchi! Huu nao ni ujinga ambao lazima tufike mahala tujikomboe nao. Sasa walichofanya akina Dr Slaa ni kuweka record straight. Sasa ukiseme kumtaja muungwana ni kosa nashangaa, mimi nafikiri hoja sio hii. Hoja ni je na yeye ni kweli ni mfisadi? Sasa kama ni mfisadi kwa nini asitajwe kama wengine wanatajwa? Kama mnatetea muungwano kutokutajwa, vipi mnasema Mkapa ashtakiwe kwa ufisadi aliofanya, upi huo kama tunasema wasitajwe? Ukombozi ni safari ndefu, lakini lazima tuitembee!

By the way what Dr Slaa and the opposition have done is more than a political manouver, it is waging a really war against corruption. Tukielewa hili hatutajadili whether it is right or wrong to name the muungwana. But if you just see what happened yesterday as a political move, then you may be fairly right to say kumtaja muungwana ni kosa. Sasa kwa yeye kuwa katika list of shame ile ya jana, tungeachana na hili jina la kumuita muungwana. tafuteni jina lingine, for sure he is not muungwana!
 
Kitila Mkumbo,
Kula 5 Mzee wangu, kweli jina la Muungwana limekuwa overtaken na events, bora lile jina la BoyZ II MeN (msanii) lirudi japo siku hizi wamekuwa wakali sana na hawataki kuitwa kwa jina hilo. Kinachoendelea hapa ni mazingaombwe na business as usual!
 
Siasa ni game ambayo timing is everything; mimi sioni kama kumtaa JK ni kosa...JK mpaka sasa hajanionyesha kitu chochote cha kumuona mjanja sana kwenye hii game ya siasa. Sasa Dr Slaa ameshamtaja, tusubiri tuone JK atajibu vipi..maana kumtaja itakuwa kosa iwapo JK atajua namna ya kujibu vilivyo na kuweka public on his side...lakini pia kama public inayofikiri itawezekanaje kumtoa JK kwenye uozo huu???
 
Hizi ni siasa za udaku. kutaja viongozi wala rushwa ndio itakupa ushindi 2015? mrema hajifunzi tu na hawafundishi wenzake kutorudia makosa yake? ndio kuna wala rushwa wengi ccm lakini kuishia na sera ya kuwataja tu na kuwaanika hadharani ni siasa za udaku tu. Upinzania should begin kuwa serious.


NAdhani mchambuzi ana ukweli ndani yake. Kuna posibility ya kuwa kweli hizi ni siasa za udaku, na ni siasa za udakau kwa kuwa waliotajjwa hakuna kitakachowakuta.

Mrema alipolipua rushwa ya mamilioni iliyokuwa ikimhusu Mkapa alifikishwa makahamani na mahakama iliona kuwa hana hatia kwa sababu aliyosema aylikuwa yana ukweli. Lakini Mahakama ilishindwa kuwachukulia hatua wahusika. Kitu kingine tukumbuke kuwa Tanzania sheria sio msumeno, ikanataka upande mmoja tu.

Wanaoadhibiwa ni wale ambao hawana madaraka. Mumeona wazi kwenye kesi ya kiongozi mdogo tu Ditopile, Tibaigana mwenyewe aliogopa hata kumkamata wakati yeye mwenyewe alimwabia "mimi si mheshimiwa, ni muuaji" lakini ilimchukua muda sana mpaka yeye mwenyewe alipoamua kwenda polisi.

Sasa who can tell me that there is any person in Tanzania who will dare to bring those big shots in justice? Hakuna dalili hata kidogo kwa watu hao hata mahakama kujaribu kuwaita.

Mkapa was better than others, lakini he became worse baada ya kuona whatever he will do, there is no one in administration strong enough and clean enough to point fingers at him, He was smart on this.

Ndio maana sasa hivi hata magazeti yakiibua scandle zake yuko kimya because he knows they will not go anywhere, kwa hiyo ni kweli kama anavyosema mchambuzi ni siasa za udaku. Upinzani wanatakiwa kuwa more serious, kuonana na mabalozi ni sehemu moja tu more is needed, wafanye juhudi zaidi ili rushwa iwasambaratishe CCM.

Sidhani kama ruswha serikalini na CCM kwa sasa ni siri. Lakini hakuna mwenye uwezo wa kufight, Ukiona jina moja limetejwa jue kuna watoto wao, ndugu zao, marafiki zao na hata wenzo kwenye big capitals in the world wananufaika. Sitashangaa Kabwe, Slaa, na wengine wanaopinga rushwa Tanzania wanaishia kufa kisiasa kama Mrema, au kufa kama kina Kolimba.

Mkapa was smart, if you can not beat them, join them....and that is exactly what he did now no one can beat them
 
the question still remains 'WHAT ARE YOU GOING TO DO ABOUT IT'??
 
Ikitokea mmoja ktk ya waliotajwa akaenda mahakamani sindio itakuwa mwisho wa mchezo,kama vile kesi ya dito.Hapa panatakiwa hamasa ya wananchi kuwashikia bango hawa walarushwa hata kuandaa maandamano ya kuwazomea hata kwa wiki nzima mpaka waamue kujiuzulu.

Inabidi kuhamasisha wananchi juu ya hili na sio kuliacha lipite.

Hivi mrema alitaja watu gani sijaona majina hali popote.Leo magazeti yote yamefyanta kuandika majina kwa kuogopa kudaiwa fidia basi kazi ipo.
 
Yeah that is a milion dollar question "What are we going to do about it". Kuna wengi wanaotajwa sana na wengine hawatajwi kabisa. I was expecting Nalaila Kiula kuwa gerezani lakini he is not and he will not be in prison, wengi wako serikalini are still enjoying red carpet traetment, lakini are worse than those who we think they are who are now serving their terms. Who will rescue us on this, sisi watanzania tumeshindwa.......
 
Unajua nimesoma baadhi ya comments humu inajikuta naaza kujiuliza ninaishi katka jaami ya namna gani hii Tanzania.Mtoto mdogo akiwa na njaa hufikisha ujumnbe wake kwa kulia then mama yake humuandalia chakula na kumlisha.

Sitaki niamini kuwa Wanzania na mindevu yetu na wajukuu lukuki tumedumaa kiasi cha kuwa watoto wadogo ambao tunahitaji kuandaliwa chakula na kulishwa.

Baba (Watanzania)mwenye nyumba amelia ana njaa,kaandaliwa chakula,eti anataka (housegirl) amlishe???Njaa niya Watanzania sio ya wapinzani.Kama hatutataka kula ni juu yetu.

NOTHING IS UNBEATABLE unless tumeridhika na hali hiyo.Watanzania tunataka tuamke na kukuta nchi imekuwa EDEN!!Tunataka tufanyiwe kila kitu,huku sisi tukiwa tumekunja mikono.Wapinzani hawafanyi hiki,wapinzani wahafanyi kile!

Tunatafuta watu wa kuwalaumu kwa uzembe na u-lazy wetu.Haya tuendelee kuwakumbatia hawa majambazi tuone nani anaumia.
 
Kitu kingine ni hicho cha kukosekana kwa mazungumzo juu ya sera. Kuongelea rushwa ni vizuri lakini kilicho muhimu zaidi ni sera za chama na jinsi ya kumkomboa Mtanzania kutoka kwenye umaskini.

Mtanzania, asante kwa hoja yako nzuri.

Inasikitisha kuona wengi wetu humu JF wakipata nafasi ya kwenda kumkomboa mtanzania wataenda kufanya ya mrema 1992 na sasa ya slaa na kabwe. Inasikitisha zaidi kuona kwamba wengi humu hawaelewi kwanini ccm haina upinzani wa maana. Narudia tena, hii sera ya kusema huyu na yule ni mla rushwa sio kwamba ni mbaya lakini isiwe ndio msingi wa sera za kuiondoa ccm madarakani.

It wont work. Why? because ikifikia push to shovel, hata ccm yenyewe ikibanwa itawageuka wanaoharibu chama - wala rushwa etc ili kujisafisha, sasa baada ya hapo kina slaa watasema nini, kwamba chama cha mapinduzi kimewasikiliza, kimewaiga? then what? Hoja yangu ni kwamba hii approach ya kubakia kupigia kelele rushwa na kuishia hapo hapo bila kuja na mikakati mingine kabambe ya kumnasua mkulima na mfanyakazi toka kwenye dimbwi la umaskini ni approach za udaku na zitaishia kujengea wana ccm safi mazingira mazuri zaidi.

Siri ya kuiangusha ccm ni kukazania mambo muhimu in the context of sera za maendeleo ya mkulima na mfanyakazi. Hii iende sambamba na mikakati ya kuchukua majimbo ya ccm kwa kujinadi na sera nzuri, sio kwa kutumia vigezo vya rushwa, wananchi wenye akili watatia shaka sana kumpa mpinzani ubunge just because ametaja majina ya wala rushwa.

Hizi za rushwa ziwe tu kama dondoo kwa sababu believe me or not, soon or later ccm ndani mle watageukana na baadhi ya viongoi ku excel kwa kusafisha rushwa while they are still wana ccm. Tupo hapa JF na muda huo ukifika tutarudia suala hili tena.

Kina kabwe wanapoteza tu muda huko mikoani, this was an aopportunity for them kunadi sera zao na mwishoni mwishoni ndio kutaja mambo ya rushwa kama mifano.
 
Back
Top Bottom