List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Bahari imechafuka, hawana pa kushikilia. Sasa hivi tutaanza kuona wekianza kutokea dirishani, kwani imeshakuwa choooo.
 
500 usd per hour is more than even what the United nations paying for the defence lawyer in ICTR, Arusha, Siera Leone special Court and ICTY (Yugoslavia).

Angalia viwango vyao hapa chini, na walio wengi wanatoka nje ya nchi husika.

i. Hourly Rates

The ICTs use a system of hourly rates for the remuneration of defence counsel. This broadly works in the following manner: each defendant is entitled to one lead defence counsel, one co-counsel, and up to three assistants and investigators. Lead defence counsel is remunerated at a rate of US $110 per hour, co-counsel at a rate of US $80 per hour; and assistants and investigators at a rate of US $25 per hour. There are caps on the number of hours allowed in a month at 175 hours for counsel and 100 hours for assistants and investigators. All members of defence teams are required to fill in forms accounting for hours spent and describing the manner in which this time has been used. These forms are then processed by defence unit staff who will make decisions on what payments will be allowed.

Source: http://www.specialcourt.org/Outreach/LegalProfession/DefenceReportSdBFEB03.html

Kwa hiyo hiyo 500 usd/hour ina harufu ya mgawo
 
Nimepitia kwa kina haya madai, na nimefikia pahala kumbe yale aliokuwa akiyaeleza ndugu yetu MCHAMBUZI kuhusu usafi wa Lowassa una ukweli fulani, maana hata Dr Slaa kashindwa kumuorodhesha ktk list yake ambayo bado inahitaji kuthibitishwa.
 
Jamani ndo utagundua kuwa waandishi wa bongo ni bongo lala yaani hakuna mhandishi hata mmoja aliyejaribu kuchimba deep ili MKONO atoe details sio bla bla za kisiasa. Swala lilikuwa je hizo 8bil ni kweli ameshazikomba au? Lakini ni obvious yes.
 
Wandugu

Hiki ni kipindi cha mpito; haya yaliyosikika mpaka sasa ni rasha rasha mvua yenyewe bado haijaanza kunyesha. Dr Slaa & Co wamejitolea sana kusema waliyoyasema hadharani na kama tunavyoona wenyewe mpaka sasa Serikali kupitia Mzee Kingunge na Mkono wote hawana la kusema wamebaki kukurupuka.

Cha MUHIMU ni sisi wananchi kuwapa USHIRIKIANO hawa wapinzani na WANAHARAKATI wetu; hawako safi kwa 100% lakini ni wazi kuwa wanaweza japo kushtusha wananchi jinsi nchi yao inavyofilisiwa na wageni; sasa katika hali kama hii ambayo rasilimali zetu zinaibiwa kwa kasi ya ajabu ni muhimu kutoa ushiriano wa dhati. Tuache siasa pembeni; hii ni nchi yetu wote.

Wanaolipwa $500 kwa saa sio Mkono peke yake; hakuna haja ya kupaniki...mengi maajabu yatasikika na watanzania watajua....time will tell.
 
Hii ni Orodha ya ufisadi BOT.

Ikifanyika Foresinc Accounting ya Mgawanyo wa Fedha zilizo wekwa kwenye account ya Tangold hatutaona wakuu wakimegewa Miela wakuu mbali mbali?

Pindi ikitoka LIST of SHAME ya Ubadhirifu wa Mali Asili Kasheshe litakuwaje?

Vipi kuhusu Ubadhirifu katika Hamashauri za Wilaya na mikoa?

SISIEMU wamekuwa wakijenga na kusambaza hofu miongoni mwa wananchi wa Tanzania juu ya kuangukiwa na nguvu za Dola, kuuawa, kunyimwa uwezo wa kufanya shughuli za kiuchumi, na haki ya kutoa mawazo bila kubughudhiwa ili kuendelea kuiba na kutawala na kudumaza maendeleo ya walio wengi Tanzania.

Wako viongozi kadhaa walio waadirifu ndani ya SISIEMU. Viongozi hawa wanashindwa kufanya kazi zao Vizuri kwa sababu Mahabithi na wenda wazimu kama akina Mkono wanatumia utajiri wao Haramu na Ukiritimba wa kisheria kujenga Hofu na kuitawanya kwa kila Kiumbe Tanzania.
Baadaye Mahabithi hawa wanachomoa vijisenti kwennda kujikosha huko majo=imboni mwao kama Musoma Vijijini kwa kujenga vijishule na kulaani mambo kadhaa hapa na pale kuhusu ubadhirifu.

Watu hawa wajenga hofu, nia yao kuu ni kucheza viwanja vyote vya Ufisadini kwa aibu yote, kisha kujibadiri haiba na kujitoa kimasomaso mbele za wananchi kwa vikofia vya Tarabush kana kwamba Heshima na Hekima zao zi juu ya Hekaya zote za uadirifu.

Njama zao zinapoanikwa hadharani wanasema mengi huku wa kijikanyaga kanyaga na kutoa matamshi tata na yanayo pingana. Katika hatua inayoonyesha kujawa na hasira ya kuumbuliwa undani wa ukweli wa utajiri wao wansema wako tayari kumlamba mtu makofi na ngumi ili kulinda heshima zao zilizo jengwa juu ya uoza.

SISIEMU hawaamini kabisa kwamba njama zao zimeanikwa mbele ya Hadhara ya Watanzania na hawana cha kufanya leo wala kesho.
SISIEMU hawaamini kwamba huu ndo mwanzo wa mwisho wa Himaya yao ya Ubadhirifu na Ufisadi.

Kila Strategy wanayo jaribu kujipanga nayo haitekelezeki kwa sababu imejengwa juu ya utelezi wa uoza wao wenyewe.

Kwanaza walisema wataandama nchi nzima wameshindwa kuandamana.
Wattandaman kupinga nini na kuunga mkono nini.

Sasa wana dai watapita nchi nzima kuwwambia wananchi wapuuzie madai ya viongozi wa safu ya upinzani. Ukweli ni kwamba hilo haliwezi fanyika.

Tatu uamuzi wao ulikuwa ni kuzuia magazeti kuandika LIST OF SHAME,jambo ambalo walifanikiwa, kisha wao SISIEMU kukaa kimya na kuipuuzia list hiyo.

Hili la kukaa kimya limewashinda kabisa wameanza kusema na kila akisimama kusema anasema lake.
 
nimepitia kwa kina haya madai, na nimefikia pahala kumbe yale aliokuwa akiyaeleza ndugu yetu MCHAMBUZI kuhusu usafi wa LOwassa una ukweli fulani, maana hata Dr Slaa kashindwa kumuorodhesha ktk list yake ambayo bado inahitaji kuthibitishwa.

Naona amemsahau tu huyo.
 
Huyu Mkono, on this one hana ujanja maana so far hagusi the real evidence, anaruka ruka tu na maneno mengi ya siasa, badala ya kuzikata evidence,

nilitegemea kuwa kwanza ataikata evidence mwenyekiti wa kamati ya bunge iliyomchunguza na kuamua kuwa kunaharufu za uajnja kwenye deal zake na BOT, na kwamba malipo aliyokwisha lipwa na BOt yanapita kiwango cha serikali cha 3% only, sillingi Billioni 8, zinapita kwa mara kumi ya kiwango hicho, hayo ndio nilitegemea atayagusa,

yeye anasema Dr. Slaa alitakiwa kuwa padri, sasa waht that has to do na evidence? Hawa waandishi wa drive by media na Rostam ndio maana haswa tuliamua kuwepo hapa forum, mpaka kieleweke!

Wakuuu tuendelee kupiga mawe, tembo akose usingizi angalau!
 
Mkono ameanzisha Kesi Mpyaaa!

Ninataka kujua ni nani ndani ya Serikali na BOT aliidhinisha malipo ya $500.00 kwa saa.

Mtu au kundi hilo la watu wana kesi ya kujibu nchini Tanzania.

Huyu Jamaa kanitibua nyongo vibaya sana.

Nina mawazo ya kutisha juu ya mafisadi hawa.

Hawafai kabisa kuendelea kuvuta hewa mahali popote duniani.


Kuibiwa Sasa Basi.
 
By the way!, .....the Dataz.....ni kwamba wakulu wate wapo NY, kuanzia Muungwana, Sumaye, Salim, Membe, Ngasongwa, Jaka Mwambi, Sophia Simba, Mramba, Mwandosya, Mama Nyoni, Sefue, Daraja!

Msafara karibu watu 120, hivi anayelipia hiyo gharama ya usafiri wao ni nani? Mwenye .....dataz...by the time wanarudi bongo serikali itakuwa imetumia hela ngapi za walipa kodi?

I mean wafanyakazi wa serikali hawapati mishahara, hawa jamaa wanasafiri tu, yaani sasa imekuwa mkomoeni tu, no wonder wanauana kwenye uchaguzi hata wa NEC,

Mkuu Dr. Slaa na Zitto, hebu lichungulieni na hili la safari nalo, vipi maana walalahoi sasa tunawaaminia!
 
kule waziri wa fedha anasema tujifunge mikanda ili tuweze kuleta maendeleo. wafanyakazi mishahara dhalili, huku kuna watanzania wenzetu wanaramba asali ya nchi kwa ulimi bila ya kutia kidoleni.

kwa hali hii iko siku watanzania watachukua maamuzi ya hatari. lazima wajue waburundi warwanda hawakuzaliwa wapigane. Darfuur na kwengineko yalianza hivi hivi wachache wananufaika sana na keki ya nchi na wengine hata harufuye hawaijui
 
Hivi kweli katika serikali ye JK hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuja na kuwaambia wananchi kuwa ni sahihi kwa Gavana wa Benki Kuu kuidhinisha malipo ya mabilioni ya shilingi kwa kampuni ambayo yeye na viongozi wengine wa juu wa serikali ni wakurugenzi?

Hivi kuna ugumu gani kwa kiongozi mmoja kusimama na kusema kuwa kwa Rais Mkapa kuanzisha biashara akiwa Ikulu akitumia anuani ya Ikulu kama anuani yake na kuweza kupata mkopo wa mamilioni ya shilingi ni sawa haina tatizo?

Kwanini asije mtu akatuambia kuwa viongozi wote wa serikali (siyo Rais peke yake) wana uwezo wa kutumia anuani za ofisi zao kama anuani zao binafsi wanapoomba mikopo?

Hivi kuna ugumu gani kwa watetezi wa serikali kusimama na kusema kuwa kwa Rais Mkapa na Waziri wake wa Nishati na Madini kuidhinisha mkataba wa kampuni ya nishati kuuuza umeme kwa Tanesco wa mabilioni ya shilingi ni sawa tu nahasa kama kampuni yenyewe wao ndiyo wana hisa wakubwa?

Kuna ugumu gani kwa wao kujibu hoja kwa hoja? badala ya kutoa kejeli na kuzunguka zunguka tu kama wanawanga!
 
Kule Spain ktk ule mkutano wa UN kuhusu mazingira, baada ya ku-present papers zetu hatua iliyofuata ilikuwa ni kukutana NewYork kwa zile nchi ambazo proposal & presentation zao zilikubalika ili kupata MSHIKO toka NewYork............kwa hiyo wiki hii yote niko hapa NewYork kabla sijarejea kwa walioniajiri.....................I was very happy to see the Tanzanian presentation & proposal ikipita.........Mama Mollel alifanya kazi nzuri sana siku ya presentation.................angalau ilifunika yale "mashimo" ya msafara wa wajumbe KUMI NA MMOJA
 
Nchi hii kwa mtindo huu, haifiki mbali na JK na hao watetezi wako kama hadi sasa wapo humu jitokezeni hadharani na kuchukua maamuzi mazito haya, hii ni nchi yetu sote jueni kwamba kuna siku ninyi hamtakuwepo na kama mnataka kuishi kwa amani basi kuweni wakweli kwenye hili.

Nchi haiwezi kuendeshwa kiujanja ujanaj kama mnavyoendelea kuifanya iende , hamuwezi kuendelea kwenda vijijini kuwadanganya watanzania waliokosa elimu milele na pia jueni kizazi cha sasa kinapata taarifa mapema kwani hata mkificha leo kesho zitatoka hadharani.

Slaa jua kwamba haupo peke yako , tuko nyuma yako , hata kama wakiondoa roho yako mawazo yako yataendelea kudumu milele, ni heri kufa umesimama kuliko kuishi ukiwa umepiga magoti. haya ni maneno ya CHE GUEVARA.
 
Leteni habari waungwana, mambo yatakaa sawa tu, hakuna marefu yasio na mwisho.
 
Kwenye hili Mzee FM Es nimekukubali ila zile za udaku na spinning hapana . Hata kama maisha yako ni siasa maana umezaliwa kwenye siasa , tufike mahali tukubaliane na mambo ya Kitaifa pale yanapotukuta kama sasa. Nimekukubali kwa hili maana ni ukomavu.
 
Kwenye hili Mzee FM Es nimekukubali ila zile za udaku na spinning hapana . Hata kama maisha yako ni siasa maana umezaliwa kwenye siasa , tufike mahali tukubaliane na mambo ya Kitaifa pale yanapotukuta kama sasa. Nimekukubali kwa hili maana ni ukomavu.

Haya mkuu tuendelee kukata ishus, ingawa sikuzaliwa kwenye siasa na sina spinning yoyote, mimi ninamkoma nyani tu giladi,

siangalii sura ya kiongozi wala chama, ni mawe tu magazeti yetu bongo yamenunuliwa na vyama vyote vya upinzani na CCM, sasa ndio maana tulikuja hapa kuweka mambo sawa, hatutaki uongo wala spinning, ila tunataka ukweli tu and in the process hii ni burudani kwenye bulogu, na I am having a lot of fun mkuu!

Kwa hiyo mkuu tuendelee kukata ishus!
 
Kuna taarifa za kuaminika kuwa katibu mkuu wa hazina ambaye ni miongoni mwa mafisadi waliotajwa kuwa kaitisha press conference na ndio inaendelea muda huu .

Sijajua bado kile kinachoendelea ila najua kuwa ni miongoni mwa mafisadi wanaotuhumiwa .

Mwenye yaliyojiri tafadhali tupe hapa kijiweni.
 
Bado anajisafisha ila waandishi nao wako wanampa makombola nafikiri habari kamili baadae kidogo.
 
Back
Top Bottom