List ya Matajiri 10 katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) mpaka Juni 26, 2023

Mbona mwanangu Zero IQ hayupo? Msinambie ameuza hisa zake zote katika soko la dar, na kutokomea ugaibuni kwenda kuwekeza huko.

Ila tuache masihara, hawa jamaa wa Top 10 hii nawaheshimu sana, investment zao zote ni kwenye Mabenk na Cement. Turudi kwenye watu wanaofahamu tabia za investment kwenye masoko ya hisa, kupanda na kushuka (Halafu kuna Kuporomoka kifo cha mende) kwa hisa, wanaweza kunielewa. Ukitaka;

1) Kufa kabla ya siku zako.
2) Kupata msongo wa mawazo kolabo na kisonono ft wazimu.
3) Kusahau nguo za ndani (Chupi) inavaliwa vipi.
4) Kuwehuka.
5) Kupata High Blood Pressure kabla ya umri wa uzee.
6) Mke akukimbie kwa kisirani kisichoisha.
7) Kupata kipara kabla ya umri.

Fanya investment kwenye soko la hisa la Dar Es Salaam Stock Market (DSE).

Tanzania yetu biashara ni sawa na kucheza kamari MBET au Wasafi BET, unahitaji uwe na moyo wa chuma kama waliopitia mafunzo ya kivita. Leo mnaweza kulala kwa amani kabisa kibiashara na kodi, kesho mnaamka na;

1) Miswaada mipya ya mabadiliko ya kodi ishapelekwa bungeni huko, na wabunge au mawaziri wetu vichaa.
2) Sheria mpya za mabadiliko ya kupandishwa kwa kodi ishatungwa au kubadilishwa na Bunge. Au sheria ndogo zishatungwa za kodi/biashara na Waziri, BOT, TRA na mpaka halmashauri mamaqe.
3) Muda wowote mnaamka mabadiliko msiotegemea wala kuwaza akilini. Yani muda wote mpo kwenye parade, mguu upande/mguu sawa/kushoto geuka!!! Waaah!!!

NOTE THAT; Tanzania hatuna mazingira rafiki wala sheria rafiki wala zilizo stable za kibiashara. Muda wowote chochote kinabadilishwa. Kitu kinachofanya biashara mpaka za kwenye soko la hisa kuwa halipo stable wala halisomeki hata uende Havard!

Usione Bakhresa na utajiri wake wote wa matrillioni amewekeza USD Million 1.5 tu, au usione Mo Dewj wala mabillionair hajaweka hata Shillingi zao kwenye soko la hisa DSE basi ukaona jamaa ni mabwege au vichaa! Wana akili sana. Jaribu wewe uone upepo wa kisulisuli una rangi gani!
 
Baharesa anazungusha hela yake maana DSE ni kusubiri GAWIO ndio maana MO humuoni na ni matajiri
 
Hakuna uwekezaji rahisi, market value business (hisa, hati fungani, amana n.k) ni uwekezaji mgumu japo unalipa sana ukiufahamu. Fuatilia hao Mangi utakuta wamepiga kitabu wengi CPA na wahasibu wabobezi hao makanjibai (Wahindi) ndio kila leo yanaandika vitabu vya uhasibu tunavitumia kwenye mavyuo yetu, ni wabobezi sana kwenye uwekezaji wa mitaji. Yote tisa nawaogopa sana wale wanaofungua kampuni na kuikuza na kuzisajili stock market.
 
Wakuu tafuteni pesa ,list hii inamsaidia nini mkulima wa huku lingusenguse?
inamsaidia Kwa sababu we always get motivated by other's success,so he will work hard, lakini pia anaweza akawaiga siku akipata pesa ainvest kama wao,so they bacome his role model.
Kwa hiyo Mimi Naona inamsaidia.
 
Hongera kanda ya Kaskazini
 
Hao wadosi hawana hela. 🤣 Kuna raia wana hela kuliko hao wa DSE
 
Hivi wakithaminisha ng'ombe wa mfugaji mmoja wa kisukuma au mmasai si tunaweza kupata mshindani wa hawa wenye hisa?

Man’gombe hayana hata thamani ya $1 million hakuna kwa mfugaji yoyote nchini. Ukiona mtu ana hisa zene thamani ya $5 million it means ana assets nyingine zene thamani hata ya $15 million.
 


You’re not a risk taker. Mambo sio complicated kama unavyoonesha hapa. Mtu kawekeza hisa zake more than 23 million in US dollar katika Bank mbili za uhakika CRDB na NMB. Hizo ni Bank bola na kubwa nchini hata ukwasi wake sio wa kipuuzi ni bank zilizo na maslah mapana kwa taifa ndio maana kila mwaka zinatangaza faida na gawio nono kwa wanahisa na serikali. Viwanda vya simenti, steel, iron sekta ya nishati kama gesi huko hakuwezi kutetereka hata siku moja kwasababu ya uhitaji wa bidhaa zake. Hao kina dewj wana viwanda vya ndio maana hawajawekeza fedha zao kwa mtu au taasisi yoyote ile. Wakati unajiuliza wenzio wanapata magawio ya kufa mtu ni juzi tu huyo Hans macha alipata gawio la $1.5 million kutoka CRDB. Kuwekeza ni mahesabu sio bra braa za kilimo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…