List ya vijana 50 wenye ushawishi yatolewa: Wapo Samatta, Kibatala, Millard Ayo, Ali Kiba, Msando

Zamani nilikuwa nasikiliza top ten kwenye radio mbalimbali. Mfano clouds fm, radio one, magic fm etc. Sasa kwenye hizo top ten ilikuwa vichekesho.

Wimbo ulioshika namba moja radio one( kwa maana ya wimbo ambao unakubalika zaidi kwa wasikilizaji), ukisikiliza clouds fm wimbo huo huo ulioshika namba moja radio one, kwenye top ten za clouds fm umeshika namba 10.

Sasa haya matokeo ya watu wanaokubalika ama wenye ushawishi zaidi nchini yananikumbusha top ten nilizokuwa nasikilizaga enzi hizo na zinazoendelea kwenye radio mbalimbali nchini Tanzania. Nimesoma list ya watu 50 wenye ushawishi Tanzania, nimebaki kucheka peke yangu. Hivi inawezekana kwa mtu kama Mjomba Msumari ambaye hajulikani hata mtaa wa pili kuwa na ushawishi kwa jamii?

Hawa watu AVENCE MEDIA, kuna kitu si bure aisee. Na ningeshauri vyombo husika kuwachukulia hatua za kisheria kwa kusema uongo, maana huu nao ni upikaji wa data.
 
kama mange kimambi hayupo basi hakuna list hapo kuna utumbo.
 
Chanzo ni Clouds Media, Facebook

Mbwana Samata ameongoza list ya vijana 50 wenye ushawishi nchini Tanzania, Millard Ayo ashika nafasi ya 3, Ali Kiba amfunika Diamond Platnumz


View attachment 677091

Ningeiheshimu na kuipongeza hiyo list endapo tu Mtanzania ambaye nadhani amefanya makubwa na anastahili Heshima kubwa JamiiForums Founder Maxence Melo angekuwepo. Niseme tu ' Personally ' nimesikitika mno yaani katika list hiyo kuna Watu wengi wa ' hovyo hovyo ' tupu halafu Mpigania Uhuru wa Kujieleza Mitandaoni na ' Genius ' aliyetukuka kabisa na ' Mtani ' wangu Maxence Melo kukosekana.

Kwenye hiyo list Watu ambao nawakubali na wanastahili kuwepo bila utata wowote kutokana na umuhimu wao ni hawa wafuatao tu:

  1. Mbwana Samatta
  2. Peter Kibatala
  3. Joti
  4. Patrick Ngowi
  5. Dina Marios
  6. Babie Kabae
  7. Salim Kikeke
Waliobaki wote ni bure kabisa na hawana faida wala umuhimu wowote na nadhani hiyo ' Taasisi ' iliyofanya huu mchakato inapaswa kutuomba radhi haraka kama siyo upesi sana Sisi Great Thinkers ' tuliotukuka ' kwani ilichokiandaa ni ' Kituko ' cha Kutufungulia mwaka wa 2018.
 
Hakuna haja ya kuponda list yao. Cha kufanya kila mmoja aandae list yake halafu aitupie hapa. Nadhani itapendeza...!!
 
Maxence Mello hayupo???
Malisa Gidlisten je??
vipi Mike Mushi?

kaseja sijui kafanya nn mwaka 2017
 
Hiyo imetolewa na mshikaji akiwa ghetto kwake hili achapishe kwenye blog yake.
 
Consigliere naomba nomination niwepo kwenye list pls.. Huyo kwenye avatar ni mimi na jina ni langu... Umoja ni nguvu tufanye jitihada na JF tupate wa kwetu kwenye hiyo list[emoji144] [emoji144] [emoji144]
Tunaambiwa Makonda ni maarufu kwa nini hayumo humo?
Tutakata rufaa kama Dr Remmy alivyokata rufaa kwa ushindi Wa Masudi sura mbaya[emoji1] [emoji1]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…