Eyce
JF-Expert Member
- Mar 16, 2016
- 7,185
- 24,330
Sijawahi isikiliza kabisa hiyo nakupenda, nimeisikia sikia nakuona clips wakati ikitrend,hivyo sijasikia mashairi yake, melody ni nzuri ila naamini UTU ni bora kote kote, kale ka biti, mistari na melody yake.
Jana nimeisikiliza vizuri mnoo, akili ikaniambia kiba HAWEZI andika mistari kuntu kama hii, hizi ni level za kina harmonize, mondi hivi.
Kiba vimashairi vyake ni ujanja ujanja, kuna baadhi ya ngoma kuna mashairi mazuri na sina hakika na mwandishiwa hizo ngoma.. Mfano mwingine ni DUSHELELE, ukisikiliza yale mashairi unaona huyu aliandika akiwa katuliza kichwa... Na siku hizi kaacha zamani ngoma nyingi alikuwa anajitaja ALI, mfano ile aje bonge la ngoma, melody ni A+ mistari ni B ama C kabisa.
Umemshusha sana 😁😁😁😁
Mbona hata mapenzi yanarun dunia ilikuwa nzuri sanaaa
Halafu nilichokijua, hizi labels mara nyingi ukiangalia nyimbo zinavyotoka, unajua kabisa kuna mkono wa mtu aliyeandika
Binafsi nikifuatilia historia ya nyimbo za harmonize kuanzia Aiyola hadi anatoka WCB, itakuwa ngumu sana kuniaminisha nyimbo kama wote na nitaubeba hazina mkono wa Ibrah..
Maana kiuandishi, Harmo hamfikii Ibrah kwenye nyimbo za mapenzi. Sikiliza nitachelewa ya Ibrah ndio utanielewa, na ndio maana nahisi harmo kaondoa wasanii wake wote konde gang ila Ibrah hamuachii. Maana Ukiachana na success, Ibrah ana kichwa cha mashairi