List ya Wasanii 10 bora kwa sasa Tanzania


Umemshusha sana 😁😁😁😁
Mbona hata mapenzi yanarun dunia ilikuwa nzuri sanaaa

Halafu nilichokijua, hizi labels mara nyingi ukiangalia nyimbo zinavyotoka, unajua kabisa kuna mkono wa mtu aliyeandika

Binafsi nikifuatilia historia ya nyimbo za harmonize kuanzia Aiyola hadi anatoka WCB, itakuwa ngumu sana kuniaminisha nyimbo kama wote na nitaubeba hazina mkono wa Ibrah..

Maana kiuandishi, Harmo hamfikii Ibrah kwenye nyimbo za mapenzi. Sikiliza nitachelewa ya Ibrah ndio utanielewa, na ndio maana nahisi harmo kaondoa wasanii wake wote konde gang ila Ibrah hamuachii. Maana Ukiachana na success, Ibrah ana kichwa cha mashairi
 
1. Marioo
2. Harmonize
3. Jay Melody
4. Mbosso
5. Jux
6. Chino
7. D. Platnumz
8. Zuchu
9. Alikiba
10. Nandy

Hizo takwimu ni kutokana na performance zao huku mtaani ndani ya miaka mitano ya hivi karibuni kulingana na mtazamo wangu.

Nipe List yako
msanii Budagala Mwanamalonja wa huku simiyu amekosekana kwenye listi kweli?πŸ’
 
Sikujua kama Marioo angekuja kuwa msanii mkubwa namna hii, jamaa nlikuwa namsikiliza ana style moja ya kuimba kila nyimbo analalamika na kulia, nlipokuja kumuona anaimba na amapino nikasema ohooooo!!!!

Mama amina nadhani ndio amapiano ya kwanza bongo kabla hata ya Diamond.
 
Diamond ni siku hizi tu kaishajipata, anapiga ngoma kufata upepo, ila diamond wa zamani au hata huyu akiamua kuandika mashairi yaliyonyooka anaweza, kiba uwezo wa kuandika mistari mizuri saana hana.
 
Mapenzi yanarun dunia, yes, ndio imo kwenye list ya zile ngoma chache kali kiuandishi kwa kiba.

Ibra sijamsikiliza saana, huenda akawa ana mchango kwenye uandishi ila yule KIPIPA, naamini nae ni mkali saana, mfano jana nimesikiliza na ngoma inaitwa mdomo na dharau, mule kwenye mdomo bado harmonize kaonesha ukubwa, kwenye dharau pia kaonesha ukubwa wake. Yule MJOMBA NCHUMALI ni hatari sema ndio basi tu inaonekana zaidi ya uandishi kwenye mengine ni empty set. Life skills, management nzur hana
 
Dogo anajitahidi sana. Nimesikiliza hii "hakuna matata" nikasema dogo anapita vizuri kwenye chaki
 
Kweli mkuu mond kajua kucheza na sanaa.
Kipindi harmonize yupo wasafi alipita kwenye reli ya mondi alafu akaja kujibrand alone kwa mipigo yake.
 
Enock inonga baka ndiyo msanii bora zaidi barani Tanzania. πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Nasikiliza sana ngoma za harmonize kajamaa kana uandishi flan hivi amazing
 
Msanii namba saba jamii forum.
Cha ajabu ndiye msanii namba moja kwenye kila kitu,kuanzia tuzo za ndani na nje.
Streams mtandaoni
Deals za makampuni.
Ngoma zake kutembea sana kitaani.
Habari zake kuuza zaidi kwenye media.
Tajiri kuliko wasanii wote Tanzania.
Niliacha kumshabikia Diamond alipojigeuza adui wa wapinzani na Rafik wa watawala.
Lakini ukweli utabaki kuwa ukweli.
Tanzania kuna Diamond peke yake then hao wafuatao ndiyo top ten
Kwa hiyo mtoe hapo kwenye list
 
Umekosea diamond kumweka hiyo nafasi in short Diamond ndio SI UNIT wa mziki wa Tanzania ili uonekane bora lazima ufananishwe nae
 
1. Marioo
2. Harmonize
3. Jay Melody
4. Mbosso
5. Jux
6. Chino
7. D. Platnumz
8. Zuchu
9. Alikiba
10. Nandy

Hizo takwimu ni kutokana na performance zao huku mtaani ndani ya miaka mitano ya hivi karibuni kulingana na mtazamo wangu.

Nipe List yako
Huo ni mtiririko kwa mujibu wa ubora au,ili nijue huu ugomvi ni mkubwa kiasi gani. Naona kuna wahuni unawatafuta ugomvi.
 
Da maisha yanikwenda kasi,mziki kusikiliza labda nikutano nao bar.
 
Mkuu ebu fungua code hapo kwa MJOMBA NCHUMALI, nimetoka kapa ujueπŸ˜…
 
List yangu kwa mtazamo wangu;

1.Diamond Platinum
2.Harmonize
3.Jay Melody
4.Mbosso
5.Zuchu
6.Marioo
7.Ali kiba
8.Lava Lava
9.Rayvanny
10.Ibrah Nation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…