Lisu atarudisha itikadi/Imani ya watu kwa CHADEMA. CHADEMA mpeni uenyekiti.

Lisu atarudisha itikadi/Imani ya watu kwa CHADEMA. CHADEMA mpeni uenyekiti.

LISU ATARUDISHA ITIKADI/IMANI YA WATU KWA CHADEMA. CHADEMA MPENI UENYEKITI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Watanzania ni watu ambao huwaamini kama wanaweza kuishi bila kuonewa. Bila kutetemekea watawala. Bila kuwa machawa wa wenye navyo.

Watanzania wengi huamini kuonewa, kudhulumiwa na Wakubwa ni HAKI yao.
Watanzania wengi wamejenga kasumba kuwa ukiwa na cheo unahaki ya kufanya chochote kwa wasionavyo.

Watanzania wengi ni conservative au tuseme wamedumaa na hawahitaji mabadiliko mazuri zaidi.

Watanzania wengi hawamaani katika utu, HAKI, ndio maana hawawezi kupigania HAKI Zao hata kwa kusema tuu.

Watanzania ndio watu pekee ambao hata wewe hapo unaweza jifanya Usalama wa taifa ukaenda kijiwe chochote ukamchukua mtu yeyote au ukampiga makofi mtu kwa kisingizio cha Usalama wa taifa na Watanzania wakakuangalia tuu

Watanzania wengi ndio watu pekee ambao unaweza kuwaweka benchi wakasugua wakisubiri huduma ya hospital au huduma yoyote na wasiwe kuhoji.

Tundu Antipas Lisu tunamhitaji kwa wakati huu ili kubusti akili za Watanzania. Kuamsha Ari.
Kung'arisha fikra,
Kuchochea Moyo wa kupenda haki na kuipigania.

Kuufanya ukweli uwe mwamvuli wa wananchi.

Kuondoa uchawa na Tabia mbaya za kujipendekeza.
Moja ya dalili ya ukosefu wa HAKI katika jamii ni uchawa na kujipendekeza.
Uchawa na HAKI havikai pamoja.
Uchawa na ukweli havikai pamoja.

Mtu yeyote anayejitambulisha na kujionyesha. kama Chawa hawezi kuwa mtenda HAKI.

LISU atarejesha imani ya watu kwenye vyama vya upinzani. Kama ilivyokuwa 2010-2015.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Dar es salaam
Umesema ukweli ndo maana alipozuiwa na polisi akienda mlandizi kwenye kampeni aliwambia polisi atalala hapohapo barabarani.Ndo maana walipozuia meli kule ukerewe akapanda boti na kampeni zikaendelea.Hii haina maana mbowe hafai;tungependa mtu asiyechezewa chezewa kama Tundu
 
Lissu anafaa tu kuwa chini ya mtu mwenye busara zaidi na huyo ni Mbowe.
 
Umesema ukweli ndo maana alipozuiwa na polisi akienda mlandizi kwenye kampeni aliwambia polisi atalala hapohapo barabarani.Ndo maana walipozuia meli kule ukerewe akapanda boti na kampeni zikaendelea.Hii haina maana mbowe hafai;tungependa mtu asiyechezewa chezewa kama Tundu

LISU ni Yakobo anajua kung'ang'ana
 
Mkuu mbona upinzani bado una watu makini ambao wana uwezo wa kuwa kugombea urais mathalan Heche, wenje na kadhalika.
Mtu yeyote anayekidhi sifa na vigezo, anaweza kugombea urais, issue ni jee ni presidential material?.

Moja ya sifa muhimu za presidential material ni statesmanship, ndani ya Chadema Mbowe ndio ana statesmanship, TL na Heche, hawana statesmanship, ni kama ma holigan fulani hivi!.

P
 
Haahaa m

Huwezi kuitakia mema chadema kwa kuendeleza ukagame, huo ni unafiki, siku ccm ikiondoa ukomo uongozi wa nchi mtaanza kulialia
Lissu akishinda chadema inakufa maana yeye atakuwa mapumziko ubelgiji na mke wake mzungu
 
Kama kuna mambo yakielezwa kwa wananchi ni maovu kiasi kwamba watu wanajawa na chuki dhidi ya chama tawala unataka yafichwe wananchi wasiyafahamu ili wasijawe na chuki dhidi ya CCM?
Hapana yaelezwe, ila nachozungumzia ni kwamba kama chama cha siasa hatoshi kuishia kuwa mzungumzaji mzuri wa kuelezea maovu na mapungufu ya chama tawala tu bali onesha kuwa wewe ndio unafaa kuwa mbadala wa hiko chama tawala.
 
Usemi Mzuri Sana.
Upinzani unatakiwa kuwa Jicho linaloona si mabaya tu bali na mazuri.
Kuwa mpinzani wa kisiasa isimaanishe uegemezi wa upande mmoja upande wa mabaya pekee kuangusha upande wa mazuri isiwe lengo.
Ingekuwa Bora kama wapinzani wangekuwa wanatoa tafsiri Zote za mabaya na Mazuri ili kuwawia urahisi wao kueleweka na wananchi.
Ingependeza Sana.
 
Back
Top Bottom