Haa😄😄haa...
Wewe
MamaSamia2025 uko serious kweli...?
Mmemnanga sana Freeman Mbowe kuwa mng'ang'ania madaraka...
Wengine wakasema CHADEMA hakuna succession plan ktk mfumo wa uongozi wao...
Leo Freeman Mbowe anataka kumwachia Tundu Lissu, wewe ukiwa unawakilisha Chawa na wana CCM wenzako unaonesha kumpenda na kumhurumia tena? Really...?
Hakuna shaka kuwa kelele za Chawa wa CCM na allies wao waliomo ndani ya CHADEMA kwenyewe, the whole plan ilikuwa ni ku - frustrate Freeman Mbowe, ajione hafai, wanachama wamwone hafai, mla ruzuku za chama tu, aondoke kisha CCM na serikali yake waweke pandikizi na iwe mwanzo wa kudhoofika kisha kufa au kulala kwa CHADEMA....
The plan has failed spectacularly. Tundu Lissu ndiye Mwenyekiti wa CHADEMA....
Kuibuka kwa Tundu Lissu (ambaye obvious atashinda uenyekiti akigombea na yeyote hata kama Samia atahamia CHADEMA na kugombea naye), hili limewashitua CCM kwa sababu huyu mtu ni moto zaidi kuliko Freeman Mbowe...
Kila la kheri CHADEMA na kila la kheri Tundu Lissu. Tunakujua wewe ni mtu makini, mwenye msimamo usiyeyumbishwa, mpenda haki, mchukia rushwa na ufisadi, mwadilifu na mtu mwenye ufahamu na maarifa mengi sana ambayo ni silaha muhimu sana ktk ulimwengu wa uovu na uonevu huu tuishio...