Yeah
Asilimia kubwa ya taarifa mbaya, (bad publicity) ya usalama wa boda ipo kwenye ujinga na upumbavu wa waendeshaji. Kutovaa gear kiusahihi.
Lakini pia tena kuna shida ya vyombo vyetu vya viwango. Hivii anayepitisha ubora wa kofia ngumu (ile helmet) huwa amefumba macho? TBS mpo wapi.?
Siku nimepakizwa na boda helment yake ikadondoka kwa upepo. Kumuuliza alikuwa hajafunga kimkanda? Kasema amefunga na eti kamekatika kwa upepo! Upepo kweli imagine?
Helment yangu ya sifuri pia ilikatika kale ka strap yaani out of normal use! Hata sio ajali. Nayo niliichukua tu emergency kabla sijanunua helment yangu ya kwanza.
Swali kwa TBS, ile kofia ngumu inapitishwaje kama haijakidhi? Kamba hukatikia pabovu. Msiruhusu ubovu kwenye kitu kinachojinasibu kama 'mimi ni kofia ngumu ya usalama'
Ndio maana maafisa usafirishaji wenyewe wanalalamika kwamba kuvaa helment ni usumbufu tu, kwanza kwenye ajali yenyewe ndiyo inaanzaga kuchomoka. Sa ndo nini.
Anyway kwa mleta mada
Travellerman Pikipiki haina mambo ya kuumiza kichwa kuhusu fuel consumption, kuwa na amani kabisa kwa kipengele hicho.