Mi nimewahi miliki pikipiki mbili tu, KTM cc390 na CBR cc650. Nilipewa maangalizo mawili makubwa Wekeza Sana kwenye Usalama wako (Safety Gears) na kua na heshima sana barabarani.
Usichukulie poa.
Unakuta mtu anaendesha pikipiki na sendo. Aisee. Ukiangimuka unapoteza vidole vyote.
Bila kofia ngumu. Au anavaa kofia ya elfu 15 sijui zile unapewa bure ukinunua pikipiki. Siwasemi ila hamna kitu pale.
Unaendesha na vest, shati, bila koti.
Etc etc etc
Wekeza sana kwenye safety gear, kuan na heshima usiendeshe kama una haraka umeacha familia umeenda kutafuta ugali wanataka jioni urudi sio wao waje hospital kukuona.