Offshore Seamen
JF-Expert Member
- Mar 9, 2018
- 5,489
- 14,091
Nilipita pale nikakuta Bodaboda zimejaa, wakasema kuna jamaa kapata ajaliJana maeneo ya puma headquarters ( kama unatokea port geti namba 3 kuelekea kamata).
Kuna jamaa kamwaga ubongo pale, alikua na SUZUKI 1200 cc, three pipes. Alikua akitokea ile njia ya bandarini kuelekea town, sasa maeneo yale kuna mkeka safi wa kuvutia lakini kuna kona za kizushi.
Jamaa katokea huko kajiachia kwenye ile barabara, ghafra bin vuu anakutana na sharp corner, bike ikamshinda akaenda chini, kichwa kikapiga kwenye ngema ubongo wote ukamwagika.
Hakuvaa helment zaidi ya miwani tu.