Akiwa live kupitia line ya simu katika East Africa Radio mtia nia wa kugombea urais kupitia CHADEMA, Mayrose Majinge amesema yeye amejiunga Chadema toka mwaka 2013 hivyo sio mgeni ndani ya CHADEMA.
Pia ameahidi kuleta siasa safi na maendeleo makubwa ndani ya nchini.
Akijibu swali la mtangazaji la kwanini anaonekana anataka kugombea urais kupitia CHADEMA na huku hawajui viongozi wa Chadema je atapangaje baraza la mawaziri? Mayrose Majinge amejibu kuwa yeye hana muda wa kuclaim viongozi wa Chadema na urais ni taasisi hivyo baraza la mawaziri hilo litapangwa na taasisi ya urais na sio yeye peke yake.
Mambo yamepamba moto.