Live from Hyatt Regency: Mkutano wa Waziri Prof. Kitila Mkumbo, TIC na EPZA na Wahariri wa Jukwaa la Wahariri, (TEF)

Live from Hyatt Regency: Mkutano wa Waziri Prof. Kitila Mkumbo, TIC na EPZA na Wahariri wa Jukwaa la Wahariri, (TEF)

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Niko hapa Hyatt Regency, zamani Kilimanjaro Kempiski, kuwaletea mkutano wa Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo na Wahariri wa Jukwaa la Wahariri.
Ratiba Kili Kempiski.jpg

View: https://www.youtube.com/live/WFUYWRfpEMo?si=IndxqjQLpwOEv19tKaribuni.
OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAENDELEO YA UWEKEZAJI NA MABORESHO YA MAZINGIRA YA BIASHARA KWA
MWAKA 2024 NA MWELEKEO KWA MWAKA 2025
Dar es Salaam, Ijumaa 10 Januari, 2025
1. Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilipoingia
madarakani, pamoja na mambo mengine, ilidhamiria kukuza uwekezaji na
kuboresha mazingira ya biashara kama sehemu ya mikakati muhimu ya
kuchochea ukuaji wa uchumi nchini. Katika taarifa hii tunaeleza kwa muhtsari
maendeleo ya sekta ya uwekezaji kwa mwaka 2024 na mwelekeo kwa mwaka
2025.
2. Mafanikio katika sekta ya uwekezaji hupimwa kwa kuzingatia vigezo vikubwa
vitatu. Vigezo hivi ni idadi ya miradi ya uwekezaji iliyosajiliwa, idadi ya
ajira zilizozalishwa kupitia miradi iliyosajiliwa, na mtaji uliovutiwa
kutokana na miradi hiyo. Majukumu ya kuhamasisha, kuwezesha na
kuratibu utekelezaji wa miradi ya uwekezaji nchini husimamiwa na kuratibiwa
na taasisi mbili za umma: Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya
Kusimamia Uzalishaji wa Bidhaa kwa Ajili ya Mauzo Nje ya Nchi (EPZA).
3. Katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2024, Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC) kilisajili jumla ya miradi 901, ukilinganisha na miradi 526 iliyosajiliwa
katika kipindi kama hicho mwaka 2023. Hii ni sawa na ongezeko la asilimia
71.3 la miradi iliyosajiliwa katika kipindi cha mwaka mmoja.

Miradi iliyosajiliwa mwaka jana (2024) inatarajiwa kuzalisha ajira 212,293
ukilinganisha na ajira 137,010 zilizozalishwa na miradi ya uwekezaji katika
kipindi kama hicho mwaka 2023. Aidha, miradi hii imeweza kuvutia mtaji wa
dola za kimarekani bilioni 9.31, ukilinganisha na mtaji wa dola za Kimarekani
bilioni 5.72 iliyotokana na miradi ya uwekezaji kupitia TIC katika kipindi cha
Januari – Disemba 2023.
5. Mikoa mitano inayoongoza kwa kusajili miradi ya uwekezaji nchini ni Dar es
Salaam (356), Pwani (166), Arusha (64), na Dodoma (47), ambapo asilimia
70.3 (miradi 633) ilisajiliwa katika mikoa hii.
6. Sekta tano zinazoongoza kwa kusajili miradi mingi ya uwekezaji ni uzalishaji
viwandani (miradi 377, 41.8%), usafirishaji (miradi 138, 15.3%), ujenzi wa
majengo ya biashara (miradi 91, 10.1%), utalii (miradi 76, 8.4%), na kilimo
(66, 7.3%). Miradi katika sekta hizi kwa pamoja zilivutia jumla ya mtaji wa dola
za Kimarekani bilioni 6.071, sawa na asilimia 65.2 ya mtaji wote uliopatikana
kwa mwaka 2024.
7. Mwaka 2024 tunaweza kuutangaza kuwa mwaka bora zaidi katika sekta ya
uwekezaji Tanzania kutokana na ukweli kwamba ndio mwaka ambao TIC
ilisajili miradi mingi zaidi ya uwekezaji (miradi 901) tangu Tanzania ianzishe
kituo hiki na kuanza kurekodi miradi ya uwekezaji kama inavyooneshwa katika
umbo la hapa nchini. Hii inavunja rekodi ya miradi 885 ya mwaka 2013.
Umbo: Idadi ya Miradi Iliyosajiliwa Katika Kituo cha Uwekezaji 1996-2024
Hadi kufikia Disemba 2024, TIC ina miradi 13,282 ya uwekezaji iliyosajiliwa
na kutekelezwa nchini, ikivutia mitaji kiasi cha dola za kimarekani 127,176
milioni na kutoa ajira zaidi ta 1.98 milioni.
9. Mafanikio katika sekta ya uwekezaji yamechochewa na sababu mbalimbali
kama ifuatavyo:
i) Kuendelea kumiarisha mifumo ya kisera na sheria katika
kuwezesha na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini
ii) Maono, hamasa na ushawishi ambao umeendelea kufanywa na
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, kwa makampuni mbalimbali ya kimataifa
kuja kuwekeza nchini kupitia ziara na mikutano mbalimbali aliyoifanya
nje na ndani ya nchi
iii) Kampeni kubwa ya kitaifa ya kuhamasishaji uwekezaji nchini
iliyofanyika mwaka jana kwa ushirikiano mkubwa katika ya TIC,
chemba za biashara nchini (TCCIA, TWCC), Mabenki, na vyombo
vya habari. Jumla ya wafanyabiashara 1,800 walifikiwa kupitia
kampeni hii katika mikoa 26 ya Tanzania Bara
iv) Kuendelea kuimarisha na kuboresha huduma kwa wawekezaji
katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ambapo sasa kuna taasisi
16 zinazotoa huduma katika kituo cha pamoja
v) Kuanzishwa kwa ofisi mpya ya Kanda ya Kaskazini mkoani Arusha
vi) Viongozi katika sekretariati za mikoa na mamlaka za serikali za
mitaa, hususan wakuu wa mikoa, kuendelea kuhamasisha
shughuli za uchumi na uwekezaji katika maeneo yao
10. Katika kuendelea kuimarisha sekta ya uwekezaji nchini na kuendelea
kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini, Serikali kwa mwaka
2025 itachukua hatua zifuatazo:

Kutunga Muswada wa Sheria Mpya ya Uwekezaji Tanzania. Pamoja
na mambo mengine, muswada huu unapendekeza kuunganisha
taasisi za TIC na EPZA. Muswada huu uliwasilishwa Bungeni mwaka
2024 na sasa upo katika ngazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge kwa
ajili ya kufanyiwa kazi.
ii) Kuandaa awamu ya pili ya Mpango wa Kuboresha Mazingira ya
Biashara na Uwekezaji (MKUMBI). Hii ni baada ya kufanya tathmini
ya utekelezaji wa MKUMBI I uliobaini mafanikio mbalimbali katika
kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Aidha,tathmini hii
ilibaini changamoto mpya zilizojitokeza ambazo serikali na wadau
wanaendelea kuzifanyia kazi. Lengo ni kuifanya Tanzania kuwa moja
ya nchi zenye mazingira bora ya kufanya biashara na uwekezaji barani
Afrika.
iii) Kuanzisha utaratibu wa kuzipima mamlaka za serikali za mitaa
katika kuboresha mazingira ya biashara na kuhamasisha na
kuwezesha uwekezaji
iv) Kuanza kutekeleza ujenzi wa miundombinu katika maeneo maalum
ya kiuchumi ikiwemo la Bagamoyo (Bagamoyo Special Economic
Zone) ili kuwezesha ujenzi wa viwanda.
v) Kushirikiana na watanzania waishio nje ya nchi (diaspora)
kuanzisha utaratibu wa kuhamasisha uwekezaji kwa kuzingatia
taratibu zitakazowekwa na TIC kwa kushirikiana na mamlaka zingine za
serikali
vi) Kwa mwaka 2025, tumejiwekea lengo la kuvutia miradi MIPYA 1,500
ya uwekezaji na mitaji ya dola za kimarekani 15 bilioni ifikapo
Disemba 2025 ($15 billion). Sekta mahsusi ni viwanda, kilimo,
uchukuzi, nishati safi, utalii, madini na huduma (service sector)
Ongezeko hili litaifanya Tanzania kuwa moja ya nchi 5 bora katika
uwekezaji barani Afrika hasa kwa wingi wa mitaji. Kwa utoaji wa
huduma, Tanzania ni moja ya nchi bora kwa uwekezaji hata sasa.

Tutaendelea kuhamasisha uwekezaji wa ndani tukiwa na lengo la
kufikisha 50% ya miradi yote ya uwekezaji kwa mwaka imilikiwe na
watanzania. Tutashirikiana na taasisi mbalimbali za serikali kuwalenga
wawekezaji wa ndani hasa wawekezaji wadogo wanaokua.
viii) Kuboresha na kuwezesha ofisi za Sekretariat za Mikoa katika
kuhudumia na kuboresha mazingira ya uwekezaji katika ngazi na
Mikoa na Wilaya nchini kote. Kwa mwaka 2025, tutaanza na
kufungua ofisi ya Kanda ya TIC mkoani Njombe ili kusogeza
huduma za uwekezaji mkoani Njombe, Iringa na Ruvuma.
Imetolewa na:
Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb.),
WAZIRI WA NCHI,
OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI.
Dar Es Salaam, ijumaa 10 Disemba, 2025
Kwa mawasiliano na taarifa zaidi:
Raymond Mtani,
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji,
S.L.P 104,
DODOMA.
Simu: +255 (0) 767074991
Email: raymond.mtani@planninginvestment.go.tz

Paskali
 

Attachments

TIC imesajili miradi zaidi ya miradi 900!, imezalisha ajira zaidi ya laki mbili, imevutia miradi ya dola zaidi ya bilioni 9!. -Prof. Kitila.
P.
 
Mafanikia sekta ya uwekezaji yamechangiwa na
1. Maboresho ya Mazingira uwekezaji ya kisheria na kisera.
P
 
2. Rais Samia, kuhamasisha, biashara ya uwekezaji kupitia ziara mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
P
 
Kuzipima Mamlaka za serikali za mtaa jinsi zinavyoboresha mazingira ya biashara.
P
 
Kuendelea kuhamasisha uwekezaji wa ndani, ili angalau Watanzania wamiliki asilimoa 50 ya miradi yote.
P
 
Back
Top Bottom