Live from King Jada Hotel Morocco DSM: Kikao Kazi Msemaji Mkuu wa Serikali, Gersom Msigwa, na Jukwaa la Wahariri, TEF

Live from King Jada Hotel Morocco DSM: Kikao Kazi Msemaji Mkuu wa Serikali, Gersom Msigwa, na Jukwaa la Wahariri, TEF

Wanabodi,

Niko kwenye ukumbi wa hoteli mpya ya King Jada Hotel, nikiwaripotia live, kikao kazi kati ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Gersom Msigwa, na Jukwaa la Wahariri Tanzania , TEF

Karibuni.

Paskali
Hivi huwa anaongea vitu gani hasa huyo Msemaji ?

Kwa umri ambao CCM imekaa madarakani hapa nchini Tanzania, Chama hicho kingekuwa kinafanya Kampeni za Siasa kwa kuonyesha vile vitu vizuri ambavyo tayari vimefanyika na kuonekana machoni mwa watu lakini siyo kuanza kufanya Kampeni za Porojo za maneno ya kuwaahidi Wananchi kwamba Watawafanyia mambo kadhaa wa kadhaa.
Hayo mambo wanayoahidi kwamba Watayatekeleza, Je, walishindwa Nini kuyatekeleza katika kipindi chote kabisa Cha Utawala wao wa zaidi ya miaka 60 hadi Sasa? Kipi hasa kiliwakwamisha kwa miaka mingi yote hiyo???
 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile, anatoa makaribisho rasmi.
Balile amesema huu ni mwaka wa uchaguzi, hivyo media ambayo ni mhimili wa nne, tumemtafuta Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ili tusemezane mawili matatu.

P.
 
Muulize kwa nini TBC inaifanyia kampeni za Siri na wazi CCM.
Pia muulizeni kama Ile live coverage ya birthday ya CCM kama TBC Ililipwa kama Wasafi na Kitenge na Zembwela na genge lao walivyolipwa kuanzia usafiri (hata wa chops) na makazi.
 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile, anatoa makaribisho rasmi.
Balile amesema huu ni mwaka wa uchaguzi, hivyo media ambayo ni mhimili wa nne, tumemtafuta Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ili tusemezane mawili matatu.

P.
Mhimili wa nne kivip? Unamaanisha kwamba huu mhimili unajitegemea kabisa bila kuelekezwa na ule mhimili wenye mizizi mirefu inayofika kwenye bahari?
 
Msigwa, ameanza kwa kutupa salaam kutoka kwa Rais Samia, alipomwambia rais kwa anakuja kukutana na wahariri, Rais Samia, alimwambia Msigwa, nenda kawasikilize na nawahidi, nitawapa kila wanachokitaka.
P
 
Msigwa amesema huu ni mwaka wa uchaguzi, amewaomba wahariri ushirikiano, amewaahidi wahariri yeye atawapa kila aina ya ushirikiano utakao hitajika.
P
 
Atasema Gazeti la mwananchi liliandika vita ya congo yafunga Barbara dar.... Halafu Mzee @Pascalmayalla wanahhabari wengine mtakenua meno kama mafisi maji na kuchekacheka na kuombea radhi mwananchi.... MWAMBIE I AACHE WATU WAFANYE KAZI AISEE ...
 
Msingwa, amemkubuka Adam Mwaibabile "mwana", alimwambia Mdogo wangu Msigwa, ukiona habari una mcheche nayo sana, usikimbilie kuiandika, tulia kidogo, punguza mcheche, ukitulia ndipo iandike huku umetulia.

P
 
Msigwa awataka wakuu wa taasisi wajitokeze, watoe taarifa, Watanzania, wapate haki ya kupokea taarifa.
P
 
Msigwa amesema huu ni mwaka wa uchaguzi, amewaomba wahariri ushirikiano, amewaahidi wahariri yeye atawapa kila aina ya ushirikiano utakao hitajika.
P
ana maana atawapa hela siyo....mwaka wa wahariri kuvuna na kupunguza njaa(siyo kuimaliza maana njaa ni hitaji endelevu la binadamu).
 
Msigwa, ameanza kwa kutupa salaam kutoka kwa Rais Samia, alipomwambia rais kwa anakuja kukutana na wahariri, Rais Samia, alimwambia Msigwa, nenda kawasikilize na nawahidi, nitawapa kila wanachokitaka.
P
Mzanzibar ana maneno matamu huyu. Tunangojea maelezo ya 4R. Au 4R zilikuwa za yeye na kamanda Mbowe tu?
 
Msigwa, ameanza kwa kutupa salaam kutoka kwa Rais Samia, alipomwambia rais kwa anakuja kukutana na wahariri, Rais Samia, alimwambia Msigwa, nenda kawasikilize na nawahidi, nitawapa kila wanachokitaka.
P
Huenda hata Samia hajui alipo Msigwa leo, fear Politicians.
 
Back
Top Bottom