Kiraka
JF-Expert Member
- Feb 1, 2010
- 4,285
- 4,074
Wanabodi,
Niko ndani ya Ukumbi wa NSSF Mafao House, nikiwaletea live ya mkutano wa Jukwaa la Wahariri -TEF na Mfuko wa Pensheni NSSF.
Mfuko wa NSSF umetisha!, sasa una thamani ya zaidi Shilingi Trilioni 8.5 ndani ya kipindi kifupi, na uendelevu wake, sustainability ni 90%!, hili sio jambo la kawaida!, ni NSSF Inatisha!.
Karibuni uandamane nami.
Paskali
Nini kipya wamefanya kupata mafanikio hayo? Au ndio hadithi za kipigaji.. tunaomba maelezo ya kina kwamba walikuwa hapa 4-5 years ago, wamefanya nini na nini mpaka kufikia hapo?
Vipi ugawaji mafao? miradi chechefu imefikia wapi? Madeni ya taasisi na serikali yamelipwa kwa kiasi gani na yamefikia wapi? from 4-5 years ago, na nani na nani ni wadaiwa wakubwa?
Isije ikawa ni vikao vya kuwaita waandishi , wahariri wakapewa bahasha ili waandike vizuri, mama afurahie, upigaji uendelee.
Kama mwandisi makini, usipojali bahasha, hayo ndio aina ya maswali na majibu utahitaji, kabla ya kuwapongeza kwa kusema NSSF Inatisha.