Baada ya muda mrwfu kuwa sitizami game za stars, leo nimetizama timu yangu ya taifa..
Nilichojifunza..
Mosi, si kweli kuwa samata hajitumi national team, jamaa anaipenda timu yake uchawi anaocheza nao, tizama kipindi cha pili kwanza alicheza kama winga wa kushoto, jitihada zake na mchango wake alionekana kama amejitolea sababu mipira mingi ilikuwa inamfikia, ila kipindi cha pili baada yya sub akaenda kucheza CF, mipira haimfikii, akawa anaonekana hana analolifanya uwanjani(huyu ndio samatta anaelalamikiwa na wa tz)
Pili, safu yetu ya viungo bado, kwa game ya leo wangekuwa na mipango mizuri, (akili yaa kushambulia) tungepata zaidi na wao wasingepata, mudathir na mzamiru wana matatizo ya kupoteza mipira, wanapiga pasi nyingi fyongo, na hata ambazo ni sahihi zinakuwa hazina madhara wakati ambao inahitajika pasi yenye madhara.
Tatu.. Kibabage hazina ya baadae, fei toto afanye michakato asoge mbele yule lusajo anaweza luwa striker mzuri kuna vitu anapungukiwa, huyu dismas hazina ya baadae.. Taifa kama taifa hatuna kiungo mshambuliaji maridhawa.