Pia baada ya kupiga kura nimeenda kazini kwangu, ambako pia kuna kituo, jambo la kushangaza ni kuwa kituoni hapo mabox yote ni ya rangi nyeupe(mifuniko), na sijui discrepancy hiyo inaelezwaje!(sijanote utofautishaji wowote), na nilipouliza wakasema kuwa yameletwa yakiwa hivyohivyo, huenda ndio ukosefu wa vifaa wenyewe..nahofia sana kura hizo kuharibika, maana zitachukuliwa kuwa zote ni za Mbunge, kumbe zingine ni za Rais!
Vijana this time wameushangaza Uma, ni wengi sana tofauti na ilivyotegemewa
Ni kweli NDU, mimi nimewakuta vijana wengi sana tofauti na 2005. Nimeshuhudia akina dada wawili wakiwapigia wenzao mbalimbali wakiwahimiza waamke kuja kupiga kura. Watu wako gado.
Sabalkheri wana jf wenzangu. Mwenzenu tayari niko mstarini nikisubiri kwenda kufanya kweli. Kuna nyomi la kufa mtu huku. Im super dupa excited
dw swahili wamesema kuwa kuanzia saa kumi askari atatakiwa kusimama nyuma ya mtu wa mwisho na watakaokuja baada ya hapo hawataruhusiwa kupiga kura.so wakuu shime tuwahi kufika vituoni kabla ya saa kumi ( habari kutoka visiwani)

Chalinze Pwani hali inaripotiwa kuwa ni tulivu sana. Shule ya msingi Msoga ndipo JK atapiga kura yake.
Hiyo ni kwa sheria gani Mkuu. Maana mwisho wa kufunga kituo ni saa 12 jioni.