Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Nimewapigia simu girlfriends wangu wa zamani (usiulize kwa nini bado nina namba zao). Cha kushangaza, wote walikuwa wamepanga kumpigia kura JK. Cha kujivunia, wote sasa nimewashawishi wampigie kura Dr. Slaa....na wameahidi kufanya hivyo...for the old time's sake.

Japo mimi sintoweza kupiga kura, najivunia kwa kuingiza kura mpya kadhaa kwenye kampi ya upinzani!
 
Chalinze Pwani hali inaripotiwa kuwa ni tulivu sana. Shule ya msingi Msoga ndipo JK atapiga kura yake.

naona keshapiga, maana hapa ubungo kuna msafara unatokea huko njia ya morogoro nahisi ni wake mkwere
 
Kuna ile habari kwamba NEC imeahirisha uchaguzi kwenye majmbo matatu. Hii maana yake nini - kwamba matokeo ya URAIS hayatotangazwa mpaka uchaguzi ufanyike kwenye majimbo hayo?
 
Hi guys. For those who have not voted yet plz do it. And vote for change.
 
JK anahojiwa baada ya kupiga kura anaulizwa matarajio ya chama chake ni nini anajibu ni Ushindi tu.

Anaulizwa juu ya muundo wa serikali yake utakuaje anasema sasa hivi ni uchaguzi.

Hali ya usalama wa nchi anasema ni nzuri.

Ushindani anasema ulikuwa mzuri. Lakini ni ushindi tu. Ameng'aka kuwa mbona hilo swali kaulizwa mara nyingi, anasisitiza ni ushindi tu.

Kura anasema amejipigia mwenyewe tu.
 
JK Anahojiwa anasema Hawawezi Kushindwa, anasema wamefanya mambo mengi sana katika miaka mitano na Mwisho anawaomba Watanzania Waipigie kura CCM! Mh Naona anaendeleza Kampeni live Star TV
 
Hawa Waandishi ni Wajinga sana, Hivi Tume inaruhusu Kampeni wazi wazi hivi halafu Kiravu atakenua
 
Salma Kikwete anadai Wanawake wafanye kama vile alivyowashawishi kufanya.

Anaamini kuwa CCM itapata ushindi mkubwa.

Anatoa mwito kwa akina mama wajitokeze.

Anasema kiongozi pekee anayefaa ni JK.
 
Jk anasema watu Million 19 ni ongezeko la kawaida na imani yake ni kuwa watu wajitokeze.
 
JK anawaomba wapige kura kwa amani na wapokee matokeo kwa amani na baada ya uchaguzi warudi katika maisha yao ya kawaida.
 
JK anasisitiza lazima mawakala wawe makini.

Kuhusu vyuo kutofunguliwa anasema yeye hapangi ratiba. Waulizwe wahusika vyuo vikuu.
 
Back
Top Bottom