Anasema ushindi ni baada ya dakika 90 na kama kanuni zimefuatwa. Kama atashindwa kwa nafasi yake kama katibu Mkuu wa CHADEMA bado atawatumikia wananchi.
Sasa hivi kama katibu Mkuu hana la kusema kwa kuwa kuna Kaimu katibu Mkuu lakini kama mgombea wa Urais anapata taarifa kutoka Nchi nzima na anapata taarifa za utata mbalimbali zinamfikia.
Kamishna Msaidizi "LUCAS ndo amemaliza kuhojiwa na Gabriel na kwamba amesema hili tukio ni la kipekee sana, hivyo watalifanyia kazi!!! hawa sio sisiemu kweli
ITV: Mbatia anahojiwa na anadai kuwa hali ni tete. watu hawaoni majina yao vituoni lakini yako vituo vingine. Wengine majina yao hayapo lakini wakienda ndani majina yao yapo.
Huko Magomeni nako mgombea udiwani amkwida mpambe wake. anaripoti Elisha hapa TBC na kwamba sasa wamepelekwa ostabei polisi!!! jamani huko kwingine wanasemaje???
Mbatia anadai hadi sasa hajapiga kura. Ana kadi lakini jina lake halipo na alipoonyeshwa kituo jina lake halipo. Msimamizi wa Kituo haonekani. Anasema amenyimwa haki yake ya kupiga kura.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.