Live kutoka kuzimu!

POLE SANA UNAMSIKILIZA HUYO TAPELI NA ANAKUAMINISHA UWONGO KIASI HICHO?SOMA BIBLIA WAFU WAKO MAKABURINI WANASUBIRI UFUFUO.
Huu ndio ukweli,kumuita tapeli nashindwa,ila huyo mtu anafanya kama yeye tu ndio anajua vitu sahihi,hafundishiki.
 
We jamaa jau hapo ndo ulipozingua sasa kwahiyo chumvi uchawi duh... anyway kwa mafundisho uliyoyasema ukisearch hell in Buddhism youtube utakutana nacho ulichokiongelea hicho.
 
Jamaa anazingua baadhi ya sehemu hasa hiyo ya chumvi dah, pia hell according to Buddhism ndo kama alichoongelea jamaa huyo YouTube vipo vyote hivyo ila yeye the way anavyowasilisha.. dah
 
Kwa hiyo rasta zimebuniwa kuzimu si ndio, na hiyo smart phone unayotumia kuleta hili bandiko imebuniwa wapi, kitu kingine natumaini huwa unatumia kioo, je asili unaijua vile kilipotoka?. kingine vipi na wale mababu zetu walikuwa wanavaa magome ya miti kwa hiyo nao wanaenda kuzimu au... bro kuna sehemu unajichanganya
 
Wala usiendelee, umeandika pumba mwanzo mwisho.
 
Upotevu uliopo apa ni upi? Yeye anatuhasa tuache dhambi ili tusikutane na moto, kuhusu hayo aliyoyaona siyo mageni masikioni mwetu.. Pia kuhusu kutafasiri maandiko aonavyo yeye, hajatoka nje ya msitari yupo palepale katika kweli. Kwamba tumkiri YESU ili tufanyike kuwa wana na warithi pamoja nae The Spirit of Tanzania
 

“Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.” Mhubiri 12:7

“Walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote linalofanyika chini ya jua.” “Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu (kaburini) uendako wewe.” Mhubiri 9:5,6,10.

Ufufuko ni Illogical kama kweli mtu akifa anaenda mbinguni au kuzimu.

Pia shetani ndio mtu wa kwanza kudanganya kuhusu kifo katika kitabi cha mwanzo alipokwambia hawa kuwa ukila hilo tunda hakika hutokufa.

Hayo mambo ya kuabudu wafu ni upotovu na ni ibada ya kishetani. Hapa shetani ameteka watu sababu anajua watu wanakuwa na uchungu sana na watu wao waliokufa, utaletewa mpaka ndoto za watu wako waliokufa if you fall for this trap unamwabudu shetani.

Yapo mafungu mengi yanayozungumzia nadharia ya kifo nimeleta tu machache.
 
Tafuta namna nyingine ya kuwausia watu waache dhambi hiki ulichoandika hapa unapotosha, sana na hakika tofauti na mawaidha ya wale ndugu zetu waislamu kuhusu kifo.
 
Amin ,usijali washinde Kwa neno,hiyo ndo kazi waliotumwa huku wakinuiza roho za kupuuza na kufanya iyonekane hadithi. Wajibu jibu moja
"Toka mbele yangu shetani"
Pamoja na yote Mungu atusaidie tukaurithi ufalme
 
Mkuu naomba kuuliza, pale yesu aliposema "waacheni watoto wadogo waje kwangu ......,"' unaeza kuwa na uelewa juu ya kauli hii, yani kwanini hakusema '"waleteni watoto wadogo kwangu ...."? Kwako Mtumishi Rabbon
Waacheni watoto WADOGO waje kwangu, msiwazuie maana watoto WADOGO kama Hawa, ufalme wa Mungu ni wao.

Kuwaacha watoto wamfuate Yesu ni kuwaelekeza waende Kanisani, ni kuwafundisha neno la Mungu.

Ni kuwazuia wasiangalie picha mbaya ambazo zitawafanya wawe wahalifu.

Ni kuwa
 
mkuu hapa kuna masomo mengine, naomba uitazame koment yako hii kisha uyaandae, na kama yapo naomba un-tag huko tafadhl


Ntafafanua Kwa uchache.

Mungu amekataza IBADA za sanamu,nazo hizo ni kama ifuatavyo:

1. Kusherehekea X-Mass tarehe 25december.

IBADA hiyo unaweza Sema ni ya Mungu lakini walioset tarehe hiyo ni ya kishetani kabisa na IBADA hiyo haabudiwi Yesu halisi. Mungu amekataza.

2. Kuwasha mishumaa makaburini.

Kuwasha mishumaa ni sawa tu na mioto mingine ya kichawi, wanga huonekana wamebeba mioto, pia ni sawa tu na Mila za kukanyaga mafiga, au kumpitisha mtoto mchanga katika moto.. Ni uchawi kabisa, hivyo ikiwa umeokoka epuka kushiriki kuwasha mishumaa makaburini.

3. Kusherehekea siku ya Kuzaliwa.

Kutunza kumbukumbu ya lini ulizaliwa Si shida, lakini kusherehekea siku hiyo ni kujiunga na miungu inayopokea IBADA hiyo pasi wewe kujua, hivyo Kwa kufanya hivyo unamkasirisha Mungu maana imeandikwa Umwabudu Mungu pekee.

4. Kuchukua au kugawana nguo za marehemu/ Mikoba nk nk.

Zipo kabila, usipochukua nguzo za marehemu kwenye kikao Cha ukoo unatengwa na kulaaniwa, ikiwa unapenda uende Mbinguni ukifa, kataa, jitenge kabisa.

Nguo ni Zina NAFSI ndani yake, Elisha alichukua joho la Elia na kulitumia kufanya Muujiza,

Likewise kupewa nguo ya marehemu asiyeokoka ni kuchukua NAFSI TABIA na mashetani yaliyokuwa ndani yake na kuyahamishia kwako.

Jitenge na mambo hayo ikiwa unatamani kuona Mbingu.

5. Kuhudhuria Makusanyiko au sherehe za kikabila.

Yapo makabila hukutana Kila mwisho wa mwaka na kusherehekea, familia au ukoo.

Watu wa kaskazini hiyo imefana na kuzoeleka sana,

Ile ni IBADA ya Mizimu, Kuna pombe Huwa inaenda kumwagwa katika kaburi la ukoo, maana yake ni kupeleka IBADA Kwa mashetani na Mizimu ya ukoo Ili kupata ulinzi na baraka za kipepo.

Kila kabila na Mila yake. Aliyeokoka lazima ujitenge nao, uwe adui wa ndugu zako Ili uwe Rafiki wa Yesu na Mbingu, la utatupwa kuzimu.

6. Kurithi Majina, au kurithisha watoto Majina.

Wengi wanapitia taabu maishani sababu ya Majina waliyopewa.

Umpa Jina mtoto la mama au shangazi ,ikiwa mtu huyo ni mchawi, Roho ya yule mchawi na mapepo yake yatahania Kwa mtoto direct.

Ikiwa umeokoka, Nenda Kwa watumishi wa Mungu uombe ushauri Jina Gani umpe mwanao kumpa future nzuri.

Ukiogopa uadui na mzazi wako Kwa kutomwita mwanao Jina ambalo unajua mtu huyo anaabudu miungu au ni mshirikina ni Kwa HASARA Yako.

Upinzani unaouona dhidi yangu unatokana na kusema Kweli yote ambao huamsha hasira ya shetani.

Endelea kusoma " Live Kutoka KUZIMU" utapata mengi usoyajua yatakayokusaidia kuepuka kutupwa KUZIMU ya moto Kwa kutojua.

Aamen
 
Are you mad?

https://jamii.app/JFUserGuide off
 
Mkuu amka Acha hallucination...Ni mbaya sana kwa afya ya ubongo wako
 
Njia ya Mbinguni ni nyembamba sana.

Mababu zako wengi wako kuzimu,

Epuka nilokudokeza na acha dhambi nilizodokeza na utazoendelea kuzisoma Ili usiwafuate Babu zako kuzimu ya moto.

Amen
 
Ntafurahi kama ntapokea majibu ya maswali haya ma3

1. Huyo ni Mungu yupi anayekasirika kusherehekea birthday?

2. Mungu wako anaitwa nani?

3. Unaweza fafanua vizuri hyo namba 3!!?
 
Ntafurahi kama ntapokea majibu ya maswali haya ma3

1. Huyo ni Mungu yupi anayekasirika kusherehekea birthday?

2. Mungu wako anaitwa nani?

3. Unaweza fafanua vizuri hyo namba 3!!?
Sitakijibu ewe mwana wa kuzimu,

Tayari umeriport Ili Uzi ufutwe,

Wamesoma wengi tayari na watapata msaada.

Amen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…