Bible inasema Mungu Ni Moto ulao, kuamini tu kwamba Yesu alikufa kwaajili ya dhambi zako hakutoshi kuhepuka hukumu bila kuacha kutenda hizo dhambi.
Yesu alisema si wote wanaomuita bwana wataurithi ufalme wa Mungu. Wewe unadhani hawa aliowataja Yesu hawakuamini Kama unavyoamini? Waliamiani lakini lakini matendo yao hayakumpendeza Mungu.
Ukiendelea na msimamo huu, hata ushoga utaona ni Jambo la kawaida kwa kudhani kinachojitajika Ni kuamini tu kwamba umeokolewa kwa neema. Au wewe unaamini mashoga, wachawi na wazinzi wataurithi ufalme wa Mungu kwa kuamini Yesu amebeba dhambi zao huku wakiendelea na matendo yao???
Dhambi ni asili na sio matendo ya sheria ndugu elewa hilo kwanza kumbuka Adam alianguka dhambini kwa uasi yaani kumtii shetani na kusikiliza kamba zake kumbuka
kufanya matendo mazuri hakumuondolei mtu dhambi kamwe ref Agano la kale Israel walitoa sadaka ya damu kwa kuhani mkuu aliyeipeleka patakatifu kwa pa takatifu kwa ondoleo la dhambi
kwa mwaka mzima soma kumbukumbu la Torati ndugu
katika Agano jipya tunae kuhani mkuu Yesu Kristo aliye toa uhai wake msalabani kwa ondoleo la dhambi milele na akafanya upatanisho kati yetu na Mungu na hilo ni agano la milele na tunapokea wokovu kwa Imani yaani kumkiri Yesu Kristo ndie Yehova tunapewa Haki ya kua wana na si kwa ajili ya matendo yetu mema ila kwa ajili ya alichokifanya Yesu Msalabani
Tatizo lililo kwa wakristo wengi hamkubali kua mlipokea msamaha wa dhambi milele pale mlipozaliwa mara ya pili hivyo mnateswa na kumbukumbu za dhambi zenu
kitu ambacho sio lengo la ukombozi
angalia watu wote Mungu alipowatokea kwanza
aliowapa Haki kuanzia Nuhu,Abram,Musa na Manabii wengine kwanza moja hawakupewa hiyo haki sababu ya matendo yao bali sababu Yeye Mungu ndie mwenye haki na anaitoa kwa mapenzi yake
kumbuka ile haki ilikua kivuli cha atakachokuja kufanya Yesu
kumbuka agano la kale ni kivuli cha agano jipya kila alichokifanya Mungu wakati huo alikua anatoa picha anachokifanya Yesu
sisi leo tuna agano bora kuliko lile la kwanza elewa hivyo
hivyo angalizo angalia kwenye Bible yako maana ya dhambi ndio uje hapa tuongee!