Live kutoka kuzimu!

Unakosea sana kunidhania hivi,mbona niliuliza vema tu ili ufafanue?,hivi badala ya kumueleza mtu akaelewa wewe unaanza kuniita na kuniweka kundi moja na hao wa dini za kuzimu unanikosea heshima yangu.

Binafsi umenikosea sana kuniita hivyo,sio kwamba wewe unajua kila kitu,la hasha kwenye imani ya kweli hawako hivi,unakosea sana.

Wewe unaona makosa ya wengine tu,huoni yako,wewe unaona mawazo ya wengine ni ushetani,hujioni yako,mbona huko kwenye biblia watu waliohojiana bila kuwabambika wenzao majina haya?,

Umekosea sana kunidhania hivyo,nina matumaini ya ufufuo na uzima wa milele katika Yesu Kristo na kamwe simuoni mtu mwingine ni wa kupotea au ana dini ya kuzimu.

Bahati mbaya zaidi kwenye uzi wako umemtangaza shetani kuliko Mungu,na unajiona hukosei na uko sawa tu.
 
"Hauna Jehanam. Ni hadithi zilizotungwa na watu fulani ili kuwatia watu hofu ili wawatawale kirahisi" X
 
Mtu unaulizwa watu tuelimike,halafu unaandika kejeli😁😁
 

Mkuu unachokisema ni sahihi kabisa. Kuzimu ipo na paradiso ipo. Mungu yupo na shetani yupo.

Bahati mbaya upotofu na ukengeufu ni mkubwa sana nyakati hizi za mwisho. Unaona watu wasivyo na hofu na Mungu, wamejaa maarifa ya ki shetani, hawana aibu wala Chembe ya staha hata kwa Mungu wao. Wanajibu kwa kejeli na dharau tu. Kwa kweli ukikosa Neema ya Mungu na Roho Mtakatifu kua nawe umepoteza kila kitu.

Warumi 10:7 au, Ni nani atakayeshuka kwenda kuzimuni? (Yaani, ni kumleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.) mambo Haya yapo kabisa na Biblia imenena wazi wazi.

Mimi natoa mfano mdogo tu wa kuzimu. Kuna Mtu au watu hua wanakufa kwa kupaparika, yaan kutapatapa na hata kufikia kujisaidia haja kubwa na dongo wakati wafapo. Sasa ile hua haiji eti ukaona ni kawaida tu Hapana. Hapo anaona kabisa nafsi yake inakokwenda ni kwenye mateso, kwa hivyo anakua anapambana isiende huko ili irudi na ndipo unaona mtu anapaparika na wengine hadi baada ya kufa unaona na machozi kabisa. Lakini kifo cha Mwenye haki wa Mungu hakina shuruba, masumbufu wala mapambano yeyote.
 
Hossana ! Hossana! ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa Jina la Bwana. nyakati hizi ni za mwisho, na hata zisingekuwa za mwisho, ishini kwa kujiandaa kwasababu mtu hufa katika siku asiyotarajia. hata yule aliyeugua sana anajua hatapona huwa hajui atakufa lini. labda wale wanaojiua wenyewe. kwasababu hatujui siku wala saa, yatupasa kujiweka tayari.
 
umeo
ngea mengi ya ukweli lakini hili la katuni sio kweli,kwani sio kila katuni ni mbaya nyingine zinafundisha watoto,mfano katuni iitwayo kibena hapa tz inafundisha hesabu,,TOM and JERRY ina ubaya gani???? alafu watoto hawajitambui kwambahiki ni kizuri au kibaya sidhani kama MUNGU ni katili ivo,,,,,alaf unasema sisi binadamu tuko chini kabisa alaf inafuata kuzimu ya shetani ambayo inasababisha maombi yetu yasifike,,,ina maana shetani anauwezo wa kukata network isimfikie MUNGU!!!!!!!........................na ndo manake MUNGU ameweka nafasi ya KUTUBU,,,,,,kumbuka biblia takatifu inasema" dhambi zote zinasamehewa isipokuwa dhambi moja tu haisameheki nayo ni" kumkashifu ROHO MTAKATIFU".......na na YESU anasema ukinikiri mimi na ukanifua basi utaokoka!!!!!!!!...narudia tena dhambi zote zinasameheka isipokuwa kumkashifu ROHO MTAKATIFU......."wewe ulkuwa unaota"
 
Ikatwe io vipi?
Ikatwe ili iweje?
Wewe utaki utamu?
Hakuna jehannum, na kama ipo thibitisha.
Jehannum ni eneo lipo huko Mashariki ya kati na ni bonde kama la msimbazi tu hata la ufa halijafikia.
Haya shauri yako
 
Huu ndio ushuhuda wako kweli kuwa mtu akifa anaenda kuteseka hapohapo?

Unaposema wanateseka,muda huohuo maandiko yako wazi kuwa wafu hawajui lolote,niambie Mungu anapata nini kumtesa asiyejua lolote maana hana utambuzi?,

La kama mwandishi aliyosema,wapi una nukuu ya kuaminika ikionyesha wafu wanajua mambo ya maumivu na njaa au kuteswa vile?,msitumie ule mfano wa luka 16 juu yq lazaro na tajiri,kumbuka ule si mfano na si uhalisia na sababu ya mfano kuwa vile ipo.

Je,kuna maisha baada ya kifo?
Na huyu mwandishi akiulizwa maswali critical anadhani watu hatumuamini Mungu,lakini hajui anayeuliza ni nani,unapataje nguvu kumuita mwanadamu usiyemjua ni farisayo au ana dini ya kuzimu?
 
Mwandish ni agent wa shetani.anamtangaza shetani kuliko mungu.fikiri moto unamwunguza mwanadamu shetani haimwunguzi uwongo gani huu! HAKUNA JEHANAM bali ipo kiama ya wafu YANI KIFO YA MILELE..malaki 4;5-6.jehanam lilikuwa shimo kubwa la taka Yesu alilitolea mfano.soma mhubiri 9;10 na ezekiel 37
 
MAOMBI HUZUIWA.

Daniel 10:13.

Daniel aliomba maombi yake yakaanza safari, yalipofika Hapo Ulimwengu wa Giza yalizuiwa, Malaika akashuka, akapamvana na Mfalme wa Giza wa Uajemi, maombi yakayoboa na kufika Mbinguni.

Maombi yakajibiwa, Malaika akatumwa ateremshe maombi, akakutana na mfalme wa Uajemi tena, zikapigwa,πŸ’ͺπŸ’ͺ Malaika akazidiwa, ndipo akatumwa Malaika mkuu Mikaeli na kumpiga mfalme wa Giza wa Uajemi Kisha majibu ya maombi yakafika tena Kwa Danieli.

Si hadithi, Hata wewe, Kila ulipo unachungwa na kulindwa na mapepo, Mtaa wowote wenye Jina una mfalme wa Anga, chini wake anao walinzi mapepo na chini ya mapepo wapo wachawi wanaohusika na mtaa huo kuhakikisha Walio ndani ya eneo la mtaa, hawaombi, nk nk nk

Na walinzi hubadilika Kila siku.

JINSI YA KUOMBA ILI MAOMBI YASIZUILIWE NA UPATE MAJIBU KWA HARAKA.

Omba Kwa kunena Kwa lugha, anenaye Kwa lugha anena maneno ya Siri ambayo Wafalme wa Giza wanashindwa kuyatafsiri, pia hayazuiliki sababu ndani yake yumo Roho mtakatifu aliye na nguvu kuliko Malaika.

KUHUSU CARTOON.

Hakuna Mahali nimesema cartoon zote ni mbaya, zamani nyingi zilikuwa na nafundisho mazuri, lakini shetani alipogundua wazazi mmeacha kufundisha watoto wenu, akapenyeza na cartoon zake,

Nenda U-Tube, angalia cartoon inaitwa Little Demon chunguza maudhui utanambia.

KUHUSU MSAMAHA WA DHAMBI.

Msamaha wa dhambi ni Kwa Walio hai, na haipatikani hivi hivi Hadi Kwanza uijue dhambi na ndipo utubu.

Huwezi kusamehewa bila kutubu.

Walio Kwisha kufa hawana nafasi ya kutubu,maana imeandikwa Baada ya KIFO HUKUMU.

Pia fahamu kuwa kama ilivyo duniani Kuna levels za utawala mf, Mkt wa Kijiji, mtaa, diwani ,mbunge, waziri, Rais.

Hivyo hivyo, Wakristo hawalingani levels. Wapo watoto kiroho wakati ktk mwili ni watu wazima,

Pia wapo najemedari wa kiroho wenye silaha zote.

Kuza level Yako kiroho utashihudia nikuambiayo.

Amen
 
 
Kuna agent wa kuzimu mwenye kuwambia watu watubu na kuacha DHAMBI na wamkiri Yesu Kristo wa Nazareth, Ili wajazwe Roho MTAKATIFU na waishi maisha matakatifu na kuacha DHAMBI na UOVU?

Mimi ni Mwana wa Mungu aliye hai, ninawatafuta waliopotea watenda dhambi Ili niwarudishe Kwa Yesu Kristo wa Nazareth,

Ili wakitubu, Majina Yao yafutwe kitabu Cha kuzimu na yaandikwe kitabu Cha Uzima.

Aamen
 
Yote sikuungi mkono hata hilo jina la kumwita ni wakala wa shetani si sawa,ila hapo uliposema πŸ‘‡

anamtangaza shetani kuliko mungu
nakuunga mkono.
Pia shida yake kubwa anajua na kuamini yuko sahihi,hapaswi kuongeza maarifa.
 
ww umepataje ukweli huo na ujaenda uko
Mungu ndiye aliyeumba shimo la kuzimu na kumtupa shetani na Malaika wake huko,

Mungu akiamua uyajue ya huko anakupeleka,

Nia ni kuwataarifu WANADAMU wasibweteke na kudhani Mbinguni unaweza kuingia kirahisi bila kuishi maisha matakatifu,

Imeandikwa tafuteni kuwa WATAKATIFU maana hakuna atakayemwona Mungu asipokuwa nao huo utakatifu.

Kuna watu wanajiita wakristo lakini Wana nyumba ndogo, wengine wanajiita wakristo lakini ndo Mafisadi waibao pesa za umma, wengine ni Wachungaji wanaiba sadaka na kwenda kujenga mahoteli Yao binafsi nk nk,

Kuwaambia Kweli kwamba ikitokea wamekufa wataenda Kuzimu ya moto ni Sawa kabisa.

Amen
 
Nimequote vifungu vya BIBLIA mbona hujibu chochote kuhusu HOJA na maandiko nilotoa

1. Kumhusu Ibrahim kutokewa na Malaika ambao ni ROHO waliovaa miili na walikula chakula, ( Mwanzo 18:1.....)

2. Pia Lutu aliwapokea Malaika ambao ni Roho wenye miili ya WANADAMU na walikula chakula Cha KIMWILI? ( Mwanzo 19:1-38.)

3. Yesu pia imeandikwa alishuka kuzimu na kumnyang'anya Shetani funguo za MAUTI na kuzimu?

4. Yesu pia msalabani anamwambia yule mfungwa pembeni yake kuwa Leo hii utakuwa nami Paradiso, ikiwa hawana miili iweje wakutane na watambuane?

Jibu HOJA hizo nne ikiwa unajua chochote.

NB: Kusoma BIBLIA na kuielewa unahitaji msaada wa Roho mtakatifu na mafunuo.

Aamen
 
According to Biblia ukifa ni kama umelala wala hujui lolote, hili wewe umeliokota wapi?
Usisome andiko moja pekee ,soma yote na uombe ufunuo juu ya maana. BIBLIA ni coded,

Yesu kabla ya kufa alimwambia mfungwa pembeni yake aliyetubu kuwa, Leo hii, utakuwa nami Paradiso hujasoma?

Hujasoma kuwa Yesu alipokufa alishuka kuzimu na kumnyang'anya Shetani funguo za MAUTI na kuzimu?

Ikiwa waliokufa hawatambui chochote kwanini mnafanya IBADA za WAFU na kuwasha mishumaa makaburini, hamjui mnawasiliana na kufanya I ada za WAFU?

Soma " Live Kutoka kuzimu" itaongeza ufahamu wako juu ya BIBLIA.

Pia nimequote maandiko Kila baada ya maelezo Fulani, Fungua BIBLIA usome kama utakuta tofauti na nilichokuletea!!
 
Ila Haya mambo mnaandikaga mnayatoa wapi?Daah nyie watu bhana
Kuna mchawi na mganga mmoja humu JF Huwa anamwambia kutumia chumvi ya mawe kuinyunyiza kabla ya kulala Ili kujinginga na wachawi,

Uliwahi jiuliza maarifa hayo potofu kayatoa wapi zaidi ya kuzimu?

Maagent wa kuzimu mnawaelewa, Agent wa Kutoka JUU kwann upate tabu kumsoma?
 
Hivi unadhani Mshana Jr mganga basi?kasoma Kwa ma monk huko we ndio unadhani mganga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…