Jambo la muhimu hapa Ni kwamba unahitaji msaada wa kiroho, Jambo hili linahitaji Muda yaani hatua kwa hatua. Unashauriwa uweke Nia katika kujifunza na kutafakari neno la Mungu.
Ni dhahiri shetani amekudanganya kwamba unachojitaji wewe Ni kuamini tu lakini Mambo mengine unaweza kuendelea na utaurithi ufalme wa Mungu (Kama kuiba iba, ua, roga Sana, uzinzi kwa wingi nk).
Ni kweli wote walio chini ya Yesu hakuna atakayepotea, lakini pia chini ya Yesu hakuna wachawi,wazinzi, waasherati, wauaji, waabuduo sanamu, wasengenyaji, wafiraji, waongo nk. Wote walio chini ya Yesu siyo tu wameamini lakini pia walitubu na kuacha matendo yao ya kale.
Mfano Yesu wakati ameletewa yule mwamanke aliyekamatwa akizini alimwambia "enenda zako usitende dhambi Tena".
Siyo kweli kwamba ukiokoka wewe Basi na mtoto wako jambazi, shoga na mwizi nae hatahukumiwa kwa matendo yake.
Mwisho: imeandikwa
"Mit 4:24
Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe."