Live Kutoka Mbinguni/ Welcome back to Heaven

Ubarikiwe ndugu Girl and!!

Mtu ni ROHO Si mwili.

Unaweza kupelekwa Mbinguni na Kisha kurudishwa tena katika mwili Yesu akiamua kufanya hivyo.

Yohana aliyeandika ufunuo wa Yohana alienda Mbinguni Kisha akarudishwa kuandika kitabu Cha ufunuo.

Habari za Mbinguni Kwa watakatifu ni kuwakumbusha kuwa duniani tu wapitaji tu.

Amen
 
Kwanini?
MTU ni roho!
Na roho INA mahali inatoka unawekewa,na ukifa inatoka inarudi ilikotoka!
Ndo maana ya hiyo aya!

Futa aya ya kwanza mwanadamu hajawahi kuwepo milele huko ni kumkufuru Mungu
 
Yesu alisema SIWAOMBEI UWATOE DUNIANI akijua fika kuna watu wanahubiri habari za mbinguni wanasahau kwamba Mungu aliumba mbingu na nchi akamuweka INTENTIONALLY mwanadamu kwenye nchi akamwambia atawale na kuvitiisha vitu vyote!

Tusiingie huu mtego, ukisoma vizuri hata mbinguni ni kwa muda tu!!!
 
Ni sawa,

Lazima tupite duniani twende Mbinguni Kisha baada ya Dunia kuangamizwa, utateremshwa mji mpya na Nchi mpya na tutaishi milele.

Kwakuwa Dunia itaangamizwa, sisi tunapita tu, tuwekeze Mbinguni, akiba zetu hazitapotea.

Ubarikiwe. Amen
 
Kingine mtumishi DO NOT, I REPEAT DO NOT UNDERESTIMATE MWILI,bila huo hauwezi kufanya kazi kwenye ulimwengu unaoonekana ni SHERIA ndiyo sababu YESU alivaa MWILI.

udhaifu wa mwili ndiyo unauwezesha kustahili nguvu za Mungu kama bible isemavyo tuwapo wadhaifu NDIPO TUNA NGUVU.

kuna sababu Mungu kakupa mwili mtumishi Rabbon
 
Siudharau mwili, ni instrument muhimu tuwapo duniani,

Lakini mwili ni dhaifu, hautendi mapenzi ya Mungu,

MWILI muda wote upo kushindana na Roho.

Asili ya MWILI ni udongo mavumbini, lakini Asili ya Mtu ambaye ni ROHO ni Mbinguni.

Asante Kwa mchango mzuri. Ubarikiwe.
 
Nimefurahi jamaa kufika mbinguni wengine tushafika na kupitiliza ata saivi hatuna uhakika tuko wapi ila najua tuko mbinguni kwa mbele yakee
 
Nimefurahi jamaa kufika mbinguni wengine tushafika na kupitiliza ata saivi hatuna uhakika tuko wapi ila najua tuko mbinguni kwa mbele yakee
Nawe ubarikiwe.

Siku ya HUKUMU Jina lako litajwe katika kitabu Cha Uzima, uingie Mbinguni Kwa maisha ya milele.

Amen
 
Hapa mtumishi huelewi unachokisema BIBLIA ikikwambia Mwili ambao hautendi mapenzi ya Mungu wanamaanisha EMOTIONS yaani hisia

Binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu anakuwaje dhaifu?

Mungu alivyomaliza kuumba aliangalia vitu vyote akaviona kuwa ni VYEMA, wewe unakuja unataka tuamini Mwili ni dhaifu? Unapingana na uumbaji??

Ukitolewa mwili unaouita UDHAIFU unakosa sifa za kuishi duniani!! Ni passport, ya kuwa hapa duniani huko mbinguni huhitaji mwili huu kufunction.

Tuwaambie watu jinsi gani wataishi maisha yaliyoandikwa katika Kumbukumbu 8,tuwaeleze jinsi gani Muumba aliuvaa mwili ili atukomboe toka kwenye dhambi ili tuhesabiwa haki kwa KULIAMINI NENO LAKE


 
Basi tusibishane.

Ubarikiwe πŸ™
 
Yaani,ila wanavyoliwa Sasa huko na wasaidizi wa mtumishi,utasikia nimefunuliwa we ndio mke wangu,anahama from one place to another
Jikite kwenye mada. Tafadhari πŸ™
 
Umejitahidi sana kuandika jambo hili la safari yako ya kwenda mbinguni.
Lakini nilipokusoma na kuona error kulingana na mafunuo ya ujumla wa maandiko ya biblia nikapata shaka kwamba hili andiko ni la kiakili na kama sivyo adui alihusika kukupa hili ono.
Kilichonipa shaka ni kuona ulipozungumzia majina 12 ya wana wa Israel kule mbinguni jina la Dani likiwepo.
Majina 12 ya wana wa Israel yaliyotiwa mhuri katika ufunuo 7 jina la Dani halimo.
Halimo kwa kuwa liliondolewa na sababu ni ibaada ya sanamu.
Ukiangalia vizuri maandiko wana wa Israel ni 12 ikiwa ni pamoja na Dani ,Lawi na Yusufu. Lakini katika kitabu cha Hesabu waliopewa heshima ya kushikilia majina 12 ya kabila za Israel pana Jina la Manase na Efraim bila kuwepo na jina la Lawi na Yusufu.
Lawi na Yusufu hawakuwepo kwa sababu Lawi yeye alichukuwa uridhi wake kwa Mungu kwa kuwa hakugawiwa eneo la kuridhi. Yusufu yeye eneo la urithi wake lilishikiliwa na mwanae mmojawapo kati ya wawili waliopewa heshima hiyo yaani Efraim na Manase.
Sasa wakati Israel walipokuwa wamerudi kwenye ardhi ya wenyeji wao wakati kukiwa na mgawanyiko kati yao juu ya ufalme wa Yuda chini ya Rehoboam mwana wa Suleiman na ufalme wa Israel chini ya Yeroboam mwana wa Nebati, eneo la Dani na Efraim ndilo lililotoa nafasi ya kujengwa madhabahu watu waabudu huko ili watu wasipande Yerusalemu kuabudu katika hekalu la Bwana lililojengwa na Suleimani.
Kwa sababu ya dhambi hii ya kuruhusu madhabahu ya mungu mgeni katika ardhi ya urithi wao Mungu aliwaondoa katika heshima ya kushikilia jina la kabila Dani na Efraimu na badala yake majina yaliyotiwa mhuri ya ufunuo 7 linarejeshwa jina la Lawi na Yusufu huku nafasi ya jina la Dani ikishikiliwa na jina la Manase.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sawa,

Kama umesoma vizuri ni ushuhuda wa Aston Mbaya. Kosa ni langu niliyereport, naomba nisamehewe Kwa kukosea na ninarudi kubadili. USHUHUDA wake haukutaja Majina, Mimi ndiye niliyekosea kuyaandika Kwa kutumia kitabu Cha mwanzo Badala ya Ufunuo.

Ahsante Kwa ufafanuzi na ninarudi kuedit.

UBARIKIWE.

Amen
 
Huyu bwana Adam Mbaya alikua anazungumza lugha gani na Yesu?
Lugha zinazotumika Mbinguni ni lugha za Mbinguni.

Mwanadamu hupewa kuelewa tafsiri ya lugha hizo. Na akiongea wanaelewana.

Ubarikiwe.
 
Ndugu Kiby karibu sana kushare nasi shuhuda za Mbinguni ulizo nazo katika Uzi huu Ili kuwatia moyo WATAKATIFU na kuhubiri INJILI.

Ubarikiwe.
 
Ndugu mwandishi naona una ujumbe mzuri ila ubora wa uwasilishaji wako upo partial .. mfano,hujaeleza namna ulivyokutana na Yesu bali unasema ukamuuliza Yesu hatujui umekutana naye vip na umemjuaje ni Yesu?
Kuongezea je,Yesu alikuwa mzungu, mwarabu,mwafrika,muhindi ? Muonekano wake ,rangi,nywele?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…