Live Kutoka Mbinguni/ Welcome back to Heaven

Ubarikiwe mtumishi Kwa ufanuzi mzuri.

Pamoja sana. Amen
 
WATAKATIFU waliookoka wafapo na kwenda Mbinguni, huenda kupumzika kusubiri siku ya HUKUMU.

Waliokufa katika Dhambi huenda kuzimu kusubiri HUKUMU.

Hawachanganywi pamoja.

Hujasoma Ufunuo imeandikwa Yesu atakuja akiambatana na maelfu ya WATAKATIFU?

Ndo nakwambia, kusoma BIBLIA utasoma, ila kuielewa ndipo ulipo mtihani.

Ubarikiwe.
 
Na ndo maan nimekuambia nionyeshe hayo mafungu unayosema 😅

Biblia inasema

Isa 8:20 SUV

Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili (Biblia), bila shaka kwa hao hapana asubuhi.

Sasa mkuu ......
Shetani bado anaendelea na msemo wake kuwadanganya na kuwaambia hakika hamtakufa ila mtafanana na yeye?

Maana ufunuo kuna Ufufuo wa kwanza na wa pili..
Ufufuo wa kwanza kwa ajili ya watakatifu na ufufuo wa pili ni kwa ajili ya wadhambi..

Sasa kama hakuna kufa anafufua nini 😅😅

Ufunuo 20:6
"Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu."


1 The 4:13-18 SUV​

Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
SASA WEWE UNATOA WAPI UNAYOFUNDISHA WATU ACHA KUPOTOSHA..

Kama hutatoa andiko nawaonya wakristo wanaokusikiliza kwa...

1 Yoh 4:1 SUV

Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
 
Kumuelewesha MSABATO KAZI sana.

Tuanzie hapa.

1. Mtu ni nini?

2. Kufa ni nini?

Twende Polepole kabisa.
 
Kumuelewesha MSABATO KAZI sana.

Tuanzie hapa.

1. Mtu ni nini?

2. Kufa ni nini?

Twende Polepole kabisa.
Dah mkuu una bahati mbaya sana me sio msabato kabisa..
Nashindwa nikueleweshe kutumia hali ipi ngoja nitumie Biblia tu maana nikitumia vitu vingine ntakupoteza..

Mtu kw mujibu wa biblia ni Mwili wenye pumzi ya uhai kwa mujibu wa maandiko ya kibiblia..

Kufa ninkuondokea na Pumzi ya uhai

Nimekujibu kwa level ya chini kabisa..
 
3. Roho ni nini?

4. NAFSI ni nini?

Nijibu, usichoke 🙏
 
3. Roho ni nini?

4. NAFSI ni nini?

Nijibu, usichoke 🙏
maswali yako ni mazuri halafu very Important..
(MIND, BODY, SPIRIT)
(SPIRIT,SOUL AND BODY)

Holy triology

natamani Nikujibu kwa mlengo wa spirituality ila ngoja nikujibu kwa mlengo wa kibiblia...

Roho (Spirit) in maana nyingi snaa natamani niongee maana huu ni ulimwengu mpana sana..

japo kibiblia ni simply Pumzi ya uhai na ulimwengu fulan

ila nafsi (Soul) ni utambuzi wa mwili yani uwepo wa kimwili

Ila natamani nieleze zaidi
 
Mungu aliposema, na Tuumbe mtu Kwa Mfano wetu,

Kati ya MWILI , NAFSI na ROHO, mtu aliye mfano wa Mungu ni yupi kati ya hivyo vitatu?

Tukipata jibu Hilo itakuwa Rahisi kujua nini maana ya "WAFU hawajui lolote ".
 
Mungu aliposema, na Tuumbe mtu Kwa Mfano wetu,

Kati ya MWILI , NAFSI na ROHO, mtu aliye mfano wa Mungu ni yupi kati ya hivyo vitatu?

Tulipata jibu Hilo itakuwa Rahisi kujua nini maana ya "WAFU hawajui lolote ".
Mkuu sasa huu ndo uwanja wangu Na ningetamani tuwe na maongezi marefu kuhusu hili..(Maana hili linahusu spirituality na mimi ndo mlengo wangu huko)

Ila Mungu aliumba Mwili akampulizia Pumzi (Roho) yenye Nafsi ya Uhai..
Kwahyo uliumbwa Mwili ila vilivyotoka kwke ni Nafsi na Roho...
Mkuu natamani tuwe na mjadala mkubwa sana kuhusu haya mambo
 
Pumzi( Roho) ilipoungana na mwili ndipo ilipozaliwa NAFSI hai.

Kwahiyo jibu kuhusu "WAFU hawajui lolote" limepatikana?

Kwamba vinapotengana hivi vitatu, kipi hakijui lolote?

Kwa maana tumejua kilicho mfano wa Mungu ni Cha milele, kufa ni kutengana udongo Ulio mavumbi usojitambua, na umilele.
 
Sasa hiyo nafsi ndo huifadhiwa mpaka siku ya hukumu ila kinachomrudia mungu ni roho
 
Bangi si nzuri
 
sasa kama wafu wakifa wanaenda mbinguni kwanini ww ukiumwa unaenda hospital si usubiri ukufe uende peponi...na kama wanaenda mbinguni basi iyo hukumu ya kiama ya kazi gan
 
duuu ambaye haielewi biblia anajifanya mjanja ety ukifa unaenda mbinguni na wengne waenda kuzimu duuuh.
..

.sasabkama ni hivi basi hakuna haja ya iyo hukumu maana wengne wameenda kuzimu wengne wapo mbinguni🤣😆😅
NAFSI huhifadhiwa wapi?

Na inapohifadhiwa hujitambua au haijitambui?
nafsi = roho + mavumbi kaburini maiti haijitambui iv unajua maana yabkufa? from biology pointbof view
 
sasa kama wafu wakifa wanaenda mbinguni kwanini ww ukiumwa unaenda hospital si usubiri ukufe uende peponi...na kama wanaenda mbinguni basi iyo hukumu ya kiama ya kazi gan
Hakuna Mbingu ya WAFU,

Mbingu ni ya WATAKATIFU Walio hai.

Amwaminiye Kristo Yesu hafi, analala tu.

Mbinguni watakatifu wanaenda kupumzika wakisubiri HUKUMU.

Kuna UNYAKUO, MAUTI ya kwanza na MAUTI ya pili, usichanye vitu hivyo vitatu.
 
Biology haijadiliwi hapa.

Hapa tunajadili spiritual realm.
 
Mbingu ya kiwaki huku kwetu kuna mbususu za kumwaga chura pro max wachana na izo fake za mloganzia
 
Mkuu kama Kuna kula na kunywa huko mbinguni, inamaana nyumba za huko Zina vyoo kama huku Duniani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…