Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo?

Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo?

Huyu p,anaharibu hiki kipindi kwa sababu ya tamaa zake za kutafta uteuzi kwa nguvu,,nawashauri startv wamtoe vinginevyo hiki kipindi kitakuja kukosa watazamaji
 
Wanabodi,



Tuko Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Bado Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo?.

Karibu

Paskali

Watanzania hatuko serious, Ferry watu hawanawi, wanapaka tu maji kuwazuga walinzi, ukiwaelimisha unaambia ucha uzungu. Kuna culture contradion kwenye hili, ugonjwa unaonekana ni was kimagharibi zaidi
 
The media has been muzzled by the myopic government, how then can the same media be efficient?. If you are not permitted to report who is suffering from or died of covid 19, then you are only remaining with one task of singing the government's favourite songs. The media is not free, therefore we shouldn't blame it.
You have to tell us which country has allowed its media to report who is suffering without approval from authorities?! Do you know what happened to the captain of one of the USA warships who leaked information to the media on almost 100 sailors on his ship who had tested positive of coid 19 virus?!
 
Media hawatimizi wajibu wake.
Tunataka tupate picha za Hospitalini hasa kula mloganzila tujue kinachoendelea.

Kingine tu ataka tujua hatma ya wafanyakazi wa afya, je wana vifaa vya kutosha vya kuwakinga?
Je familia zao je?
Je wanalipwa stahiki zao vizuri?
Media zetu zinatakiwa zitupe haya yote .
Waandishi wa habari ni kama wanajeshi na madaktari. Wapo mstari wa mbele
 
Update 1 Live imemalizika mchango wangu 1
Nimepongeza hatua ya serikali kuweka list ya wazungumzaji rasmi 5 wa Corona kitaifa ambao ni
  1. Rais wa JMT
  2. M/Rais
  3. Waziri Mkuu
  4. Waziri wa Afya
  5. Msemaji Mkuu wa serikali.

  1. Nikasema hatua hii ni mzuri ili taifa lipate taarifa moja iliyonyooka, kama kila mtu ataachwa ajisemee itakuwa chaos, utaratibu huu unaitwa restrictive media reporting na hutumika hata wakati wa vita.
  2. Information is a two way traffic, serikali inatoa tuu taarifa, media ilikuwa ina wajibu wa kufikisha taarifa za serikali kwa umma, lakini hakuna utaratibu wowote wa serikali kupokea mrejesho hao wananchi wanaopelekewa taarifa na maelekezo ya serikali jee wanasemaje?. Wanatekeleza?, Wananawa kwa maji tiririka?. Wanafanya social distancing?. Kwenye eneo hili, media hatujatimiza wajibu wetu kikamilifu.
  3. Kazi ya hao wazungumzaji wanne ni kutoa update ya Corona. Kwenye eneo hili la media kutoa taarifa za serikali za Corona, media tumetimiza wajibu wetu kikamilifu kabisa na tunastahili pongezi za dhati.
  4. Lakini ukweli Corona ni zaidi ya updates, kila vizara, kila idara, kila Taasisi itakuwa affected na Corona hivyo mawaziri wengine na wakuu wengine wote wana wajibu wa kuizungumzia Corona haswa how to mitigate the after effects, huko sio kutoa update huko ni kuisaidia serikali na Watanzania jinsi ya kukabiliana na madhara ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Corona. Kwenye eneo hili la kutoa taarifa nyingine zozote kuhusu madhara ya Corona kwa sekta nyingine zote, media hatujatimiza wajibu wetu kikamilifu.
  5. Watoa taarifa wa serikali wanaisoma taarifa ya maandishi na kuwasomea media hakuna any room kwa media yoyote kuuliza kupata ufafanuzi, matokeo yake media kazi yake ni kulishwa tuu habari, spoon fed, na media kazi yake ni kumeza tuu hizo, habari, hukuna kuzichakata, hakuna news analysis, hakuna news relevance alimradi Msemaji ni serikali na serikali imesema.
Pl
 
Wanabodi,



Tuko Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Bado Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo?.

Karibu

Paskali

Wajibu wa vyombo vya habari ni kutoa habari. Siyo kutabiri kama wafanyavyo baadhi ya viongozi uchwara wengine wa dini. Wnakutajia mpaka tarehe itakavyokuwa hivi na vile. Tuwaachie upuuzi huo wao wenyewe. Vyombo vya habari toeni taarifa ya uhakika wa mambo mliyoyaona. Kwisha.
 
Binafsi nafikiri ile marufuku ya kuongelea corona iwe ni kwa watu 3 ama haijaeleweka sawasawa au ilikua too much kiasi media zikaamua kurefrain juu ya hili swala. Ama kwa kujua au kutokujua

The best thing media itakuambia ni kunawa mikono na kutumia sanitizer. Nafikiri media ingeweza kua na wajibu mkubwa zaidi ya kukumbusha kunawa mikono.
 
Jukumu la Pili la Media ni Uelimishaji Jamii
Hili pia media imejitahidi ila bado, Watanzania wanaelimishwa kuhusu Corona lakini kazi ya uelimishaji bado inafanywa kwa kiwango cha chini, hivyo kuna watu wananawa kwa maji tiririka kwasababu ni lazima, lakini kwenye social distancing bado, Misongamano bado ipo kila mahali.
Zaidi ya kuripoti zile updates za Corona, hakuna TV yoyote, redio yoyote, au magazeti yenye dedicated Program kuhusu uelimishaji umma wa Corona zaidi ya yale matangazo ya Corona.
Hivyo kwenye jukumu la media za Tanzania katika uelimishaji umma kuhusu Corona bado sana.

Kwa vile Corona haina dawa, Watanzania walipaswa waelimishwe hao wagonjwa huko kwenye vituo walikotengwa wanafanywa nini hadi wengine wanapona kabisa na kuruhusiwa ili wenye uwezo wawatibie watu watu kwa kuzua na sio kusubiri watu waugue wazidiwe wakarudikane kusubiria... wakati watu wangeelimishwa huduma ya kwanza ingeanzia nyumbani.

There's a lot of education inputs kutoka nje kuliko kutoka ndani. Serikali imetoa list ya wataalamu official watakao elimisha kuhusu Corona, sijabahatika kuona hata kipindi kimoja cha wataalamu hao

Vituo vya Redio na TV vitenge dedicated Program za uelimishaji umma kuhusu Corona. Hao waataakamu wawe pro active kwenda kwenye media kuelimisha umma.

The regulator, TCRA, atoe muongozo kwa vyombo vyote vya utangazaji na mitandao ya kijamii kuandaa vipindi elimishi kuhusu Corona

Wakati Wazungu wamehangaika kutafuta tiba, sisi tungewatumia wataalamu wetu wote kuanzia madaktari, watiba mbadaka, tiba asili, ma sangoma, waganga hadi Babu wa Samunge kukijaribishia kikombe.

Hao wachungaji wenye uwezo wa nguvu za uponyaji, waruhusiwe mahospitalini ili tushuhudie uwezo wa nguvu zao na sio kuwakamua masikini Watanzania kwa kusingizio cha kufanya miujiza, wenye uwezo wajitokeze na serikali iwaruhusu.

Unapo deal na gonjwa ambalo halina tiba na kuna wagonjwa wamezidiwa mahututi na hatimaye watakufa tuu, what is wrong to turn them into Guinea pigs and test them, we may save them, hata kama kwa kuwajaribishia hizo tiba mbadala na bado wakafa, let it be, at least tumejaribu, hata tusinge jaribu, they were going to die tuu anyway. Let's try to do anything something kuliko doing nothing.

P
 
3. Jukumu la 3 la Media ya Tanzania Kubudisha Jamii
Kazi ya tatu ya media ni kuburudisha jamii. Kwenye eneo hili pia media ya Tanzania haijatimiza wajibu wake kikamilifu.
Kwa vile Corona ni janga, na kufuatia kilichotokea Wuhan, Italy, UK na US, Corona imetisha na kuogofya, media nazo zikalipokea hivyo hivyo. Shujaa wa eneo hili ni rais Magufuli aliposema tusitishane, ka Corona ni ka ugonjwa kadogo tuu, tena sio kirusi ni shetani disguise as kirusi, tukamkabidhi kwa Mungu kiboko ya shetani!.
Psmoja na mabalaa yote ya janga la Corona, pia kuna mazuri ya Corona, kuna positives za Corona zilipaswa kuangaliwa. Mwana FA na Salaam did. Kuna watu wanapona wanaruhusiwa. Media ilipaswa kuwatafuta madaktari waliofanya miujiza tufanye human interest stories za mazuri ya Corona. Kuna watu wamepiga pesa kwa kuziangazia fursa za Corona, hata Diamond alichofanya akiwa quarantine ni jambo zuri, tusiizungumze Corona kwa ubaya tuu, tuizungumze kwa wema. Italy Wazee ni wengi mno na wanaishi sana, hivyo Corona ni kama mkombozi fulani kwa blessing in disguise, ame fykelea...

Sisi baadhi ya familia, baba na mama ni work class, familia yangu nina watoto 9, wamepishana miaka 2, the oldest ni 24, 22, 20, hawa wako vyuo.
Then kuna 18, 16 na 14 wako sekondari
Kisha kuna 12, 10 na 8 wako primary. Ukiondoa Christmas Day, there is no any other time watoto wote wako nyumbani. Kwenye Corona wote wamerudi home, baba ni mwandishi wa habari wa mikutano, warsha, seminar, makongamano na events, zimesimamishwa, niko home. Wife ni mfanyabiashara wa safari za nje, zimesimamishwa, Nyumbani kuna Dada wa jikoni, dada wa usafi, kaka wa garden, feeding a family of 15 is not a joke. Ukishinda nyumbani na watoto ndipo unagundua kiukweli hawa wadada wa kazi, walipaswa kulipwa vizuri!.

Hivyo Corona has lots and lots of human interest stories na sio habari tuu za ku stigimize kwa idadi inaongezeja, lakini wanaopona hatuwazungumzi. Kutembelea kambi za quarantine na ku file stories about life in quarantine zitakuwa very interesting stories.
P
 
4. Jukumu la 4 la media ya Tanzania as a Watchdogs of the Society kwe janga la Corona
Kazi ya Watchdogs ni wale mbwa wanaofanya kazi ya ulinzi, kazi yao ni kubweka tuu ili kumjulisha mwenye nyumba something is not right. Hapa ndipo media inasemwa ni mhimili unaojitegemea wenye kazi ya kuiangalia jamii na kuiangalia serikali.

Hawa mbwa pia wapo mbwa wa aina 3,
1. Sheppards Dogs habweki ana ng'ata.
2. Barking Dogs kazi yake ni kubweka tuu haumi
3. Lap Dogs kazi yake ni kuchezesha mkia na kukamba lamba.

Kwenye janga hili la Corona, the Tanzania media has failed this nation katika role ya Watchdogs.
Toka Corona inaanza kule Wuhan ije December 2019 tungekuwa na serious media, tungeanza kubweka ili kuianda serikali yetu for preparedness kwa Corona, angalieni China ilipolipuka tuu Wuhan, mpaka imedhibitiwa haikufika Beijing na wala haikuingia Japan.

Tanzania ndio nyumba yetu, baba mwenye nyumba ni rais wetu na serikali yake, wao wako ndani wamelala, sisi media ndio mbwa ambao tuko macho tunalinda nyumba. Corona ndio mwizi anayekuja kutuibia nyumbani kwetu.

Media ya Tanzania ingekuwa ni Sheppard dog, ingefanya kazi kama gazeti la The Washington Post wakati wa kahfa ya Watergate, naomba tukiri udhaifu kwenye complex issue kama hii ya Corona, media zote za Tanzania hakuna hata moja yenye uwezo kuajiri ma medical journalist wa kuandika story za kina kuhusu Corona ambazo zingeisaidia serikali yetu. Angalieni CNN na Dr. Sunjay Gupta.
Hivyo media ya Tanzania kwenye kuisaidia serikali kwenye hili la Corona ni zero. Naamini kuna madaktari wazuri tuu ambao wanaoenda kuwa watu wa media kama alivyo Dr. Maro kwa Clouds.

Tukija yule mbwa wa pili wa barking Dogs, kiukweli mainstream media pia has failed this nation on this role. Kazi hapa ni kubweka tuu ili kumuansha mwenye nyumba.

Media ambayo imelitenda hili ni JF pekee.
Pale rais wa nchi anaposema ka Corona ni ka ugonjwa kadogo tuu na serious media ambayo ni barking Dogs zilipaswa zibwekwe.

Rais Magufuli na serikali yake walipaswa wasaidiwe ma media kwa kuwaonyesha good oractices elsewhere ambazo zimesaidia.

Rais Magufuli aliporuhusu mikusanyiko ya nyumba za ibada, serious media ilipaswa i bweke kwa kuonyesha kama Roma wenyewe kwenye Ukatoliki wamefunga makanisa, Saud Arabia wenye Uislamu wamefunga misikiti who are we?. Media tulipswa kuwaumbua viongozi wa dini wanaohemea sadaka hata kwa kuhatarisha maisha ya watu.

Hapa Tanzania tulipaswa kuwa na strong independent media yenye uwezo wa kumweleza rais Magufuli na serikali yake kuwa baadhi ya hatua anazosita kichukua ikiwemo kuendelea kuruhusu mikusanyiko ya nyumba za ibada is wrong. Media ionyeshe jinsi Mungu alivyo Omnipresent yuko popote na mikusanyiko ya nyumba za ibada sio miongoni mwa mikusanyiko muhimu. Sisi jf tulisema.

Kwenye hili media ya Tanzania ni just lap Dogs!. Kazi ya mainstream media zetu haswa za electronics ni kuchezesha tuu mkia na kulamba kamba kila kinachofanywa na serikali, hakuna analysis, hakuna critics na mwendo wa kusifu tuu na kupiga makofi.

Mimi kwenye Programs yangu hii ya Jicho Letu, angalau tumemuita Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndugulile, maswali yalikuwa mengi muda ulikuwa mfupi ila naomba kukiri udhaifu hata mimi pia ni Lap dog tuu, kwasababu the right to information act inataka tuwaandikie maswali tuwape rasmi lazima maswali yote yangejibiwa.

Hata hivyo bado nina mshukuru Dr. Abbas for being available twice at my disposal tukashindwa sisi. Kwa upande wa Dr. Ndugulile kiukweli nilimbwekea ila naye yuko fit sana kukwepa mishale. Hata yeye namshukuru na ni mwana jf mwenzetu ila...

Kitendo cha media ya Tanzania kukubali kuwa lapdog hivyo kushindwa kuitumia position yetu as Mhimili, the 4th Estate or The 4th protocol kumepelekea media kudhaurika, kama the Washington Post limewahi kumchoropoa rais fulani Ikulu, media ya Tanzania ingeonyesha iwezo huo kwa kuisaidia serikali kuiambia mipango yake haitekelezeki na kuonyesha matokeo ya serikali kutokusikiliza ni nini, hajafu serikali kweli ikadharau na sasa tunaelekea kwenye hicho media ilichokisema. Kikitokea cha kutokea, ambacho kama serikali ingeshauriwa na kusikiliza, tusinge fika huku tunakokwenda kifika, serikali kama hii ingekuja kuwarudia wananchi na kuwaeleza nini?.

Media has failed this nation!. Hatukutimiza wajibu wetu kikamilifu.

P
 
Pascal Mayalla,hayo umeyaongelea Star TV lini?Nje ya huko TV mlipopata wasaa na mahali pa kusemea mlifanya hivyo?Je, ni salama kuongea ukweli hapa nchini hadi uwalaume mainstream media?Unafahamu kilichoifanya Mwananchi Online kufungiwa?Vipi kesi za uhujumu uchumi za kina Kabendera?
 
Alafu umealikwa na star tv,hao TBC unaitangaza kwenye Tv nyingine ili iweje,hata kama unatafuta uteuzi ,umepitiliza,kwani wateule wote huwa wanalamba viatu vya wakubwa ndipo wanapata nafasi?
Mbona Cnn siyo ya serikali na ipo mstari wa mbele kutoa elimu na taarifa kuhusu Covid -19. Kualikwa Star Tv sio kosa jambo la msingi ni kuleta ujumbe wenye manufaa juu ya hili janga.
 
Masuala nyeti kama haya yalikuwa yakitokea panakuwepo na waandishi wa habari wenye upeo wa ziada, wanaenda mbali zaidi kufanya uchunguzi wao, wajue idadi ya walioambukizwa, waliopona, na vifo vipo vingapi, hii ingesaidia kuuaminisha umma kama mapambano yanayoendelea yanafanikiwa au hapana.

Matokeo yake utawala huu umewafunga midomo wote hao, mnataka wote wafanye kazi moja ya kusifia tu, ndio maana jana Waziri wa Afya akasema sasa ataanza kuripoti ukweli, kumbe hiyo kazi ilitakiwa iwe inafanywa na waandishi wanaojielewa, wamewafunga midomo, wakatulisha habari za uongo mpaka wamechoka wenyewe.

Sasa unaposema kama media inatimiza wajibu wake naona hiyo media imelazimishwa kutimiza huo wajibu kwa upande mmoja tu, ule wa kusifia, vinginevyo wakae kimya kama wana maoni tofauti, huu ndio unaoitwa "uzalendo wetu" wa siku hizi.

Wengi wameamua kuchagua njia ya pili kukaa kimya, kwasababu kwa wengine ni sawa na kuwatusi kuwalazimisha wafikirie kwa upeo mdogo kwenye jambo wanaloona wanaweza kwenda mbali zaidi, ila wanaogopa kuwakasirisha watawala kwa mawazo na maoni yao watakayotoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu napenda nikupongeze katika hili bandiko. Wengi wamejisahaulisha ni kwanini sheria ya habari ilipitishwa fasta... wala hawataki kuwakumbuka wanahabari wahanga waliojaribu kuandika yasiyopendwa...
 
Back
Top Bottom