Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo?

Mkuu Denoo J, kwanza asante kwa mchango wako kwenye mada hii, usemayo ni kweli, swali ni jee kwenye media zetu Tanzania, jee tuna waandishi wenye upeo huo wa ziada na uwezo wa kufanya story ya uchunguzi kuhusu maambukizi ya Corona?.
Wakati serikali walikuwa na maabara moja ya kitaifa kupima Corona iliyopo Dar es Salaam, hospital ya mabalozi iliyopo Masaki, Agha Khan na Regency walikuwa tayari wanapima na wanahudumia wagonjwa, baada ya serikali kuweka restrictions za updates za Corona ni taarifa ya serikali pekee, na vipimo ni vya serikali tuu, nani angethubutu kumpa data huyo mwandishi?. Na lets assume mwandishi huyo katumia mbinu zake za ki IJ, kapata data za Masaki, Agha Khan na Regency, then ndio angezifanyia nini wakati tayari serikali imeisha weka restrictions?.
P
 
Mkuu Denoo J, hili nimelieleza vizuri sana, kuwa kwenye uhabarishaji wa taarifa za serikali kuhusu Corona, media imetimiza wajibu wake ipasavyo, ila katika wajibu wa jumla wa media, bado hatujatimiza wajibu wetu kikamilifu.
P
 
Mkuu Michael Makene, asante nimekisikia, na karibu mitaa hii.
P
 
Wandugu, hapa nafanya tuu follow up ya Corona nikipitia kujikumbusha niliwahi kuandika nini au kusema nini kuhusu Corona na hiki kinacho endelea sasa. Corona is real tusifanye masihara, tujilinde kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Kila Jumamosi asubuhi kuanzia saa 1:30 hadi saa 3:00 asubuhi , Star TV, huwa ninakuwa live kwenye kipindi cha TV cha Jicho Letu Ndani ya Habari ambacho huwa kinatangwa live na Star TV kila siku za Jumamosi asubuhi, kwa Jumamosi ya kesho, mgeni wetu ni Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe tukijadili kuhusu athari za Corona kwenye sekta ya Habari, nini kifanyike.

Ukipata nafasi karibu utufuatilie.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…