Live on Star TV, Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe azungumzia changamoto za Corona Sekta ya Habari

Waziri wa habari mh Mwakyembe amesema bunge la Uingereza juzi limeanza vikao kwa kuiga ubunifu wa Spika Ndugai.

Mwakyembe amesema sasa wabunge wa UK wanakaa katika chambers wakiwa wachache wachache wakiendelea na vikao vya bunge ukiwa ni ubunifu ulioasisiwa na Spika Ndugai.

Tanzania kwa sasa tumekuwa nchi ya mfano hata Rais Trump amefuata nyayo za Rais Magufuli kwa kutangaza siku maalumu ya Maombi ya kuliombea taifa.

Maendeleo hayana vyama!
Huu uchafu ndiyo Pascal Mayalla alitaka tufuatilie?
 
Nimemsikia waziri anasema jamii forums si chombo cha habari ni kijiwe cha wahuni,,, na awastahili kulindwa kwa sababu watoa taarifa wa jamii forums awana weredi wa habari zaid ya mitusi tu wanatukanana

Tunazidiwa hata na Wakenya wanapashana taarifa bila mitusi lakini Ss watanzania ni aibu kwa kweli....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mayalla naona umetumia nafasi vyema kutema nyongo zako kwa Waziri...Naona hujagusia swala la amri toka juu au unamsubiri Ngosha mwenyewe ndio uje umuulize.?

Halafu Waziri anasema maswala ya kawaida huwa mnaongea vizuri tu ila maswala mazito ya kazi humwambii...Bila shaka amekufungulia mlango wa chumbani kazi kwako nategemea baada ya Muda mfupi vipindi vyako vitakuwa hewani.

Usisite kutupa update kwa utatuzi wa Changamoto zako kwa Mh. Waziri.

Yote kwa yote Nimependa utulivu wako na ujenzi wako wa hoja, Natamani siku moja kipindi Cha Kitimoto kirudi hewani bila vitisho vya amri toka juu.

Mayalla kwa kisukuma maana yake ni nini?
 
Waziri wa habari mh Mwakyembe amesema bunge la Uingereza juzi limeanza vikao kwa kuiga ubunifu wa Spika Ndugai.

Mwakyembe amesema sasa wabunge wa UK wanakaa katika chambers wakiwa wachache wachache wakiendelea na vikao vya bunge ukiwa ni ubunifu ulioasisiwa na Spika Ndugai.

Tanzania kwa sasa tumekuwa nchi ya mfano hata Rais Trump amefuata nyayo za Rais Magufuli kwa kutangaza siku maalumu ya Maombi ya kuliombea taifa.

Maendeleo hayana vyama!
Ndugai huyu aliyeruhusu mtu asiye na sifa kushiriki shughuli za bunge? Huyu ndio wa kuigwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu Waziri anasema maswala ya kawaida huwa mnaongea vizuri tu ila maswala mazito ya kazi humwambii...Bila shaka amekufungulia mlango wa chumbani kazi kwako nategemea baada ya Muda mfupi vipindi vyako vitakuwa hewani.

Usisite kutupa update kwa utatuzi wa Changamoto zako kwa Mh. Waziri.
Ina maana huenda Mayalla akarudishiwa zile tenda zake za kazi alizopokonywa?

Wamrudishie bhana, jamaa ni mtu wa watu na hana makuu.
 
Mayalla mimi nilitegemea ushauri Star TV maswali kwa Waziri yawe ana kwa ana badala ya kupokelewa na Bulendo kisha kuchambuliwa, nategemea endapo atarudi tena mtafanya hivyo na muda wa maswali uwe robotatu ya muda wa maongezi ya Waziri, mleteni aje hapa tuhangaike naye.
 
Nimemsikia waziri anasema jamii forums si chombo cha habari ni kijiwe cha wahuni,,, na awastahili kulindwa kwa sababu watoa taarifa wa jamii forums awana weredi wa habari zaid ya mitusi tu wanatukanana
Tunazidiwa hata na Wakenya wanapashana taarifa bila mitusi lakini Ss watanzania ni aibu kwa kweli....

Sent using Jamii Forums mobile app
Bahati mbaya Mayalla hakuwepo vinginevyo asingempongeza kwa hotuba mzuri yenye weredi na bashasha.
 
Pasko na Dotto mmeahidi kuja kumuita waziri siku nyingine ajibu hoja. Ukijakubali kuhojiwa tena muulize swali lifuatalo. Kuna magazeti yalisgawahi kushtakiwa mahakamani kwa uchochezi(Mwanahalisi na Mawio). Baada ya hukumu ni kuwa magazeti hayo yalishinda kesi na mahakama iliridhia yaendelee kuchapiswa lakini serikali imeyazuia. Tatizo nini? Kwanini serikali haitii maamuzi ya mahakama?

Ndiyo sababu ya kutoweka maswali ya ana kwa ana hata akishindwa kujibu hauwezi kumbana.
 
Kutoka kwa Waziri, watazamaji wamepata ufafanuzi wa kina wa masuala muhimu yanayohusu uhuru na haki ya taarifa na sekta ya habari na mawasiliano kwa ujumla. Taarifa sahihi na kamili ni nyenzo muhimu kwa wachambuzi na wadau wa siasa na habari. Ni matarajio ya wengi kwamba Waziri atapata fursa nyingine kutoa maelezo ya serikali ili kurekebisha upungufu wa taarifa unaozikabili taasisi za habari na mawasiliano nchini katika kutekeleza majukumu yake ya asili na kisasa.
 
Back
Top Bottom