LIVE: Tanzania Primier League (TPL)... Simba SC dhidi ya Kagera Sugar moja kwa moja kutokea uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

Sidhani Manula Ni mbovu kiasi hicho sema Zana anapenda Sana kupanda na kusahau majukumu yake ya kawaida, anajiona winga zaidi kuliko beki
Manula amekuwa mbovu,hayuko mchezoni,goli alilofungwa na Coastal Union na mipira iliyogonga mwamba yote hakuwa golini!
 
57' mabadiliko kwa timu ya Kagera Sugar.
anatoka Venance Ludovick, anaingia Omary Daga
 
60' Simba 0-1 Kagera Sugar
 
Kwa nini kila siku Kagera tu. Wasitufanyie upuuzi, tumekuwa wateja wa Kagera sasa.
 
63' Simba wanapata kona imechongwa na Chama, mpira unaokolewa na kipa wa Kagera Said Kipao kwa kuweka katika himaya yake
 
65' James Kotei anazawadiwa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa Kagera
 
67' Simba wanafanya shambulizi la hatari na wanakosa nafasi ya wazi

68' Zana Coulibaly wa Simba yeye na kipa anakosa nafasi ya kuisawazishi timu yake

69' Mabadiliko kwa timu ya Kagera Sugar
anatoka Paul Ngalioma, anaingia Majid Hamis.

69' Mabadiliko kwa timu ya Simba anatoka James Kotei, anaingia Jonas Mkude
 
Zana coulibaly hajui kucheza mpira ila ana mbinu za kucheza mpira, hastahili kucheza Simba
 
73' Tshabalala anapiga krosi inamfika Kagere anapiga kipa wa Kagera Said Kipao anaokoa, lakini tayari inakuwa OFFSIDE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…