Live Updates:Costal Union vs Yanga

Wamevurugwa kwa kweli, hata hivyo nimeongea na kiongozi mmoja wa Coastal Union amenihakikishia kuimaliza Yanga hiyo kesho. Vitu wanavyofanya Coastal Mazoezini wanataka kurudisha heshima waliokuwa nayo miaka ya 80-90. yanga alikuwa hatoki

Hata Aveva aliapa kuifunga Mbeya City, lakini matokeo unayo. Viongozi na wasemaji wa vilabu kama Masao Bwire na Thobias Kifaru ni wataalam wa kujigamba lakini hawaingii viwanjani kucheza. Hivyo, basi Yanga hatutishwi na maneno, tunasubiri muda tuwakandamize tuchukue pointi zetu 3.
 
Sijui kwanini mikia mmefurahia mimi kuitakia kheri Coastal, mpira ni upendo atii.
Mpende adui yako, hata Mwenyezi Mungu atakubariki pia.

Game ya kesho Yanga atashinda, iwe kwa uchochoro au barabara. Tutashinda kwa uwezo wa aliye juu, nimepataje upako sasa.
Sijarudisha kadi wala kuhamia popote, mimi ni Yanga damu, nitamalizia maisha yangu yote kuipenda Yanga.
Yanga mbele daima, nyuma mwiko.
Kila la kheri Yanga kesho Mkwakwani Tanga.
 
Mikia mnachekesha kama nini, mmekomaa na mechi haahya Yanga huku timu yenu ikiwa na kibarua pevu dhidi ya Mgambo Shooting, hamtoi mawazo ya kupata ushindi. Mmekomaa kuiombea Coastal Union ishinde. Shame in you all mikias.

Haahaa suburini dozi kesho
 
Viongozi wamepeleka timu yao ya Yanga makaburini. Kocha mzee wa watu kasema No lakini haikusaidia. Mchezaji wao Sherman nae kwenye Mwanaspoti anahojiwa anasema kulikuwa na chupa yenye maji ya ajabu iliokuwa inawafanya wakose magoli kwenye mechi na Ndanda.Professional player ana imani za kijinga kupita maelezo. Kisingizio eti ni mwafrika hana budi kuamini ushirikina.
 
Mikia mnachekesha kama nini, mmekomaa na mechi ya Yanga huku timu yenu ikiwa na kibarua pevu dhidi ya Mgambo Shooting, hamtoi mawazo ya kupata ushindi. Mmekomaa kuiombea Coastal Union ishinde. Shame in you all mikias.

Hizo ni dalili kuwa hawana imani na timu yao mkuu...
 
Kila nikiangalia ramli yangu sioni pakutokea YANGA...Wagosi tupeni raha kesho..
 
Natangaza msiba wa ndugu yetu mpendwa ndala ndefu na mazishi yatafanyika kesho kwenye viwanja vya mkwakwani...habari ziwafikie ndugu.... Makoye Matale wa kati kati ya jiji... Bantu lady akiwa pale shimoni kariakoo...bila kusahau wana ukoo wote wa Jangwani...Mungu ailaze mahala pema motoni roho ya marehemu AMEN...
 
Last edited by a moderator:



tehe tehe tehe
 
Ushindi wenu siku zote unategemea na dau mnalowapa waamuzi na uwepo wa kadi nyekundu.........
 
Ushindi wenu siku zote unategemea na dau mnalowapa waamuzi na uwepo wa kadi nyekundu.........

Ama kweli nyani haoni kundule, yaani mikia fc leo wakukaa na kusema yanga inabebwa na waamuzi!!!? hebu njoo utuambie ile penati ambayo mlipewa siku mnacheza na mbeya city ilikuwa halali? au umesahau kwa kuwa penati yenyewe iliota mbawa!!!! vipi ile tabia ya timu yenu kuwahonga wachezaji wa timu pinzani mumeiacha au wadhani kuwa watu hatuyajui haya!!! Ni afadhali unyamaze tu kama huna la kusema.
 
Sisi ni tuhuma tu hamna ushahidi wa wazi hata Azam wanatuhumiwa. Yanga kuna ushahidi. Katibu Mkuu wenu Makongoro alifungiwa maisha na CAF kwa kujaribu kumhonga refa kutoka Ethiopia kwenye mashindano ya klabu bingwa ya Africa. Hivyo Yanga mna rekodi ya kuhonga sio tuhuma.Na ndio timu ya kwanza Tanzania kiongozi kufungiwa kwa kuhonga waamuzi.
 

Ulimboka Mwakingwe wa Simba alimhonga Shaaban Kado wa Mtibwa Sugar, alikamatwa na kufunguliwa mashtaka mahakamani, unataka kutuaminisha nini wewe? Unafikiri sisi ni mambumbumbu wenzako?

Chanzo: http://www.dullonet.com/sports/2011/12/24/ulimboka-mwakingwe-apandishwa-kizimbani/
 
Ila yule refa akat Amis Tambwe hakupokea hela yetu au. Mkuu tafta kahawa utulie uone tunavyomfanya mchezo mbaya kosto
Angalia msije mkarudi Dar kwa miguu na mkayaacha magari yenu MKWAKWANI kwa mshituko wa mabao......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…