Jana alikiri safu ya ushambuliaji ya yanga ni butu mno, leo mtu mzima amewafundisha kitu. Hongera kwa Cannavaro binafsi.
Ndiyo maana kuna uzi nilisema Yanga bila yeye hakuna kitu.
Yanga mmeshinda lakini ukweli ukweli moyoni mnaujua. Timu ni mbovu mno, inacheza mpira wa kubutua bora liende, Coastal Union nao mpira wao leo ulikuwa ni mbovu mno. Kila wakati waliotea wao, mipango ya magoli hakuna ilimradi mpira uende mbele.
Ndio maana Yanga ikikutana na timu inayoweka mpira chini lazima iumie. Ukweli ndiyo huo hata ukibisha tukutane wenyewe kwa wenyewe kama kocha hajafukuzwa.