Live Updates: FC Platinum vs Simba SC, Uwanja wa Taifa - Zimbabwe

Live Updates: FC Platinum vs Simba SC, Uwanja wa Taifa - Zimbabwe

Huwa nahangaika sana sana, kuitumia .
Haha
Screenshot_20201223-120654.jpg
 
Licha ya pasi za mwisho lakini huyu Mzamiru huwa anamakosa mengi Sana pale katikati pasi nyingi huwa zinapotea kwake na huwa hawezi kabisa kubadilika kulingana na kasi ya mchezo
Nikweli,
 
Licha ya pasi za mwisho lakini huyu Mzamiru huwa anamakosa mengi Sana pale katikati pasi nyingi huwa zinapotea kwake na huwa hawezi kabisa kubadilika kulingana na kasi ya mchezo
Sasa tutambadili vipi ?!
 
CAF CHAMPIONS LEAGUE QUALIFICATIONS.

Raundi ya kwanza, mkondo wa kwanza.

(Oooh, Ataepita mikondo(aggregates) yote miwili ataingia hatua ya makundi moja kwa moja. )

10:00 JIONI: FC Platinum, Zimbabwe v Simba SC, Tanzania

UWANJA: Uwanja wa Taifa, Harare- Zimbabwe.

ITAONESHWA MUBASHARA: Azam Sports HD 1.

Na. Da Gladiator.

Patashika ya ligi ya mabingwa Afrika kufuzu hatua ya makundi, raundi ya kwanza, mkondo wa kwanza, kuendelea leo Jumatano 23, Disemba 2020. Leo zitapigwa mechi kifutu katika viwanja mbalimbali. Lakini katika uwanja wa Taifa Harare-Zimbabwe kuna bonge la mechi kati ya Simba SC, Tanzania na FC Platinum, Zimbabwe.

Hii ni baada ya mnyama huyo mkali mwituni Simba SC kuwaondosha kwa aibu raundi ya awali, mabingwa wa nchi bora, kubwa na maarufu kisoka Plateau Utd FC ya nchini Nigeria na Luis Miquisson kuibuka mchezaji bora wa mechi zote mbili na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo.

Mkondo wa kwanza.
Plateau Utd FC 0-1 Simba SC,
Goli: C C Chama, 59'.

Mkondo wa pili.
Simba 0-0 Plateau Utd FC.

Je, Simba SC ama FC Platinum kuibuka mbabe? Kaa nami/nasi usikose ukahadithiwa. Kumbuka mtanange ni kuanzia saa 10:00 jioni.

Nyongeza;

Usisahau kuwa UTO leo wanacheza mchezo wao wa kimataifa, Uwanja wa Sokoine-Mbeya, wamesafiri usiku kucha kwa basi maana mbeya ni mbali, na sidhani kama watatoka salama, maana si kwa yale madera yao .

"Kulitaka mwana, kulipewa mwana".
#SimbaNguvuMoja.
#AnotherLevel.

Karibuni kwa michango yenu.

....We jamaa bwana... Eti baada ya Simba kuiondosha kwa aibu Plateau FC kwa goli 1-0. Mnacheza sana mpira mdomoni nyie Mikia FC
 
Sasa tutambadili vipi ?!
Hatuwezi kumbadili kwasababu ndio aina yake ya uchezaji, huyu anatufaa kwenye match za nyumbani ambapo wapinzani wanakuwa under pressure wanacheza kwa tahadhari kubwa sana lakini kwa match za ugenini hapana, au kwenye ligi ya ndani hasa kwenye viwanja vya mikoani ambako anavimudu vema.
 
Hatuwezi kumbadili kwasababu ndio aina yake ya uchezaji, huyu anatufaa kwenye match za nyumbani ambapo wapinzani wanakuwa uder pressure wanacheza kwa tahadhari kubwa sana lakini kwa match za ugenini hapana, au kwenye ligi ya ndani hasa kwenye viwanja vya mikoani ambako anavimudu vema.
Duuh,
 
Mkuu nimependa maelezo yako.
 
Back
Top Bottom