. Nimeona sema huyu Breandan Rogers sioni kama ataweza kuleta vifaa na kengine siamini sababu Swansea inacheza pasi nzuri ndio Breandan Rogers atafanya LFC iwe hivyo nikujidanganya, mie sito judge sana ila nampa kuona nani ataleta na game 15 ndio nitajuwa kama jamaa anafaa muhimu Van da gaal.
Walipaswa kumrudisha Benitez,huyu sidhani kama atamaliza mkataba
rubaman ... hawa liverpool na mambo yao ya ku gamble wakiendelea nao watakuwa ni timu ya mid table kila msimu.Huyu Rodgers atakuwa kama Roy Hodgson.. makocha wanaopata mafanikio katika timu ndogo mara nyingi wanapata shida kureplicate mafanikio katika timu kubwa. Liverpool majukumu makubwa na matarajio makubwa. Swansea City walikuwa na Aim ya kubaki PL. Liverpool ni timu inayotakiwa kugombania top 4 na ubingwa, Rodgers sidhani kama ataweza kuwafanikisha hayo. Bora wangempa Van Gaal mwenye experience na CV yake imekwenda shule..
Anyway, kama mpenzi wa Arsenal nafurahia tumepoteza(tumepunguza) mpinzani mmoja wa top 4
rubaman ... hawa liverpool na mambo yao ya ku gamble wakiendelea nao watakuwa ni timu ya mid table kila msimu.
lol mmepunguza mpinzani gani wa top 4?
Haya nendeni mkajipongeze na hizo ndoto zenu halafu tukutane msimu utakapoanza. Kuwa na kocha mzoefu hakukupi guarantee ya mafanikio pia. Maana ya ku-gamble ni kuwa unaweza kupata au kukosa, sasa kuna mwingine anadai tume gamble huku akihitimisha kuwa tumepoteza tayari! Shehe yahya ametuachia warithi wake wengi kweli!Liverpool wakiendelea na jamaa huyu hadi mwisho wa msimu ujao kuna uwezekano wa kuendelea kugombea Europa League. Uhakika wa Arsenal kuendelea kucheza Champions League :lol: :lol:. Chelsea wali-gamble kwa AVB wameishia top 6, bahati yao wamebeba CL trophy.
Pazi,Hahahaha hatujawahi kulichukuwa lakini si unajua mnakosa pesa ngapi kwa kushindwa kucheza CL kwa miaka 2 sasa..Pesa zingewasaidia kukamilisha Stanley project. Afu huwezi jua tunaweza kulibeba kama timu mbovu kama Chelsea imelibeba kibahati-bahati hata sisi inaweza kutuangukia siku moja LOL. Van Persie haondoki, Euro kabla haijaisha atakuwa kashavunjika viguu vyake vya chupa nani atajiingiza mkenge kumpandia dau. :lol: :lol: :lol:
Wazeiya mupo?!!! Naona Rodgers kamsajili Fabio Borini kutoka Roma, ila nimeudhika kuondoka kwa Maxi Rodriguez, angeondoka Andy C Maxi abaki.
Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa mda mrefu sababu ya kuumia goti kulikosababisha afanyiwe upasuaji, kiungo wetu mahiri Lucas Leiva anatarajiwa kucheza katika mechi za maandalizi ya msimu mpya.
Aaaa mkuu, Long time sijakusoma, vipi shwari? Shamrashamra za kusherehekea ubingwa zimeisha? Naona babu wa man u anatia fitna kuhusiana na Van Persie mmedhamiria kumchukua kweli?pamoko mzee wa YNWA