Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Wana-Liverpool wenzangu huu sasa ni ugonjwa........naubatiza Jina la "self-esteemlessness".

Binafsi sikubaliani kabisa na mtizamo wa hapo juu kutokana na sababu hizi:

1) tayari tumeshacheza na Manure na tumemchapa. Why not hao wengine "wakubwa" ulowataja?
2) huyo unayemwita kibonde WBA alimchapa Manure (tena OT kabisa), huku sisi tukimchapa jana 4-1
3) misimu mingi huko nyuma Liverpool hupoteza points nyingi kwenye hii michezo ya mwanzoni mwa msimu. Msimu huu imekuwa tofauti...so, kwa nini tusiwe na optimism ya kufanya vizuri this season?

Mimi nina imani sana msimu tutafanya vizuri (sina uhakika na ubingwa though) iwapo:

1) pair ya SAS itakuwa injury-free kwa sehemu kubwa ya msimu. Vijana sasa hivi wako very hot!
2) Rodgers atamtumia zaidi Cotihno pale kati badala ya Henderson ili kuipa midfield yetu extra creativity. Kwa kweli mimi binafsi naungana na opinion ya Alex Ferguson kuhusu Henderson - he simply doesn't deserve to be in that red shirt!
3) mwezi January tutawauza Aspas na Henderson halafu ile bid yetu kwa Diego Costa iliyoshindwa last time sasa iwe re-submitted pale Athletico Madrid.

Tukifanikiwa hiyo ya 3 hapo juu, hata ubingwa tunaweza kuanza kuuota for once!

sasa coutihno ci ndye creative midfielder aliyeko hapa liver,na akiuzwa inakuaje? Kwa hendo mm sina tatizo akiondoka
 
Wadau, hivi tumeshaenda etihad au bado?! Wale jamaa wanatembeza vichapo kama machizi!!!
Kesho tuko na Tottenham... Muhimu sana tushinde, vinginevyo....!!
 
Liverpool is currently in fifth position... more likely we will be seven by Christmas kama tutafungwa kesho
 
Wakuu leo tupo london kupambana na wahuni wa kule spurs..tukiwa tunawakosa wachezaki wetu muhimu sana katika game kama ya leo,steven na daniel hali ni mbaya tumuombe mungu tu tupate hata droo ushindani pale juu kwenye table umekua mkali sana wapinzani wetu wote weeked hii wameshinda..macho na maskio ni saa Moja kamili...YNWA.
 
Wadau, hivi tumeshaenda etihad au bado?! Wale jamaa wanatembeza vichapo kama machizi!!!
Kesho tuko na Tottenham... Muhimu sana tushinde, vinginevyo....!!

teh teh teh goli 16 kazifunga timu tatu kubwa. man u, arsenal na spurs so kuweni makini mkikutana na hawa jamaa
 
Naam na nyie mliokua mnasumbua miaka ya 80 Kua mabingwa Mmeanza Kua Kero mitaani na kauli mbiu yenu You will never walk alone! Eti mnaota ubingwa na nyie! Leo mnapigwa mzidi kupotea!

Leo mnatembea peke yenu!
 
vipi jamani matokeo?? mbona kimya tujuzeni tulio mbali na runinga
 
Hongereni sana Liverpool hawa vibonde wa London msimu huu ni vichapo vizito.Naona kama tulivyosema Gerrard akipumzishwa Liverpool itakuwa nzuri zaidi
 
Hongereni sana...Arsenal tuna kazi sana manake kule juu kushakuwa kugumu sana
 
Naam na nyie mliokua mnasumbua miaka ya 80 Kua mabingwa Mmeanza Kua Kero mitaani na kauli mbiu yenu You will never walk alone! Eti mnaota ubingwa na nyie! Leo mnapigwa mzidi kupotea!

Leo mnatembea peke yenu!


Wee jamaa ni mtata sana! Sisi hata tukipoteza hatutembei peke yetu... vipi wewe hupendi?!
 
Club ya L'pool naipendaga sana mchezo wake na ukiifuatilia historia yake utaipenda mwenyewe tu.

Viva Liverpool FC!!!!
 
Back
Top Bottom