Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Leo ni PFA Award hii ndio my Premier League XI: 1.David de Gea bila Huyu United wangeokota mengi nyavuni 2. Azplicueta nimetizama game za Chelsea Huyu jamaa kamsaidie sana na game ya Leo na LFC nimempa heshima zake. 3. Anapigwa Luke Shaw Huyu Dogo anaweza kuchezea Chelsea au Man United mwakani! 4. kompany Huyu jamaa ni Real Captain kwa City anauwezo wa kucheza hata Middle unapomuhitaji 5.koscienly mwanzo wengi mashabiki wa Arsenal walimchoka ila jamaa amesimama Arsenal vizuri na Yule Mjerumani pale 6. Yaya Toure kila timu EPL inatamani Kuwa na mtu jembe Kama Huyu ukiwa naye Huyu wengine malizieni yenu tu 7. Eden Hazard Huyu jamaa anajuwa ku dribble na ku bend mpira weak yake ufungaji ila si kazi yake sana hawakupata natural number 9 Chelsea wa kuonekana Huyu mtu Kama ni mkali sana. 8. Ni Aaron Ramsey Kama mashabiki wake wanavyomuita Rambo hapa ningemuweka Steven Gerrad ila sababu Aaron Ramsey kaumia haitokuwa haki Huyu asingeumia Arsenal wangekuwa mbali na Pengine Huyu ndio angekuwa PFA player of the year! 9.Daniel Sturidge jamaa kajitahidi kuonyesha kipaji chake 10.Luis Suarez Goals na Assist zinajielezea PFA player of the Year 11. Ni David Silva haya ni maoni yangu tu. XI. David de Gea,Azpuliceta,kompany,koscienly,shaw,hazard,Yaya toure,Ramsey,silva,daniel sturidge,luis suarez.
 
Wakuu Biashara na nyinyi imeisha Leo! Sasa ni Mijadala huru!

Asanteni sn kwa kunogesha jukwaa!

Pamoja sn wakuu! Lv u all!
 


Nashukuru sn Mkuu na nikupe pole Mwana!

Na pia niwashukuru wote waliotoa hongera zao! Sitoweza kuwajibu kila mmoja Na niwashukuru sn ambao tumekua tunajadili juu ya hii game kwa Zaidi ya mwezi sasa!

Pamoja sn wakuu!

Nafahamu sisi Chelsea ubingwa Wa EPL ni mgumu kwetu nafasi iko Kwa City na nyie Liverpool. Chamsingi game zote mshinde na muombee city apoteze!

Mimi kwangu yoyote Yule akiwa bingwa ni sawa! Maana akili yetu na nafasi yetu ni kwenye CL.

Km kushindwa mshindwe wenyewe!

Kila laheri wakuu!
 
Last edited by a moderator:
Acha kabisa unajua ile advantage ya kuwa home ilinpa matumaini sana kiasi kwamba nikaamini chelsea wakbana sana basi matokeo itakuwa droo lakini imekuja kinyume kabisa!

hiii game hata wao chelsea mwanzo walikuwa wanajua litakuwa gum sana upande wao.

lakini walipopata gori wakapata sana nguvu aisee.
yaani tunapishana na ubingwa hivihivi hii game droo ulikuwa ni ushindi MKUBWA sana kwetu onasasa tunaanza kushinda tukiomba dua kuwa man city apoteze mechi nikitu ambacho ni ndoto zaidi game ya leo tungeshinda ndio ingekuwa tunatawazwa mabingwa
 
Jana Dan alves kaniacha hoi,mashabiki wa vilareal walimtupia ndizi kama ishara ya kumbagua,wakati anajiandaa kupiga kona,akaiokota,akaimenya ile ndizi akaila palepale,halafu akapiga ile kona,vilareal wakajifunga wenyewe,likawa goli
 
Poleni Sana wakuu BR anakwambia "there were probably two buses parked today" na statement ambayo imenikuna hii hapa aisee "Jose has got his result today credit to chelsea, ts the oposite of how we want to play. It's not difficult to coach 10 players in the 18 yard box."
 
Wakuu hayo yameshapita! Komaeni kuweka presha kwa City mpk game ya mwisho!

Mtazamo wangu: timu yenu ktk upande Wa viungo haiko sawa wakabaji na washambuliaji! Na pia Suarez na wenzake pale mbele wabadirike kabisa kwasababu ni wepesi kupotea Km wanakabwa sn. Kocha pia abadilike ktk aina ya mpira anayofundisha. Huwezi waruhusu wachezaji washambulie tuuu huku alafu kukaba wanajisahau hasa wanapokutana na timu za mafundi Km Chelsea!
 
Mkuu agosti 8 nafurahi sn kukuona ktk Uzi huu!

Naam. Sasa ni muda Wa kutoa hoja huru!

Wenzetu wanasema pengo la Henderson limeonekana Jana! Nini maoni yako hasa kwa holding midfields za liver na attacking mid? Maana kwa Mtazamo wangu kwa msimu ujao ndio wanaweza kua Vzr na Km wataongeza baadhi ya wachezaji.

Na pia nini maoni yako juu Brendan Rodgers ktk ufundishaji wake Wa mpira na aina ya mpira ambayo liver wanacheza?
 
Last edited by a moderator:
Morinho noma,kauhamisha ubingwa toka kwa Liverpool kaupeleka kwa Man city
 
Hivi kweli mlikuwa mnategemea kuifunga chelsea na hii defending yao?
 


Niliwaambia kwamba nguvu wanazotumia kutudharau tutazitumia kuwaudhi humu jukwaani.
Walinitukana sana hapa..
lakini leo wanaona aibu ..najua wanapita kusoma komenti tu lakini hawana la kusema.

LIVERPOOL FC vijogoo
CHELSEA FC Simba wa Blue.
Mosdef yuko wapi jamani?:A S cry:
 
Morinho noma,kauhamisha ubingwa toka kwa Liverpool kaupeleka kwa Man city

Mkuu Viol kawaida yetu sisi kuongea sn kabla ya game au baada ya game Km tumetoa sare au tumepoteza kwa mizengwe. Ndio huja kutoa sababu!

Lkn kwa matokeo Km ya Jana hatuna cha kuongezea Kwani Yale yote tuliyosema yametimia!

Ni hoja nyepesi tu sasaivi!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…