Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Huko promised land Caanan mbona hamfiki
Mnarandaranda tu kama Israelites kule jangwani

Subirini miaka 400πŸ˜‚
Safari ya kwenda nchi ya ahadi ni ngumu balaa. Kama alitegemea itakuwa rahisi, basi alijidangaya. Katika safari hii, milima na mabonde ni mengi. Mambo yakienda vibaya kidogo, tupo vigeugeu kibao tunamgeuka fasta, kama wale waisraeli wa Musa. Jamaa wakilala njaa jangwani kidogo tu wanalilia kurudishwa utumwani. Wakiletewa kware wawakamate wawachinje wawapike wale, wanalalamika kwa nini hao kware hawakuja wakiwa washapikwa rosti style na ugali kabisa in the first place...
 
Asije tu kuwa kama Musa
Atasota na Kanani hafiki
 
Mrithi ndio atawaingiza chaka
Oneni wenzenu Chelsea
Hahaha. Kumbuka hao kenge hawako katika safari kama yetu. Wao ni kama wanaishi nchi ya ahadi ila wakatoka kidogo kwenda shambani na kufanya mambo mengine ya kimaisha. Sasa wakati wa kurudi na ngamia zao wamekuta lango kuu limefungwa limebaki lango dogo ndilo liko wazi (yaani tundu la sindano, ambalo jamii ya kiyahudi ilikuwa inaita ule mlango mdogo wa waenda kwa miguu ndani ya milango mikbwa iliyokuwa ikitumika kwa magari na wanyama) na wao wanafosi kuingia na ngamia. Wakisimplify tu mambo wanarudi ndani fresh kabisa.
 

Mbavu ile, jamaa alikuwa anaujua. Moja ya Fullbacks waliojaaliwa balance (offensive and defensive)
 
The courtship that the Reds made to Mbappe when he was still in Monaco has never been forgotten and neither have the discussions in the private plane of the shareholders of the English club flying over the Mediterranean.

Liverpool have never broken contact with Mbappe's entourage & remain in the race to sign him.

[@lequipe]
 

Najua upo kwenye utani kuhusu Mane, ila tuongee uhalisia kwa nilichokisoma mahali jana.

Bayern walijikuta Mane ndiye top earner wao, haikuwa shida, ila ilikuwa ni kwa nini mwafrika awe top earner? Zengwe likaanza Tuchel akatumwa amwambie Mane atakuwa 3rd choice LW. Hakuitwa Mane wala wakala wake. Hivyo Bayern wanted to get rid of him.

Baadae wakasema atauzwa kwa 17M baada ya kumuona jamaa anautwanga wakasema atauzwa kwa 30M, kumbuka hawakuwa na sababu ya moja kwa moja ya kumvunjia mkataba.
 
Mambo haya yanasikitisha sana. Mtu mwenye ngozi nyeusi bado anatakiwa kuruka pale mwenzake wa ngozi nyeupe anapotembea.

Yes natania tu kuhusu kuoa kwake.
 
View attachment 2867643
[emoji23][emoji23][emoji23] Hii inamaana tuna defence nzuri?
The MoNA
MosDef
Captain Marvelous

Number don lie. Na mfumo pia ni mzuri.
Tumecheza mechi nyingi bila natural DM, tumecheza mechi kadhaa bila 1st GK, nyakati tofauti tumecheza bila Vvd, Konate and Matip, nyakati kadhaa tumemkosa TAA nyakati tofauti tumecheza bila natural LB, kwa hiyo utaona kuna defending patterns zinatubeba. Na ubora wa Beckor.
 

Kwa 21st Century kwa mfumo wa 4-4-2 hichi kikosi ni sawa kabisa.
Ila kwa mfumo wa 4-3-3 basi hapo kati ya Suarez au Torres lazima mmoja atoke ili kwenye Mido aingie mmoja kati ya Mascerano au Fabinho.

But kwa kikosi changu cha muda wote basi ni πŸ‘‡πŸ‘‡

John Barnes - I. Rush - Salah

Alonso - Gerrard - Dalglish

Robbo - VVD - Ph. Thompson - TAA

Bruce Grobbelaar

Kocha: Bob Paisley​
 
Mambo haya yanasikitisha sana. Mtu mwenye ngozi nyeusi bado anatakiwa kuruka pale mwenzake wa ngozi nyeupe anapotembea.

Yes natania tu kuhusu kuoa kwake.

Naam nimekuelewa mkuu. Umeona ishu ya Onana. Kaitwa national team lakin bado yupo klabuni na atacheza mechi mbili in a space of 24hrs. 14/1 Utd vs Spurs, 15/1 Gambia vs Cameroon. Japo kuna taarifa sijathibitisha kuwa amestaafu national team.

Chukulia hii scenario huoni kuna dalili za 10%??? Maana Eto’o alijidai mkali last AFCON akasema waliosaidia kufuzu ndio hao wataenda kupambania timu. Lakini kwa Onana hajasema chochote as of now. Je, utd hawawaamini 2nd & 3rd GK? Hili sakata unaweza kutafsiri kwa angle kadhaa na ukawa karibu na ukweli.

1. Kuna harufu ya 10% kwa ETO’O
2. Onana anahofia kupoteza nafasi yake utd.
3. Ubaguzi (ingekuwa mechi inaanza 14/1 Gambia vs Cameroon kisha 15/1 utd vs Spurs bila shaka wasingekubali acheze kutokana na uchovu).
 
View attachment 2867643
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Hii inamaana tuna defence nzuri?
The MoNA
MosDef
Captain Marvelous

Kama umekusudia kulinganisha na hao waliopo basi sisi tuna defence nzuri kuliko wao (kwa kutumia kanuni ya Lesser of the two evils).

Lakini ukiangalia in performance bila ya kulinganisha na hao wabovu basi deference yetu yetu ni mbovu kwasasababu kuconcede magoli 18 kwenye mechi 20 hapo ni karibia wastani wa kuruhusu goli 1 kila mechi jambo ambalo ni baya sana.

Kwenye mechi 20 angalau uconcede magoli 10 ndiyo unaweza kusema una defence nzuri.
 
Ishu ya Onana sijaifuatilia na kweli hata sijajua kuwa hayuko national team.

Kwa upande mwingine, tumuache abaki huku EPL maana yeye ndiye anatusaidia sisi wapinzani kujichotea points kwa manyumbu πŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…