Liverpool FC (The Reds) | Special Thread


Karata yetu kwa sasa dhidi ya Arsenal πŸ‘‡

1) Man City - Away
2) Man United - Away
3) Spurs - Away

Kuhusu Kipara hata sijui nitegemee kwa wapi ukiacha matumaini ya kutoa sare na Arsenal, hivyo tushinde mechi zetu tu.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mkuu hawa ni wazee wa false hopes, ukitaka kuenjoy burudani ya mpira basi lazima wawepo watu kama hawa mashabiki wa Arsenyani.
Watu kama hawa hata kipindi cha Jesus walikuwepo, hawa ndio waliofamta Yesu na kumuamuru ageuze vipande vya mawe kua mikate[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ni watu ambao wao hawaamini neno bali wanaamini miujiza tu.
 
Kwa mawazo yangu: Kipara anapaswa kupigwa pini/ Pep must be stopped.

Mawazo yangu yanaweza kutofautiana na Arteta ila ningekuwa Arteta ningewaza hivi:

Iko kisaikolojia...

Kutokana na sare ya Liverpool na Man City, Arsenal inaongoza ligi. Mpinzani anayefuata ni City. Arsenal inatakiwa ihakikishe inapata ushindi (mzuri tu) kwa Man City, nyumbani kwa City. Ile boost Arsenal atakayo pata kwa ushindi wa hivyo itakuwa kubwa sana. Mechi 9 zilizobaki wataenda kufanya mauaji na kubeba kombe.
 

Hii ndio ilifanya niamini kwa nini Salah hajaanzishwa pamoja na sababu nyingine.

Nahisi huwa ni tactical, plus luck pia, japo itategemea na mpinzani amekuja vipi. Na mara zote wapinzani kipindi cha kwanza huwa hawawezi kumaliza mechi.
 

Mie pia naiona hii mechi kuwa ngumu sio kwa ubora wa Man u bali upinzani wa jadi uliopo.

Everton as usual, bad lack tunamalizia away na hawa jamaa wawili. Ila ukomavu utaamua mechi hizi. Uzuri tutakuwa na full Squad kufikia huko.

We need Jota and Jones as early as possible.
 

Sijui kwa nini watu wanaona Arsenal ni mwepesi na hawezi kutwaa ubingwa. Historia ipo hapo ili kuvunjwa pia.

City msimu huu mechi nyingi hawashindi convincingly unlike last season. Bado Arsenal anaweza kubeba ubingwa vizuri sana, unavyoona Arsenal ana mechi ngumu, same na City na LFC tuna mechi ngumu vile vile. Mnaweza kuamka vibaya kama game ya Arsenal mkafungwa au draw.

Last season waligombea ubingwa kwa kuongoza muda mrefu injury ya Saliba na Draw ya Anfield ikawatoa mchezoni.

Arteta kuna alichojifunza, labda apate injuries za key players kama Klopp tuone kama yupo tayari kwa ubingwa au lah.!!! Kuna muda unapaswa kupitia situation ngumu ili kukomaa.

YNWA.
 
Everton ya siku hizi haiwawezi kwa lolote wala kwa chochote. Labda Man United.
 

Clean. Nakumbuka Klopp aligongwa fainali wee mpaka siku alipojua fainali sio ligi one match then BOOM akabadili approach yake na imekubali.

Nafikiri test aliyoipata Anfield ndio imemuwasha kipara sana, game na Arsenal kitawaka sana.

Kama mie Arteta naenda kama Underdog, namuheshimu City, nazuia kwanza kisha tucharuane kwa counter. Ila its not Arteta & Arsenal type of play. Miaka ya kuteswa na Bayern na Barca uchezaji ni ule ule. Pep kamsumbua Arteta kwa sababu uchezaji ni ule ule. Kwa hiyo nategemea Arsenal bado watafunguka. Wanaweza kufunguka na kupata point(s), ikiwa tu watakuwa na FULL AWARENESS, FOCUS & CONCENTRATION throughout the game. Wanahitaji full performance na zaidi ya hapo kuwakabili hao jamaa.

Ni mechi ambayo City watacheza do/die hata kwa msaada wa Referee.
 
dawa ni kushinda mechi zote zilizobaki iwe dhidi ya Man UTD au yeyote yule pasipokujali matokeo ya wapinzani
 
]
 

Kwa akili ya kawaida unaamini utampiga Kipara pale Etihad?

Hivi ukitoa Klopp aliyempiga City nje ndani kwenye UCL kuna Kocha mwengine aliyewahi kumpiga Kipara nje ndani?
 

Mpaka sasahivi sioni wa kumfunga Kipara pale Etihad labda Real Madrid.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…